Kwanini China na Singapore zimefaulu lakini Afrika imeshindwa kuendelea?

Kwanini China na Singapore zimefaulu lakini Afrika imeshindwa kuendelea?

Hili jambo ni kweli
Katika maana rahisi kabisa, ndani ya POLITICAL EMPIRICISM tunakutana na kitu kama "PRAGMATISM" ambacho binafsi naamini ni muhimu mno kwa siasa za Afrika, hasa kipindi hiki cha mtafuruku mkubwa wa falsafa za kidunia. Nakubaliana na wewe kwa sehemu kwamba RULE OF LAW, ACCOUNTABILITY na MERITOCRACY vina umuhimu kwenye uongozi, lakini kuikomboa jamii yetu ya Tanzania tunahutaji mbinu nyingi zaidi ya hizi tatu.
 
Inapokuja kumtawala mtu mweusi ngozi nyeupe wote lao moja.
 
Singapore na Uchina zinatawaliwa na jamii ya Hakkas/Han Chinese. Hii jamii ndiyo imekuwa ikitoa wafalme wa Uchina kwa miaka zaidi ya 2000. Raisi Deng Xiaoping wa Uchina na Lee Kuan Yew wa Singapore wote ni watu wa kabila moja, yaani Hakkas. Hii jamii kiasili ina utamaduni wa kuwekeza kwenye elimu na kujifunza tokea kipindi cha Mfalme Ha Wudin (156 B.C) alipoanzisha mitihani ya taifa ili kuweza kupata maofisa wa kuongoza serikali.

Kiufupi, Uchina haijawa jamii kongwe zaidi duniani kimazinga-ombwe au bahati-nasibu. Ukiachana na huu ushabiki maandazi ambao wengi tunalishwa kutokana na propaganda za Magharibi hasahasa Marekani, utafahamu kwamba Uchina siyo taifa la mchezo mchezo. Umetaja kitu kiitwacho MERITOCRACY, ambacho kimekuwepo Uchina kwa zaidi ya miaka 2000. Mtu unapewa nafasi ya uongozi kwasababu ya vigezo, siyo nasaba na mbeleko.

Ukifuatilia historia ya Uchina utakutana na watu aina ya Sun Tzu Wu aliyeandika (The Art of War), Confucious, Cao-Cao, Taizong ambao mbali na kuwa wanajeshi wazuri, walikuwa ni watu wenye uwezo mkubwa, nidhamu ya hali ya juu na wasomi. Sisi huku kwetu ukishajua kuongea au ukiwa mtoto wa fulani basi unapewa nafasi kubwa serikalini. Ukweli mchungu kama tukisema tutumie MERITOCRACY nchi lazima itasimama kwasababu zaidi ya asilimia 70% kuanzia Raisi wa nchi utakuta hawana vigezo vya kushika hiyo nafasi. Hivyo unaweza ukaifanya Tanzania iparanganyike ndani ya mwaka.

Hapa nakumbuka riwaya (Novel) la ISAAC ASIMOV liitwalo FOUNDATION ambapo anasema kwamba THE GALACTIC EMPIRE ilimpata mfalme aitwaye CLEON ambaye alikuwa ana kila sifa ya uongozi na mwenye akili nyingi mno. Sasa anakufa swali la msingi ni kwamba nani atakayerithi nafasi yake kuongoza ufalme wenye raia kama Trilioni 7 wanaoishi kwenye sayari mbalimbali. Ikabuniwa mbinu kwamba watoe damu ya CLEON na kutengeneza CLONES ambao watakuwa ni yeye mwenyewe ili kuendelea kuongoza ufalme. Wakatengeneza kitu kiitwacho THE GENETIC DYNASTY ambayo ilitawala kwa miaka zaidi ya 400 ikileta mafanikio makubwa mno.

