Ukisoma Biblia kwa makini utaona kuwa hata watu wa Mungu waliopendwa sana kama Ayubu, Paulo, na hata Yesu mwenyewe, walipitia mateso makali, huku wengine waliomkataa Mungu wakionekana kustawi kwa muda.Ni Kama Mungu hatujibu sisi Wenye huo uhuru.. Why tunaendelea kuwa masikini zaidi ya hao wasio na huo uhuru
China na Urusi zinadhibiti uhuru wa kuabudu hata kwa watu wa imani ya kweli kama Wakristo. Ni kweli kila taifa lina utamaduni wake, lakini tunapozungumzia uhuru wa kuabudu, tunazungumzia haki ya msingi ya kiroho kwa kila mtuKila nchi inaongozwa na tamaduni zake,swali lako haliko vizuri.
Hivi na Mimi nikikuuliza kwa Nini nchi za Magharibi zina ruhusu uhuru wa wanaume kwa wanaume kuingiiana ?
Na kwa Nini pia zinaruhusu ndoa za jinsia moja?
Wakati hayo hayaruhusiwi na nchi nyingine mfano China na Urusi?
Wewe mkristo uchwara umewahi kufika Urusi ama China ukakutana na hayo ?China na Urusi ni nchi zenye sheria kali za kudhibiti dini zote:
1. China
Nchini China, kuna aina mbili za Makanisa ya Kikristo:
(a)Makanisa yaliyosajiliwa rasmi na serikali: Haya yanasimamiwa na taasisi maalum za serikali: TSPM kwa makanisa ya Kipentekoste na Kiprotestanti na CPCA kwa Wakatoliki. Makanisa hayo yanaruhusiwa kufanya ibada lakini kwa masharti magumu, kama vile: Kuwa na wachungaji waliopitishwa na serikali, kudhibiti mahubiri yasizungumze sana kuhusu kurudi kwa Yesu, siku ya hukumu, au siasa. Yanatakiwa pia kuonyesha bendera ya taifa, picha ya Rais, na kuimba wimbo wa taifa.
Makanisa yaliyosajiliwa yanafungamana na sera za serikali ya Kikomunisti. Serikali hiyo ndiyo inayopitisha matumizi ya Biblia zilizochapishwa kwa idhini ya serikali pekee (kwa Kichina).
Baadhi ya mistari au maandiko ya Biblia hizo huchujwa, hubadilishwa au kufasiriwa kwa mtazamo wa "maadili ya kisoshalisti" au "uzalendo kwa taifa."
Kuna hata juhudi za kuandika "Biblia mpya ya Kisoshalisti", ambayo inafasiri baadhi ya mafundisho ya Yesu kwa mtazamo wa falsafa ya Kichina.
Ripoti zinasema kwamba, serikali ya China iliweka toleo lililopotoshwa, la ile habari ya Yesu na mwanamke aliyefumaniwa uzinzi(Yohana 8:1–11), ndani ya kitabu kilichotungwa kwa ajili ya wanafunzi wa sheria (law students) katika vyuo vya sheria, likionyesha kuwa Yesu alimhukumu mwanamke huyo badala ya kumsamehe, jambo ambalo si la kibiblia.
Serikali ya China ilianzisha sheria kali zaidi mnamo mwaka 2018 zinazodhibiti shughuli zote za kidini, hata zile za makanisa yaliyosajiliwa. Moja ya vipengele vyake ni kwamba: vijana walio chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki katika ibada, mafunzo ya Biblia, au shughuli yoyote ya dini.
Katika makanisa yaliyosajiliwa nchini China, kuna kamera za ufuatiliaji wa waumini.
(b)Makanisa ya "underground" au yasiyosajiliwa: Haya ni makanisa yanayokataa kusajiliwa kwa sababu: Hayataki serikali ya China iingilie imani yao na pia hayataki kuongozwa na wachungaji wa serikali. Makanisa hayo hufanya ibada kwa siri (underground churches).
Makanisa hayo hayakubaliwi kusajiliwa hata yakijaribu, kwa sababu yanashutumiwa kuwa na mafundisho "yenye ushawishi wa kigeni" au "yanayotishia mshikamano wa taifa hilo."
Wachungaji na waumini wa makanisa hayo, wakikamatwa, hunyimwa haki za kiraia, hutishiwa na wanaweza kupigwa, kuteswa na kufungwa muda mrefu.
2. Russia
Russia ina mazingira yasiyo na uhuru mkubwa wa kidini, hasa kwa madhehebu ya Kikristo yasiyokubaliwa na serikali ya nchi hiyo.
Mnamo mwaka 2016, serikali ya Russia ilipitisha sheria inayojulikana kama “Yarovaya Law”, iliyowekwa kama sehemu ya juhudi za kupambana na ugaidi. Lakini kwa uhalisia, sheria hiyo imekuwa ikitumika kuwabana zaidi Wakristo. Sheria hiyo kwa kiwango kikubwa inalenga kudhibiti imani isiyokubaliwa na Kanisa la Orthodox la Urusi, ambalo lina uhusiano wa karibu na serikali. Dini yoyote inayoonekana kama ya kigeni au yenye ushawishi wa kigeni hutazamwa kwa mashaka. Sheria hiyo inapiga marufuku mahubiri ya hadharani na kusambaza Biblia mitaani. Na hata kuhubiri katika nyumba ya mtu binafsi bila ruhusa ya serikali hilo ni kosa la kisheria.
