Kwanini China na Singapore zimefaulu lakini Afrika imeshindwa kuendelea?

Hili jambo ni kweli
Katika maana rahisi kabisa, ndani ya POLITICAL EMPIRICISM tunakutana na kitu kama "PRAGMATISM" ambacho binafsi naamini ni muhimu mno kwa siasa za Afrika, hasa kipindi hiki cha mtafuruku mkubwa wa falsafa za kidunia. Nakubaliana na wewe kwa sehemu kwamba RULE OF LAW, ACCOUNTABILITY na MERITOCRACY vina umuhimu kwenye uongozi, lakini kuikomboa jamii yetu ya Tanzania tunahutaji mbinu nyingi zaidi ya hizi tatu.
 
Inapokuja kumtawala mtu mweusi ngozi nyeupe wote lao moja.
 
Kwa kiasi chake nimekuelewa.
 
Yes, pia msingi wa pragmatism umechangia sana katika maendeleo ya Singapore na China toka miaka ya mwanzo ya uhuru wa Singapore mr. Lee miaka yote alisisitiza kuwa Singapore yapaswa kuendelea kutumia muelekeo wa kipragmatist katika kukabiliana na vita baridi pia katika kukabiliana na changamoto inazo ikabili Singapore.

Deng Xiaoping alikubalina na njia ya kuwa pragmatist katika vitendo hakukubaliana na dhana ya kubaki katika dhana moja hata isipo zalisha.

Deng na Lee walipendekeza kuwa yapaswa kubadilika pale njia inayotumika inashindwa kuleta matokeo yaliyo tarajiwa haipaswi kuwa viongozi wa kimawazo tu yapaswa kuwa viongozi wa vitendo kama ambavyo pragmatism inafanya kazi.
 
🤝🤝🤝🤝🤝🤝
 
Reactions: TPP
Inapokuja kumtawala mtu mweusi ngozi nyeupe wote lao moja.
Dunia ipo katika njia ya mkubwa kumtawala au kumuonea mdogo Afrika yapaswa kukabiliana na hali hii.

Mataifa mengi ya bara la Asia yaonesha mwanga wa kukabiliana na hali hiyo. Mataifa mengi ya Afrika bado yapo dhaifu kukabiliana na hali hiyo.

Inapaswa kujengwa misingi bora ya kiutawala ili kupinga kutawaliana na kuoneana
 

Kwa viongoz gani na wananchi gani? Sisi tufaa kutawiwa bwashee
 
Tatizo dini zetu zimatufunsisha ujinga
Singapore mbona zaidi ya Nusu wananchi wake ni Wakristo na waisilamu? Nchi zote za South east Asia ni za kidini na zina Maendeleo makubwa
 
So, kama meritocracy system, rule of law, accountability haiwezekani kabisa Afrika ni njia gani zitakazo wezekana Afrika katika kukabiliana na changamoto zake ?
Mkuu,
Meritocracy system ,rule of law and accountability.
Naomba ufafanuzi wa hivyo vitu.
 
Africa ni wanafiki,wabaguzi,walalamishi na udini mwingi wa kinafiq….Kamwe hawawez endelea
Malalamiko, ubaguzi, unafiki, udini hizi ni changamoto zinaipata nchi yoyote hata bara lolote.

Bara la Ulaya lakabiliwa na changamoto ya ubaguzi hio hajaweza kuwa changamoto ya kuizuia Ulaya kushindwa kupiga hatua

Mataifa mengi ya Asia yalikuwa na pia sasa kwa asilimia kadhaa yakabiliwa na changamoto ya ubaguzi na udini pia hizo hazijaweza kuwa vizuizi kwa mataifa ya Asia kushindwa kupiga hatua.

Singapore na China ilikabiliwa na changamoto hizo katika miaka ya mwanzo baada ya kuwa huru waliweza zitatua changamoto hizo na kutengeneza njia bora za kiutawala na kuweza kupiga hatua.

Meritocracy system, Rule of Law, Accountability inasaidia kuweka watu wote sawa katika taifa na kuepesha matabaka na kujenga mshikamano bora ya kihaki hivyo taifa hupiga hatua
 
mengine yoote ni theory tu, shida ni kuwaza burebure.

maendeleo huja kwa watu kufanya kazi kwa bidii na nia ya dhati kujenga nchi na kuupiga vita umasikini.
 
Usifananishe watu (China& Singapore) na sokwe wapenda ngono na starehe
Hapana. hatupaswi kufikia hatua ya kufananisha jamii moja na jamii nyengine na wanyama wa porini.

Unafikiri China na Singapore ni bora sana kuliko mataifa ya Afrika ? Hapana hata China na Singapore zilikabiliwa na changamoto nyingi miaka ya nyuma ambazo zaweza kuwa ngumu kuliko hata inazo kabili Afrika sasa lakini zimeweza piga hatua baada ya kutumia njia bora.
 
mengine yoote ni theory tu, shida ni kuwaza burebure.

maendeleo huja kwa watu kufanya kazi kwa bidii na nia ya dhati kujenga nchi na kuupiga vita umasikini.
Kufanya kazi kwa bidii bila kuwapo kwa njia bora za kiutawala matokeo tarajiwa hushindwa kutokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…