Nasema hivi kwasababu kuna ukweli ambao wengi hampendi kuusikia ila ntausema. UONGOZI SIYO ASALI KWAMBA LAZIMA KILA MTU ALAMBE. Binafsi huwa naamini LEADERS ARE BORN, hayo mengine huwa ni geresha tu za ulimwengu wetu. Lakini pia, ukweli ni kwamba UCHINA na SINGAPORE hadi kufika hapo hakukuwa na kitu kiitwacho THE RULE OF LAW kama ambavyo unataka kutuaminisha hapa. Kule kulikuwa na kitu kiitwacho RULE BY LAW. Hizi nchi mbili walikubali kutoa kafara haki za binadamu na kisiasa (CIVIL & POLITICAL RIGHTS) ili waweze kupata haki za kijamii na kiuchumi (SOCIAL, CULTURAL & ECONOMIC RIGHTS).

Deng Xiaoping ndiye aliyewatandika wanafunzi wajuaji kule Tiananmen mwaka 1989, huku Lee Kuan Yew ndiye alikuwa anawashughulikia wapinzani hasahasa wale wa dini ya kiislamu wenye asili ya Malay ambao walitaka kusababisha matatizo miaka ya 60's na 70's. Singapore ni nchi iliyokaa vibaya mno kama Uchina tu. Ndani ya Singapore kuna jamii tatu, WACHINA, WAHINDI na WAMALEI. Hizi jamii zina tamaduni zake na miungu yake hivyo haziingiliani kabisa. Miaka ya 60's na 70's zilitokea vurugu kubwa za kidini na kutaka kuivuruga Singapore, Lee Kuan Yew alifikiria mbali sana kwasababu alikuwa ni mtu mwenye akili za ziada (Kiongozi anatakiwa kuwa hivi).

Ili kuondoa mikwaruzano isiyo na msingi, vyombo vya dola kama POLISI vikageuzwa NEUTRAL. Kwamba leo hii akitokea askari mwenye asili ya kichina akamuua raia mwenye asili ya kihindi au kimalei nchi haiwezi kukalika. Wakaamua kwenda kusaini mkataba na Nepal na Uingereza ili kuwaajiri THE GHURKAS REGIMENT ambao mpaka leo ndiyo polisi nchini Singapore. Ukifanya kosa nchini Singapore huwezi kuachiwa mpaka ushughulikiwe ipasavyo. Kule huwezi kusikia watu wanaleta mambo ya dini kama hapa kwetu. Ukiyaleta wanakula kichwa na unapotea mazima.

Uchina nako kuna shida kubwa. Ili kuweza kutawala jamii yenye watu zaidi ya Bilioni 1 inahitaji akili na mabavu. Hapa tutapingana lakini ukweli ndiyo huu. Historia ya Uchina inasema kwamba nchi ile huwa na kawaida ya kugawanyika na majimbo mengi kuendeshwa na makundi yanayopambana, hivyo bila kuwa na STRONG CENTRAL GOVERNMENT nchi itavurugika kabisa kama ilivyokuwa miaka ya 30's ambapo majenerali walikuwa wanamiliki majeshi yao ya kikanda na silaha za kutisha na nchi iko kwenye ANARCHY. Hivyo wanachina wanaamini kwamba FIRST YOU BUILD PROSPERITY, then PROSPERITY BUILDS YOU. Mambo kama demokrasia na haki za binadamu huja baada ya watu kushiba na kuwa na mali.

Nchi za Magharibi wanaamini yale ya falsafa za karne ya 18, kwamba HUMAN RIGHTS BRINGS ABOUT ECONOMIC PROSPERITY. Falsafa za watu aina ya John Locke wanaosema kwamba msingi wa jamii yoyote ni mali (Property) na serikali haitakiwi kuweka mkono wake, ikiweka inabidi ipinduliwe kwa kukosa uhalali. AU Jeremy Bentham wanaosema msingi wa mambo ni UTILITARIANISM, kwamba wengi wakitaka wape tu.

Afrika tukiwa tumetawaliwa na wakolini wa Magharibi hizi falsafa ndizo tunaziiga lakini hazitoi matunda yanayotakiwa. Upande mwingine wapigania uhuru wakaja na ujamaa ambao nao ulikwama kwenye baadhi ya mambo. TUFANYEJE SASA ? Tuachane na yote tuwe IMPERICISTS.