Baadhi ya makanisa ya Kipentekoste nchini Urusi, yamepigwa marufuku kabisa, yakituhumiwa kuwa “magenge ya kidini yasiyo halali.” Viongozi wa makanisa hayo hukamatwa na kufungiwa akaunti za benki, au kupigwa faini kubwa. Watu wanaokutwa na Biblia au Maandiko ya kidini nyumbani mwao huweza kuhojiwa au kufuatiliwa. Wengine hufungiwa ibada zao au kunyimwa kufanya mikutano ya hadhara hata kama wana usajili.
China na Urusi ushoga sio kosa kisheria, hakuna sheria za kupinga ushoga.Kila nchi inaongozwa na tamaduni zake,swali lako haliko vizuri.
Hivi na Mimi nikikuuliza kwa Nini nchi za Magharibi zina ruhusu uhuru wa wanaume kwa wanaume kuingiiana ?
Na kwa Nini pia zinaruhusu ndoa za jinsia moja?
Wakati hayo hayaruhusiwi na nchi nyingine mfano China na Urusi?
Kwa nini nguvu kubwa inatumika kulazimisha watu kufuata dini fulani?Zijue nchi zinazotoa adhabu kali kwa wanaobadili dini na kuwa Wakristo
Katika karne hii ya 21 ambapo ulimwengu unazungumzia uhuru wa kuabudu, bado kuna nchi kadhaa zinazotumia sheria kali, hasa za kidini, kuzuia watu kubadili dini zao. Katika nchi zifuatazo, mtu anayebadili dini na kuwa Mkristo huonekana kama msaliti, adui wa jamii, au hata mhalifu anayestahili adhabu kubwa. Hizi ni baadhi ya nchi zinazotoa adhabu kali kwa wanaomkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi:
1. Afghanistan
Mtu yeyote anayebadili dini kutoka Uislamu na kuwa Mkristo hukamatwa, kuteswa, kufungwa maisha au hata kuuawa. Watu wengi hulazimika kuficha imani yao kwa gharama yoyote, kwani jamii na serikali ya Afghanistan huona ubadilishaji huo kama kosa la usaliti dhidi ya taifa hilo na dini yao.
2. Iran
Mtu anayekiri kuwa Mkristo baada ya kutoka Uislamu huweza kushtakiwa kwa “kuchochea uasi” au “kueneza ufisadi duniani.” Hukumu yake inaweza kuwa kifungo cha muda mrefu gerezani au hata hukumu ya kifo. Wakristo waliotokea katika Uislamu huishi kwa siri, wakihofia serikali ya nchi hiyo na familia zao.
3. Saudi Arabia
Katika nchi ya Saudi Arabia, hakuna uhuru wa kidini kwa namna yoyote. Kubadili dini kutoka Uislamu na kuwa Mkristo ni kosa kubwa, na mtu anaweza kuuliwa kwa sababu hiyo chini ya "Sharia". Mikutano ya ibada za Kikristo hufanyika kwa siri, ndani ya nyumba, kwa tahadhari kubwa.
4. Somalia
Wakristo wenye asili ya Kisomali hupitia mateso makali kutoka kwa wananchi wenzao, familia, na makundi ya kijihadi kama al-Shabaab. Adhabu inaweza kuwa ni kuchapwa viboko hadharani, kufukuzwa katika familia, au kuuawa bila huruma. Wakristo nchini humo ni wachache na huishi kwa kificho.
5. Pakistan
Ingawa kuna uhuru wa dini kwa mujibu wa katiba, sheria ya kukashifu dini hutumika vibaya dhidi ya wale wanaobadili dini na kuwa Wakristo. Wanaweza kufungwa maisha au hata kuhukumiwa kifo. Mara nyingi, mashtaka ni ya uongo yanayotokana na chuki za kidini.
6. Libya
Serikali ya Libya haina udhibiti kamili wa nchi nzima kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe na mivutano ya makundi yanayogombea madaraka. Kutokana na hali hiyo ya kutokuwa na utawala imara wa sheria, "jihadist groups" kama ISIS-Libya au mengine yenye msimamo mkali huchukua nafasi hiyo kutawala maeneo fulani kwa kutumia tafsiri kali za "Sharia." Katika maeneo hayo, Wakristo wanaobadili dini au hata wageni Wakristo wanaweza kukamatwa, kuteswa, kuuliwa hadharani au kwa siri. Wakristo wengi ni wahamiaji wanaokutana na ukatili mkubwa. Huonekana kama “wazushi” au “wapelelezi kutoka nchi za magharibi.”
7. Eritrea
Nchi hiyo haina sheria kali za kidini, lakini serikali ya Eritrea imeorodheshwa kuwa miongoni mwa nchi zilizo kinyume na Wakristo wanaoabudu nje ya madhehebu yanayotambuliwa rasmi. Wengi hukamatwa bila mashtaka, kufungwa kwa miaka mingi kwenye magereza ya jangwani na chini ya ardhi.
8. North Korea
Wakristo wote nchini Korea Kaskazini, hata bila kubadili dini, wanaonekana kama tishio kwa utawala wa nchi hiyo. Mtu akiokoka na kuanza kumfuata Yesu Kristo, huweza kutupwa gerezani maisha au kuuawa mara moja, yeye pamoja na familia yake.