KERO Kwanini Dar na Pwani hakuna suluhu ya kudumu ya maji safi? Miaka yote visingizio ni "Uhaba wa Mvua Ruvu"

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

DodomaTZ

Senior Member
Joined
May 20, 2022
Posts
197
Reaction score
233
photo_2025-12-12_23-01-47.jpg

Wananchi wanachoteseka Kibaha - Pwani​
Takribani mwezi mzima sasa, maeneo mengi ya Dar es Salaam na Pwani, yamekumbwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi. Kibaha - Pwani Mitaa mingi haina huduma hiyo kwa miezi kadhaa, Wananchi wanauziwa maji kwenye tenki kuanzia Sh 20,000, 25,000 hadi 30,000 kwa tenki moja la Lita 1,000 (inategemea mangapi, mfano ukinunua moja bei ni Sh 30,000, ukin unua mawili inakuwa 25,000 na ukinunua matatu inakuwa 20,000).

Tatizo hili, mbali na kuwa kero kwa Wananchi, linaibua maswali mengi kuhusu uwajibikaji wa mamlaka zinazohusika na usimamizi wa rasilimali hiyo muhimu, hususan DAWASA pamoja na wadau wengine katika sekta ya maji.

Wakati maeneo kadhaa ya jiji yakikosa maji kwa siku nyingi, hakukuwa na taarifa za mapema kutoka mamlaka hizo ambazo zingewezesha Wananchi kujiandaa dhidi ya changamoto hiyo.

Ni baada ya malalamiko kuongezeka ndipo DAWASA ilitoa taarifa ikieleza kuwepo kwa upungufu mkubwa wa maji katika chanzo kikuu cha Ruvu. Hapo ndipo tukaona pia ziara za Waziri wa Maji maeneo mbalimbali ya jiji, akitoa ufafanuzi kuwa uzalishaji wa maji kutoka Ruvu umepungua kwa zaidi ya asilimia 50, hali iliyoleta msukosuko huu.
photo_2025-12-12_13-03-42.jpg

MailiMoja - Pwani
photo_2025-12-12_16-10-04.jpg

Mbezi Makonde​
Swali muhimu la kujiuliza ni: Kwa nini mamlaka hazikutoa taarifa mapema ili kuwawezesha wananchi kujiandaa na changamoto hii? Zaidi ya hapo, karibu kila mwaka Dar es Salaam na Mikoa ya Pwani kwa jumla hukumbana na tatizo la upatikanaji wa maji na mara nyingi maelezo yanayotolewa yanahusishwa na upungufu wa mvua unaoathiri Mto Ruvu. Je, ni kweli hadi sasa hatujapata mbadala au mikakati madhubuti ya kuzuia tatizo hili kujirudia?

Cha kushangaza ni kwamba viongozi na wadau mbalimbali wamekuwa wakizungumzia mara kwa mara athari za mabadiliko ya tabianchi ikiwa ni pamoja na kupungua au kuongezeka kwa mvua, kuongezeka kwa joto, na athari nyingine. Iwapo tunatambua changamoto hizi mapema, kwa nini basi tunachelewa kufanya uwekezaji wa kutosha katika kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa uhakika?

Ni muhimu kutambua kuwa Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha shughuli za kijamii na kiuchumi; hivyo kukosekana kwa maji kunagusa moja kwa moja ustawi na maendeleo ya wananchi.
photo_2025-12-12_23-03-14.jpg

Mbezi Majogoo​
Wito wangu kwa mamlaka husika ni kwamba suala la maji halipaswi kuendeshwa kwa ubashiri. Linahitaji uwajibikaji wa dhati, mipango endelevu, na utekelezaji wa mikakati thabiti itakayotoa suluhu ya kudumu sio propaganda au ahadi zisizotekelezeka.

KIBAHA - PWANI, WENYE MADOZA WANANUNUA MAJI DAWASA KWENDA KUWAUZIA WANANCHI
Maeneo ya Kibaha Mkoani Pwani mitaa mingi haina maji ya DAWASA, hali inayowafanya Wananchi kununua kwenye madoza kwa gharama kubwa.

Wananchi wanalazimika kutumia Bodaboda kununua maji, wale wanaotaka kununua doza gharama zake ni kama nilivyosema hapo juu kuanzia Sh elfu 20 hadi 30 kwa dumu moja, jambo ambalo ni gumu kulimudu kwa Watanzani wengi wenye kipato cha chini.
photo_2025-12-12_13-01-40.jpg

Moja ya magari yanayouza tenki moja la maji Sh 20,000 hadi 30,000 Kibaha.​

Ajabu ni kuwa wanunuaji wa maji hayo wao wananunua kwenye Ofisi ya DAWASA, kwa bei ndogo ya isiyozidi Sh 3,000 kwa Tenki la Lita 1,000, lakini haohao DAWASA wanadai mitambo yao haina nguvu kusukuma maji kwenda kwa Wananchi wote waliounganishiwa huduma Kibaha.
 
