Kwanini dini hizi UYAHUDI, UKRISTO na UISLAMU zinatofautiana siku ya kusali wakati chimbuko lao Moja (Abrahamic Religions)

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
Kama wote tunavyojua, Dini ni miongozo ya kiimani hapa Duniani, mafundisho yake utupa njia na namna ya kuishi hapa duniani kwa kufuata miongozo ya mnae mwabudu.

Leo nitazungumzia kwa nini siku za Kuabudu utofautiana katika kila Dini na nitajikita zaidi kwenye Dini zenye chimbuko la Ibrahimu au Abraham (Abrahamic Religions).

1. UISLAMU
Katika Uislamu, Ijumaa (Jumu'ah) inachukuliwa kuwa siku muhimu zaidi ya wiki kwa ibada, tafakari za mafundisho, na mshikamano wa Waislamu. Uchaguzi wa siku hii ya Ijumaa kama siku ya ibada ulitokana na mafundisho na desturi za Kiislamu zilizoanzishwa kipindi cha Mtume Muhammad, zikiongozwa na ufunuo wa Qur'an na Hadithi zake. Ukisoma Qur'an 62:9, Mwenyezi Mungu "Allah" anawaamuru na kuwakumbusha waislamu kuwa wakisikia adhana siku ya Ijumaa waache biashara na vitu vingine waende kumkumbuka Mwenyezi Mungu wao.

> “Enyi mlioamini, ikitangazwa adhana ya Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kumkumbuka Mwenyezi Mungu na muache biashara. Haya ni bora kwenu, lau mnajua.” (Qur'an 62:9).

Mtume Muhammad aliweka Sala ya Ijumaa ya pamoja (Salat al-Jumu'ah) kama tukio la kila wiki linalojumuisha sala, hotuba (Khutbah), na mshikamano wa Waislamu. Katika Qur'an 62:9, anayezungumza hapo ni Mwenyezi Mungu kupitia ufunuo ulioteremshwa kwa Mtume Muhammad. Waislamu wanaamini Qur'an yote ni Neno la Mwenyezi Mungu, ambalo lilifunuliwa kwa Mtume kupitia Malaika Jibril (Gabriel).

NB: Ijumaa inachukuliwa kuwa siku ya baraka ambapo matukio makubwa katika historia ya Kiislamu yalitokea, kama vile Uumbaji wa Adamu na pia kwa imani ya Kiislamu inasadikika Siku ya Kiyama inayosubiriwa itaangukia siku ya Ijumaa.

2. UYAHUDI
Wayahudi huadhimisha Jumamosi kama siku yao kuu ya ibada na kupumzika, inayojulikana kama Sabato (Shabbat). Sabato ya Kiyahudi uanza jioni ya Ijumaa, ambayo huendelea kutoka kuzama kwa jua (machweo) siku ya Ijumaa hadi usiku wa Jumamosi. Wayahudi hushiriki sala, mlo wa sherehe, na kupumzika wakati huu. Sabato inalenga zaidi Jumamosi, maandalizi na desturi huanza Ijumaa kwa Sababu katika maandiko Kisabato Siku uanza Jioni (Jua linapozama) na kumalizika kesho yake Jioni (Jua linapokaribia kuzama). Na hii ni kutokana na Maandiko ya Torati (Biblia Agano la Kale) wakati MUNGU anaumba Ulimwengu.

> “Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza" (Mwanzo 1:5)

Ukisoma kitabu cha Mwanzo sura ya kwanza mstari wa 5, kila siku ya uumbaji huanza na "jioni" na kisha "asubuhi," ikionyesha kuwa siku ya Kiyahudi huanza machweo na kuendelea hadi machweo ya siku inayofuata.

Kwa hivyo, Sabato, ambayo ni siku ya saba ya wiki, huanza machweo ya Ijumaa na kuendelea hadi machweo ya Jumamosi.

