Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
China na Urusi ni nchi zenye sheria kali za kudhibiti dini zote:
1. China
Nchini China, kuna aina mbili za Makanisa ya Kikristo:
(a)Makanisa yaliyosajiliwa rasmi na serikali: Haya yanasimamiwa na taasisi maalum za serikali: TSPM kwa makanisa ya Kipentekoste na Kiprotestanti na CPCA kwa Wakatoliki. Makanisa hayo yanaruhusiwa kufanya ibada lakini kwa masharti magumu, kama vile: Kuwa na wachungaji waliopitishwa na serikali, kudhibiti mahubiri yasizungumze sana kuhusu kurudi kwa Yesu, siku ya hukumu, au siasa. Yanatakiwa pia kuonyesha bendera ya taifa, picha ya Rais, na kuimba wimbo wa taifa.
Makanisa yaliyosajiliwa yanafungamana na sera za serikali ya Kikomunisti. Serikali hiyo ndiyo inayopitisha matumizi ya Biblia zilizochapishwa kwa idhini ya serikali pekee (kwa Kichina).
Baadhi ya mistari au maandiko ya Biblia hizo huchujwa, hubadilishwa au kufasiriwa kwa mtazamo wa "maadili ya kisoshalisti" au "uzalendo kwa taifa."
Kuna hata juhudi za kuandika "Biblia mpya ya Kisoshalisti", ambayo inafasiri baadhi ya mafundisho ya Yesu kwa mtazamo wa falsafa ya Kichina.
Ripoti zinasema kwamba, serikali ya China iliweka toleo lililopotoshwa, la ile habari ya Yesu na mwanamke aliyefumaniwa uzinzi(Yohana 8:1–11), ndani ya kitabu kilichotungwa kwa ajili ya wanafunzi wa sheria (law students) katika vyuo vya sheria, likionyesha kuwa Yesu alimhukumu mwanamke huyo badala ya kumsamehe, jambo ambalo si la kibiblia.
Serikali ya China ilianzisha sheria kali zaidi mnamo mwaka 2018 zinazodhibiti shughuli zote za kidini, hata zile za makanisa yaliyosajiliwa. Moja ya vipengele vyake ni kwamba: vijana walio chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki katika ibada, mafunzo ya Biblia, au shughuli yoyote ya dini.
Katika makanisa yaliyosajiliwa nchini China, kuna kamera za ufuatiliaji wa waumini.
(b)Makanisa ya "underground" au yasiyosajiliwa: Haya ni makanisa yanayokataa kusajiliwa kwa sababu: Hayataki serikali ya China iingilie imani yao na pia hayataki kuongozwa na wachungaji wa serikali. Makanisa hayo hufanya ibada kwa siri (underground churches).
Makanisa hayo hayakubaliwi kusajiliwa hata yakijaribu, kwa sababu yanashutumiwa kuwa na mafundisho "yenye ushawishi wa kigeni" au "yanayotishia mshikamano wa taifa hilo."
Wachungaji na waumini wa makanisa hayo, wakikamatwa, hunyimwa haki za kiraia, hutishiwa na wanaweza kupigwa, kuteswa na kufungwa muda mrefu.
2. Russia
Russia ina mazingira yasiyo na uhuru mkubwa wa kidini, hasa kwa madhehebu ya Kikristo yasiyokubaliwa na serikali ya nchi hiyo.
Mnamo mwaka 2016, serikali ya Russia ilipitisha sheria inayojulikana kama “Yarovaya Law”, iliyowekwa kama sehemu ya juhudi za kupambana na ugaidi. Lakini kwa uhalisia, sheria hiyo imekuwa ikitumika kuwabana zaidi Wakristo. Sheria hiyo kwa kiwango kikubwa inalenga kudhibiti imani isiyokubaliwa na Kanisa la Orthodox la Urusi, ambalo lina uhusiano wa karibu na serikali. Dini yoyote inayoonekana kama ya kigeni au yenye ushawishi wa kigeni hutazamwa kwa mashaka. Sheria hiyo inapiga marufuku mahubiri ya hadharani na kusambaza Biblia mitaani. Na hata kuhubiri katika nyumba ya mtu binafsi bila ruhusa ya serikali hilo ni kosa la kisheria.
Baadhi ya makanisa ya Kipentekoste nchini Urusi, yamepigwa marufuku kabisa, yakituhumiwa kuwa “magenge ya kidini yasiyo halali.” Viongozi wa makanisa hayo hukamatwa na kufungiwa akaunti za benki, au kupigwa faini kubwa. Watu wanaokutwa na Biblia au Maandiko ya kidini nyumbani mwao huweza kuhojiwa au kufuatiliwa. Wengine hufungiwa ibada zao au kunyimwa kufanya mikutano ya hadhara hata kama wana usajili.