Nenda Mwanza. Ziwa liko pale pale. Maji siyo ya chumvi. Mjini hakuna maji hata tone!

Nenda Morogoro. Mito kibao na mingine inapita pale mjini kabisa. Ila ukifungua bomba linatoka tope!

Sisi hatuwezi kitu!
Mkuu Watanzania hawana shida ya maji,Maji wanayo labda kwenu ndo hakuna maji!

Watanzania wao wanataka Amani
 
Kwani kuna tunachoweza mkuu? Tunachangia mbolea ya Samarinda kwa maendeleo ya dunia!
 
Huyo waziri wa maji kazi yake kupongeza wake Gen Z wakiandamana mnawapinga ngoja mkome
 
Kwa takribani mwezi mzima sasa, baadhi ya maeneo katika Jiji la Dar es Salaam yamekumbwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi.

Tatizo hili, mbali na kuwa kero kwa wananchi, linaibua maswali mengi kuhusu uwajibikaji wa mamlaka zinazohusika na usimamizi wa rasilimali hiyo muhimu, hususan DAWASA pamoja na wadau wengine katika sekta ya maji.

Wakati maeneo kadhaa ya jiji yakikosa maji kwa siku nyingi, hakukuwa na taarifa za mapema kutoka mamlaka hizo ambazo zingewezesha wananchi kujiandaa dhidi ya changamoto hiyo.

Ni baada ya malalamiko kuongezeka ndipo DAWASA ilitoa taarifa ikieleza kuwepo kwa upungufu mkubwa wa maji katika chanzo kikuu cha Ruvu. Hapo ndipo tukaona pia ziara za Waziri wa Maji maeneo mbalimbali ya jiji, akitoa ufafanuzi kuwa uzalishaji wa maji kutoka Ruvu umepungua kwa zaidi ya asilimia 50, hali iliyoleta msukosuko huu.

Swali muhimu la kujiuliza ni: Kwa nini mamlaka hazikutoa taarifa mapema ili kuwawezesha wananchi kujiandaa na changamoto hii? Zaidi ya hapo, karibu kila mwaka Dar es Salaam hukumbana na tatizo la upatikanaji wa maji na mara nyingi maelezo yanayotolewa yanahusishwa na upungufu wa mvua unaoathiri Mto Ruvu. Je, ni kweli hadi sasa hatujapata mbadala au mikakati madhubuti ya kuzuia tatizo hili kujirudia?

Cha kushangaza ni kwamba viongozi na wadau mbalimbali wamekuwa wakizungumzia mara kwa mara athari za mabadiliko ya tabianchi ikiwa ni pamoja na kupungua au kuongezeka kwa mvua, kuongezeka kwa joto, na athari nyingine. Iwapo tunatambua changamoto hizi mapema, kwa nini basi tunachelewa kufanya uwekezaji wa kutosha katika kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa uhakika?

Ni muhimu kutambua kuwa Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha shughuli za kijamii na kiuchumi; hivyo kukosekana kwa maji kunagusa moja kwa moja ustawi na maendeleo ya wananchi.

Wito wangu kwa mamlaka husika ni kwamba suala la maji halipaswi kuendeshwa kwa ubashiri. Linahitaji uwajibikaji wa dhati, mipango endelevu, na utekelezaji wa mikakati thabiti itakayotoa suluhu ya kudumu sio propaganda au ahadi zisizotekelezeka.
Mkuu wewe si umesoma? Andika proposal ipitishe kwenye proper channels. Sometimes kulalamika tu siyo suluhu unaweza kuchangia kutatua tatizo
 
Nenda Mwanza. Ziwa liko pale pale. Maji siyo ya chumvi. Mjini hakuna maji hata tone!

Nenda Morogoro. Mito kibao na mingine inapita pale mjini kabisa. Ila ukifungua bomba linatoka tope!

Sisi hatuwezi kitu!
Inasikitisha sana miaka nenda rudi shida ya Maji aitatuliwi hapa mwanza ziwa lipo ila maji bombani hakuna
 
View attachment 3514904
Wananchi wanachoteseka Kibaha - Pwani​
Takribani mwezi mzima sasa, maeneo mengi ya Dar es Salaam na Pwani, yamekumbwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi. Kibaha - Pwani Mitaa mingi haina huduma hiyo kwa miezi kadhaa, Wananchi wanauziwa maji kwenye tenki kuanzia Sh 20,000, 25,000 hadi 30,000 kwa tenki moja la Lita 1,000.