Desturi hii ya kuabudu siku ya Jumamosi inatoka katika zile Amri 10 za Mungu alizopewa Musa, ambapo Amri hiyo ni Amri ya Nne, inayopatikana katika Torah (Kutoka 20:8–11 na Kumbukumbu la Torati 5:12–15), inayosema:

> "Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana Mungu wako. Siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumishi wako wa kiume, wala mtumishi wako wa kike, wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Kwa maana kwa siku sita Bwana aliziumba mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo Bwana akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu." (Kutoka 20:8–11)

"Iishike siku ya Sabato uitakase, kama Bwana Mungu wako alivyokuamuru. Siku sita fanya kazi yako yote, lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana Mungu wako. Usifanye kazi yoyote siku hiyo, wewe wala mwanao, wala binti yako, wala mtumishi wako wa kiume, wala mtumishi wako wa kike, wala ng’ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako yeyote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumishi wako wa kiume na mtumishi wako wa kike wapate kupumzika kama wewe. Kumbuka kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na Bwana Mungu wako alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu na mkono ulionyooshwa. Kwa hiyo Bwana Mungu wako alikuamuru uishike siku ya Sabato." (Kumbukumbu la Torati 5:12–15)

Kwa mujibu wa ufahamu wa Kiyahudi, Jumamosi ni "siku ya saba" ya wiki, ikiakisi siku ambayo Mungu alipumzika baada ya kuumba dunia.

Kalenda ya Kiyahudi, ambayo imekuwepo kwa maelfu ya miaka, imetumia mzunguko wa siku saba wa wiki bila kukatizwa au kuingiliwa.

Wayahudi kote ulimwenguni wamekuwa wakiadhimisha Sabato kwa karne nyingi, wakizingatia Jumamosi kama siku ya kupumzika na ibada.

Sabato ni agano kati ya Mungu na watu wa Kiyahudi, ikionyesha uhusiano wao wa kipekee na Yeye. Kuiheshimu Sabato ni ishara ya uaminifu kwa agano hili.

Katika Torah, Mungu anasisitiza umuhimu wa Sabato katika vifungu kama Kutoka 31:16-17, vinavyosema:

> “Waisraeli wataishika Sabato, wakiisherehekea kwa vizazi vijavyo kama agano la kudumu. Itakuwa ishara kati Yangu na Waisraeli milele.” (Kutoka 31:16-17)

Hili ni Agano ambalo Mungu aliliweka kati yake na Wayahudi (Waisraeli).

2. UKRISTO
Maana ya Ukristo ni Ufuasi wa Yesu Kristo. Na Ukristo Chimbuko lake ni Uyahudi. Baada ya Wayahudi kushindwa au kukataa kumuamini Yesu, kulitokea mgawanyiko wa kiimani ambapo baadhi ya Wayahudi wakiwemo wanafunzi wa Yesu kuanza kuhubiri habari njema za Yesu baada ya Yesu kupaa mbinguni kwa mujibu wa Biblia. Ambapo miaka ya baadae wafuasi wa mafundisho ya Yesu Kristo wakatengeneza Dini ya watu wanafuata mafundisho ya Yesu Kristo ikiambatana na mafundisho ya Agano la Kale (Torati). Ukristo unaamini mafundisho ya Kiyahudi na mafundisho ya Yesu Kristo.

Katika Ukristo kuna mgawanyiko wa Siku ya kuabudu na hii ni kulingana na Madhehebu;

Siku ya Jumapili ndio utumiwa na Wakristo wengi kama siku ya kuabudu. Siku hii chimbuko lake linaanza miaka mingi saba baada ya Yesu Kondoka. Katika mwanzo, Wakristo wa mapema walikuwa Wakristo wa Kiyahudi. Hii ilimaanisha kuwa waliheshimu Sabato ya Kiyahudi, ambayo ilikuwa ni Jumamosi — siku takatifu ya mapumziko na ibada. Hata hivyo, Wakristo waliongeza mabadiliko baada ya tukio la ufufuo wa Yesu Kristo (Jumapili), ambao waliona kama kielelezo cha ushindi wa kifo na dhambi, na hivyo walijitahidi kufanya ibada ya kipekee siku ya Jumapili.

Kanisa la Kwanza la Kikristo lilianzishwa na Petro akishirikiana na James (Kaka wa Yesu). Na lilianza mara moja baada kufa na kufufuka kwa Yesu, na kanisa hilo liliitwa Church of Jerusalem.

Wakristo waliona Jumapili kama siku ya kwanza ya juma—siku ya kuanza upya, sawa na mwanzoni mwa uumbaji na ushindi wa Yesu dhidi ya kifo. Kwa hiyo, ibada ya Jumapili ilikuwa na maana kubwa zaidi kwa Wakristo, inawakilisha mabadiliko mapya na kufufuka kwa maisha kupitia Yesu Kristo.