Tuchagua tuwe na kiongozi aina ya Raisi John Pombe Magufuli ambaye ni mbabe na anatumia mkono wa chuma na kutawala nchi kama familia yake, ilhali anajenga MADARAJA, RELI, MABWAWA YA UMEME, ANANUNUA NDEGE, ANATOA ELIMU YA BURE nk au tuwe na Raisi Samia Suluhu ambaye ni Laissez-Faire, anawaacha muongee ilhali anapenda CRONYSM, PATRONAGE, NEPOTISM, CAPITALISM na SIAZA ZA UKANDA ZA MIMI MZANZIBARI.

KIUKWELI TANZANIA IKO NJIA PANDA:

MERITOCRACY
haiwezekani kabisa.

ACCOUNTABILITY haiwezekani pia, hata kule Uchina na Singapore haiwezekani ndiyo maana ukizingua wanakuua tu bila huruma ili kuleta mfano kwa wengine wasifanye hicho kitu. Haya mambo tuwaachie wazungu tu ambao nao baada ya miaka 500 yanaanza kuwashinda. Nchi zao zimejaa rushwa, urasimu na matabaka makubwa mno baina ya wenye nacho na wasio nacho.

RULE OF LAW haiwezekani pia, nchi yenye watu wenye akili aina zetu kuwapa uhuru uliozidi kama ule wa Marekani ni kujitengenezea bomu tu. AV DICEY anasema lengo la utawala wa sheria ni kumfanya kila mtu awe chini ya sheria, jambo ambalo kiuhalisia ni zuri lakini haliwezekani kwetu. Wengine wameenda mbali na kusema RULE OF LAW lazima ihusishe HUMAN RIGHTS and JUST LAWS. Jambo ambalo hapa Afrika ukiliruhusu sana litaleta shida. Wewe angalia ishu ya bandari, hata yale majizi sugu ndiyo yamekuwa mstari wa mbele kujifanya mazalendo. Kule Uchina yasingefanya hivyo.
Kwa kiasi chake nimekuelewa.
 
Katika maana rahisi kabisa, ndani ya POLITICAL EMPIRICISM tunakutana na kitu kama "PRAGMATISM" ambacho binafsi naamini ni muhimu mno kwa siasa za Afrika, hasa kipindi hiki cha mtafuruku mkubwa wa falsafa za kidunia. Nakubaliana na wewe kwa sehemu kwamba RULE OF LAW, ACCOUNTABILITY na MERITOCRACY vina umuhimu kwenye uongozi, lakini kuikomboa jamii yetu ya Tanzania tunahutaji mbinu nyingi zaidi ya hizi tatu.
Yes, pia msingi wa pragmatism umechangia sana katika maendeleo ya Singapore na China toka miaka ya mwanzo ya uhuru wa Singapore mr. Lee miaka yote alisisitiza kuwa Singapore yapaswa kuendelea kutumia muelekeo wa kipragmatist katika kukabiliana na vita baridi pia katika kukabiliana na changamoto inazo ikabili Singapore.

Deng Xiaoping alikubalina na njia ya kuwa pragmatist katika vitendo hakukubaliana na dhana ya kubaki katika dhana moja hata isipo zalisha.

Deng na Lee walipendekeza kuwa yapaswa kubadilika pale njia inayotumika inashindwa kuleta matokeo yaliyo tarajiwa haipaswi kuwa viongozi wa kimawazo tu yapaswa kuwa viongozi wa vitendo kama ambavyo pragmatism inafanya kazi.
 
Yes, pia msingi wa pragmatism umechangia sana katika maendeleo ya Singapore na China toka miaka ya mwanzo ya uhuru wa Singapore mr. Lee miaka yote alisisitiza kuwa Singapore yapaswa kuendelea kutumia muelekeo wa kipragmatist katika kukabiliana na vita baridi pia katika kukabiliana na changamoto inazo ikabili Singapore.

Deng Xiaoping alikubalina na njia ya kuwa pragmatist katika vitendo hakukubaliana na dhana ya kubaki katika dhana moja hata isipo zalisha.