Tatizo hili, mbali na kuwa kero kwa Wananchi, linaibua maswali mengi kuhusu uwajibikaji wa mamlaka zinazohusika na usimamizi wa rasilimali hiyo muhimu, hususan DAWASA pamoja na wadau wengine katika sekta ya maji.

Wakati maeneo kadhaa ya jiji yakikosa maji kwa siku nyingi, hakukuwa na taarifa za mapema kutoka mamlaka hizo ambazo zingewezesha Wananchi kujiandaa dhidi ya changamoto hiyo.

Ni baada ya malalamiko kuongezeka ndipo DAWASA ilitoa taarifa ikieleza kuwepo kwa upungufu mkubwa wa maji katika chanzo kikuu cha Ruvu. Hapo ndipo tukaona pia ziara za Waziri wa Maji maeneo mbalimbali ya jiji, akitoa ufafanuzi kuwa uzalishaji wa maji kutoka Ruvu umepungua kwa zaidi ya asilimia 50, hali iliyoleta msukosuko huu.
View attachment 3514903
MailiMoja - Pwani
View attachment 3514906
Mbezi Makonde​
Swali muhimu la kujiuliza ni: Kwa nini mamlaka hazikutoa taarifa mapema ili kuwawezesha wananchi kujiandaa na changamoto hii? Zaidi ya hapo, karibu kila mwaka Dar es Salaam na Mikoa ya Pwani kwa jumla hukumbana na tatizo la upatikanaji wa maji na mara nyingi maelezo yanayotolewa yanahusishwa na upungufu wa mvua unaoathiri Mto Ruvu. Je, ni kweli hadi sasa hatujapata mbadala au mikakati madhubuti ya kuzuia tatizo hili kujirudia?

Cha kushangaza ni kwamba viongozi na wadau mbalimbali wamekuwa wakizungumzia mara kwa mara athari za mabadiliko ya tabianchi ikiwa ni pamoja na kupungua au kuongezeka kwa mvua, kuongezeka kwa joto, na athari nyingine. Iwapo tunatambua changamoto hizi mapema, kwa nini basi tunachelewa kufanya uwekezaji wa kutosha katika kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa uhakika?

Ni muhimu kutambua kuwa Dar es Salaam ni kitovu muhimu cha shughuli za kijamii na kiuchumi; hivyo kukosekana kwa maji kunagusa moja kwa moja ustawi na maendeleo ya wananchi.
View attachment 3514905
Mbezi Makonde​
Wito wangu kwa mamlaka husika ni kwamba suala la maji halipaswi kuendeshwa kwa ubashiri. Linahitaji uwajibikaji wa dhati, mipango endelevu, na utekelezaji wa mikakati thabiti itakayotoa suluhu ya kudumu sio propaganda au ahadi zisizotekelezeka.

KIBAHA - PWANI, WENYE MADOZA WANANUNUA MAJI DAWASA KWENDA KUWAUZIA WANANCHI
Maeneo ya Kibaha Mkoani Pwani mitaa mingi haina maji ya DAWASA, hali inayowafanya Wananchi kununua kwenye madoza kwa gharama kubwa.

Wananchi wanalazimika kutumia Bodaboda kununua maji, wale wanaotaka kununua doza gharama zake ni kama nilivyosema hapo juu kuanzia Sh elfu 20 hadi 30 kwa dumu moja, jambo ambalo ni gumu kulimudu kwa Watanzani wengi wenye kipato cha chini.
View attachment 3514902
Moja ya magari yanayouza tenki moja la maji Sh 20,000 hadi 30,000 Kibaha.​

Ajabu ni kuwa wanunuaji wa maji hayo wao wananunua kwenye Ofisi ya DAWASA, kwa bei ndogo ya isiyozidi Sh 3,000 kwa Tenki la Lita 1,000, lakini haohao DAWASA wanadai mitambo yao haina nguvu kusukuma maji kwenda kwa Wananchi wote waliounganishiwa huduma Kibaha.
Mdau watakuteka, kukutesa na hata kukufungulia kesi ya JINAI!
KISA HUTAKI AMANI NA UTULIVU!
TANGU DA MANGE AWAFUNGUE MACHO NA MASIKIO MMEKUKUWA WASUMBUFU KUDAI HAKI ZENU!
KWANI MKIENDELEA KUWA MAZOMBIE, WADANGANYIKA, MFU KUNA UBAYA GANI?!
Huduma BORA za afya, miundo mbinu, elimu, nk nk ZATAKIWA KUPEWA "ELITES' ONLY!
 
Kuna mradi wa Bwawa la Kidunda.... Umeanza sijui umefikia wapi?
 
Back
Top Bottom