Kwanini China nchi ya kidikteta ina maendeleo makubwa kuliko Kenya na Zambia?

Kwanini China nchi ya kidikteta ina maendeleo makubwa kuliko Kenya na Zambia?

Hiyo hoja ya watu kukimbilia kwenye mataifa ya Magharibi huwa ni moja wapo ya hoja za kipumbavu na sijui ni kwann huwa mnaiendekeza.
Yaani utadhani nchi za Magharibi tu ndo zina wahamiaji tu hapa duniani.

Suala la mtu kutoka nchi moja kwenda nyingine mara nyingi huwa nitafuta furusa hasa za kiuchumi kwani wachina wako Marekani na Ulaya tu? Wachina siwametapakaa mpaka ndani ya nchi yetu?

Mbona Ufilipino na India ni mataifa yanayo jiita ni ya kidemokirasia lakini mamilioni ya raia wake wamejazana mashariki ya kati ambapo mataifa yote yanaongozwa kidkiteta?
Wachina walio katika nchi yenu ni wapitaji tu,
Itachukua muda mrefu sana kukueleza sababu Wahindi wamesambaa sehemu kubwa ya dunia lakini kwa wingi zaidi Marekani, Canada, Ulaya Africa na Uarabuni na huku wakiwa hawapo Russia au China.
Jifunze Historia vizuri, Philippines iliyopitia mikononi mwa Ferdinand Marcos bado ni demokrasia changa, pia ni rahisi Wafilipino masikini kwenda uarabuni kuliko Marekani.
Kuna mengi unatakiwa ujifunze.
 
Kama tumekubaliana ya kuwa democracy pekee haiwezi kukuletea maendeleo, basi kila nchi iwe huru kuchagua ni mfumo gani utakao faa kuliongoza taifa lao la msingi huo mfumo uwawezeshe raia wa nchi husika kuishi maisha mazuri.
Siku hizi hakuna nchi inayolazimishwa tena kufuata mfumo wa utawala wa nchi nyingine. Kila nchi inajiamulia mfumo wake wa utawala mradi usiue raia wako.
 
Unalosema ni kweli, yapo mambo mengine ambayo hayakuwepo ila watu waliongeza chumvi... Lakini yapo mengi sana ambayo ni ya kweli kama vile wanainchi wa Libya kutokulipa bills za umeme na maji, elimu Bure kwa ngazi zote, matibabu Bure na endapo kama Kuna ulazima wa kwenda kutibiwa nje basi serikali ndio iligharamia na wanainchi kupewa nyumba za kuishi hasa wale waliokuwa hawana uwezo.... Haya yote yalifanyika japo ni katika substandard.

Kwanza kitendo tu Cha Gaddafi kuendesha nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo Libya bila kutegemea msaada wa aina yoyote ni jambo la kishujaa sana na anastahili maua yake maana viongozi wengi wa kiafrika wameshindwa.
Waarabu wengi wa Africa Kaskazini hata hawajitambulishi sana kama Waafrika wanajiona kama sehemu ya Uarabuni zaidi au Ulaya. Halafu chukulia suala la demokrasia na udikteta kama range na sio binary.
 
Na Mimi nazidi kusisitiza kuendekeza demokrasia kwa nchi yeyote ambayo Bado inajitafuta ni kujichimbia kwenye umasikini...
Udikteta umekuwepo Africa kwa muda mrefu sana ila umaskini pamoja na vita havijawahi kuisha. Wachache walijitahidi kwa hatua angalau chache katika demokrasia kama Botswana, Senegal, Ghana, Seychelles, Namibia na Mauritius wamekuwa na afadhali kimaendeleo.
 
Demokrasia ni neno pana. Wengi wanahusisha demokrasia na uchaguzi au vyama vingi jambo ambalo ni kosa. Na pia: demokrasia bila uwajibikaji ni bure. Unakuwa na demokrasia ya corruption utegemee maendeleo?
Hakuna demokrasia ya corruption, hata China kuna ufisadi.
 
Kwanini China nchi yenye udikteta wa chama kimoja ina maendeleo makubwa kwenye nyanza mbalimbali kuliko nchi za kidemokrasia za vyama vingi kama Kenya na Zambia?