Deng na Lee walipendekeza kuwa yapaswa kubadilika pale njia inayotumika inashindwa kuleta matokeo yaliyo tarajiwa haipaswi kuwa viongozi wa kimawazo tu yapaswa kuwa viongozi wa vitendo kama ambavyo pragmatism inafanya kazi.
🤝🤝🤝🤝🤝🤝
 
  • Thanks
Reactions: TPP
Inapokuja kumtawala mtu mweusi ngozi nyeupe wote lao moja.
Dunia ipo katika njia ya mkubwa kumtawala au kumuonea mdogo Afrika yapaswa kukabiliana na hali hii.

Mataifa mengi ya bara la Asia yaonesha mwanga wa kukabiliana na hali hiyo. Mataifa mengi ya Afrika bado yapo dhaifu kukabiliana na hali hiyo.

Inapaswa kujengwa misingi bora ya kiutawala ili kupinga kutawaliana na kuoneana
 
Dunia ipo katika njia ya mkubwa kuntawala au kumuonea mdogo Afrika yapaswa kukabiliana na hali hii.

Bara la Asia laonesha mwanga wa kukabiliana na hali hiyo. Mataifa mengi ya Afrika bado yapo dhaifu kukabiliana na hali hiyo.

Inapaswa kujengwa misingi bora ya kiutawala ili kupinga kutawaliana na kuoneana

Kwa viongoz gani na wananchi gani? Sisi tufaa kutawiwa bwashee
 
Tatizo dini zetu zimatufunsisha ujinga
Singapore mbona zaidi ya Nusu wananchi wake ni Wakristo na waisilamu? Nchi zote za South east Asia ni za kidini na zina Maendeleo makubwa
 
So, kama meritocracy system, rule of law, accountability haiwezekani kabisa Afrika ni njia gani zitakazo wezekana Afrika katika kukabiliana na changamoto zake ?
Mkuu,
Meritocracy system ,rule of law and accountability.
Naomba ufafanuzi wa hivyo vitu.
 
Africa ni wanafiki,wabaguzi,walalamishi na udini mwingi wa kinafiq….Kamwe hawawez endelea
Malalamiko, ubaguzi, unafiki, udini hizi ni changamoto zinaipata nchi yoyote hata bara lolote.

Bara la Ulaya lakabiliwa na changamoto ya ubaguzi hio hajaweza kuwa changamoto ya kuizuia Ulaya kushindwa kupiga hatua

Mataifa mengi ya Asia yalikuwa na pia sasa kwa asilimia kadhaa yakabiliwa na changamoto ya ubaguzi na udini pia hizo hazijaweza kuwa vizuizi kwa mataifa ya Asia kushindwa kupiga hatua.

Singapore na China ilikabiliwa na changamoto hizo katika miaka ya mwanzo baada ya kuwa huru waliweza zitatua changamoto hizo na kutengeneza njia bora za kiutawala na kuweza kupiga hatua.

Meritocracy system, Rule of Law, Accountability inasaidia kuweka watu wote sawa katika taifa na kuepesha matabaka na kujenga mshikamano bora ya kihaki hivyo taifa hupiga hatua
 
mengine yoote ni theory tu, shida ni kuwaza burebure.

maendeleo huja kwa watu kufanya kazi kwa bidii na nia ya dhati kujenga nchi na kuupiga vita umasikini.
 
Usifananishe watu (China& Singapore) na sokwe wapenda ngono na starehe
Hapana. hatupaswi kufikia hatua ya kufananisha jamii moja na jamii nyengine na wanyama wa porini.

Unafikiri China na Singapore ni bora sana kuliko mataifa ya Afrika ? Hapana hata China na Singapore zilikabiliwa na changamoto nyingi miaka ya nyuma ambazo zaweza kuwa ngumu kuliko hata inazo kabili Afrika sasa lakini zimeweza piga hatua baada ya kutumia njia bora.
 
mengine yoote ni theory tu, shida ni kuwaza burebure.

maendeleo huja kwa watu kufanya kazi kwa bidii na nia ya dhati kujenga nchi na kuupiga vita umasikini.
Kufanya kazi kwa bidii bila kuwapo kwa njia bora za kiutawala matokeo tarajiwa hushindwa kutokea
 
Back
Top Bottom