Jibu rahisi tu .. udikteta wa china ni udikteta chanya yaan wa kijamaa udikteta uko Kwenye Siasa tu.. yaan kule Hakuna mazingaombwe ya mkuu wa wilaya au sijui governer ghafla kuwa bilionea baada ya kushika ofisi ya umma kwa miaka kadhaa
china you choose your carrier play ground.. kama mfanyabiashara. Kaa mbali na siasa tena serikali Itatengeneza mazingira rafiki ya biashara zenu.. watawaletea opportunity kutoka nje ..mtaenda nje kutengeneza pesa mrudi
Ndan muwekeze kw agharama nafuu maana serikali itawapa unafuu katika nyanja mbali mbali.. ikiwemo kuwa mteja namba mmoja wa bidhaa zenu

Ila.. ukileta ujuaji sababu ushapata pesa tunakuficha tu kama Mzee wa Alibaba "jack ma"

Kama Ukichagua siasa China sahau kuwa tajiri viongoz wa kisiasa wanaishi kwa code of conduct ngumu wataishi vizuri ila hawatahodhi utajiri ..

Afrika demokrasia yetu kiini macho.. viongoz hawatoi nje kuleta ndan.. wanatoa ndan kupeleka nje au vya ndan wanawapa wagen..

Na wafanyabiashara wanashindana kuwawaweka karibu wanasiasa kuliko kuwa wabunifu wa ushindan wa kibiashara..

Ila mwisho wa yote china wameweza sababu ya aina ya utamaduni wao wa kimaisha kiasili... kuanzia ngaz ya chini.. nenda yotube angalia maisha ya wachina vijijini utaona displine ya maisha kuanzia ngaz ya chini kabisa mindset yao ni tofauti ni hardworkers, problem solvers na wabunifu sana wa kurahisha ka.. ndio mana china watu kugonga 100 years sio issue.. kuanzia tajiri had maskini

mtu akilelewa kwenye mfumo huo.. akifika kwenye daraja la juu ni rahis kufanya wonders..

Africa toka kiasili mfumo wa maisha ni greediness.. toka miaka ya enz na enz unasikia mara kuna mzee anamiliki eka 800 mara ana ng'ombe 50,000 hapa dar unaambiwa mara wazee wa kizaramo walikuwa wana eka na eka za maeneo.. ila ubunifu na productivity zero...
 
Democracy is doing well in the western world, but failed terribly in Africa.
we naww mbulula tofauti na sehemu waliyoianzisha inafanya vizuri wap Asia poor, Middle East poor, Latin america poor and Africa poorest
 
Kwanini China nchi yenye udikteta wa chama kimoja ina maendeleo makubwa kwenye nyanza mbalimbali kuliko nchi za kidemokrasia za vyama vingi kama Kenya na Zambia?
Jiulize pia Kwa Nini Tanzania nchi ya kijamaa iliyokuwa ya chama kimoja 1965-1992 na mfumo wa vyama vingi wa fake wa kuzugia 1992- 2024
Na inaongozwa ccm na bado ni masikini
 
Hapo kwenye uwajibuikaji ndipo demokrasia inapopaharibu barabara..!!
Hujui maana ya uwajibikaji? Au pengine tatizo lako ni namna ya kusimamia huo uwajibikaji ukidhani kuwa nguvu ikitumika ndiyo kutakuwa na uwajibikaji? Mbona mtu binafsi anaweza kuendesha biashara yake?
 
Siku hizi hakuna nchi inayolazimishwa tena kufuata mfumo wa utawala wa nchi nyingine. Kila nchi inajiamulia mfumo wake wa utawala mradi usiue raia wako.
Kumbe nchi za Magharibi zimejipa majukumu ya kulinda maisha ya watu wa dunia nzima sio?
Lakini mbona hii dhana ya kulinda maisha ya watu mbona hawajawahi kuitumia kwa tawala ambazo zinaendana na masilahi yao?

Kama walimvamia Gadaffi kwa sababu ya kuuwa raia , mbona hawakuivamia Misri na kumtoa Al sisi baada ya kuuwa maelfu ya waandamaji walio kuwa wakipinga kuondolewa kwa Mohammed Morsi madaraka ,badala yake ndo akawa mshirika wao?
Au mbona mpaka sasa hawajaivamia Israel na kumtoa Netanyau ambaye amesha uwa maelfu ya watoto badala yake ndo wanao mpa silaha zanazo muwezesha kufanya mauaji hayo?
Hizi fikra zako ambazo zinakufanya uone kuwa kila linalo fanywa na wamagharibi ndo halali ndo maana halisi ya utumwa wa kifikra na upumbavu.
 
Back
Top Bottom