Ingawa Wakristo wa mapema walikuwa bado wanajihusisha na Sheria ya Kiyahudi ambayo ilielekeza kutunza Sabato ya Jumamosi, siku ya Jumapili ilikua kama siku ya ibada kwa sababu ya ufufuo wa Yesu. Lakini kutumia siku ya jumapili kama Ibada ilileta shida nyingi kwa Wayahudi ambao ni Wakristo kupelekea changamoto kwa baadhi ya Wakristo ambao walikuwa wanataka kuendelea kuadhimisha Sabato kama ilivyokuwa kwa Wayahudi, kwa hofu ya kupoteza utambulisho wao wa kidini na kijamii.

Wakristo walikumbana na mateso kutoka kwa Wayahudi, hasa wale waliokuwa na maoni ya kiimani dhidi ya mabadiliko haya ya kuabudu Jumapili. Wayahudi waliokataa kumkubali Yesu kama Masiya waliona ibada ya Jumapili kama upotofu na kuikataa Sabato, hivyo walipinga kwa nguvu mabadiliko haya.

Pia Wakristo hao wa Kale walikumbana vita kali ya kuteswa kutoka kwa Dola ya Roma. Wakristo wa Kiyahudi walianza kueneza Injili ya Yesu Kristo Duniani kote, na Ukristo ukazidi kupata wafuasi kuzidi kuenea na kushirikiana na watu wa mataifa mengine, Roma ilianza kuona Ukristo kama tishio kwa amani na umoja wa kifalme wa Dola ya Kirumi. Kwa sababu ya kuabudu Mungu mmoja na kutokana na imani yao ya ufufuo wa Yesu Kristo, Wakristo walichukuliwa kuwa waasi kwa kutoabudu mfalme au mungu wa Roma (Mungu Jua yani "Sol Invictus").

Warumi walifanya kila jitihada kuua ukristo, na Wakristo walikumbana na mateso kama kupigwa, kuwekwa jela, mashambulizi ya kikatili kama vile kuuliwa kwa kuchomwa moto na kutupwa katika mapango yenye wanyama, kukamatwa kwa ajili ya burudani ya watazamaji wa Kirumi. Petro ambaye alikuwa mwanafunzi wa Yesu alifahamika kwa jina lingine la "Simon" ni miongoni wa Wakristo waliouwawa na Warumi kwa sababu ya kueneza Ukristo. Petro alisulubishwa msalabani na Warumi kisha wakaugeuza msalaba kichwa chini miguu kujuu wakidai kuwa hawezi kusulubiwa kama Yesu hivyo wao watamsulubisha kichwa chini, na inasemekana Mji wa Vatican ndipo mahali aliposulubiwa kichwa chini. Mwingine aliyeuwawa ni Mtumishi Paulo ambae kiasilia alikuwa Raia wa Kirumi, Paulo aliuwawa kwa kukatwa kichwa katika jiji la Roma ya leo.

Kwa miaka kadhaa Rumi ilizidi kugawanyika na kutengeneza utawala wa Rumi ya Magharibi na Utawala wa Rumi ya Mashariki. Rumi hizi mbili zilipigana sana ambapo baadae alitokea mfalme mmoja kutoka utawala wa Rumi ya Magharibi aliyeitwa Constantine. Kama ilivyokuwa desturi yao ya vita Constantine aliendeleza mashambulizi dhidi ya Rumi ya mashariki, mpaka usiku mmoja ambapo alipata ndoto au maono na kuona msalaba angani ulioambatana na maneno "Kwa Alama hii, Utashinda" kisha akadai Yesu alimtokea na kumuambia kuwa kupitia Msalaba atashinda vita, ambapo aliwaamuru wapiganaji wake kuchora Alama ya Msalaba kwenye mavazi yao ya kivita. Constantine baadae aliibuka kidedea kwenye vita hiyo na kutoka hapo akashawishika kuingia katika Imani ya Ukristo ambao ulipigwa vita sana miaka hile.

Kwa sababu Constantine alikuwa ni Mfalme, Mwaka wa 321 AD kwa nguvu ya ushawishi wake mkubwa alitangaza rasmi Jumapili kuwa siku ya mapumziko kwa Dola ya Roma, jambo ambalo pia lilikuza ibada ya Kikristo. Ingawa ibada ya Jumapili ilikuwa tayari ikifanywa na Wakristo, amri hii ilifanya kuwa rasmi na kutambulika zaidi ndani ya utawala wa Roma.

Ikumbukwe kuwa Sol Invictus, yani mungu wa jua wa Kirumi, nae aliheshimiwa hasa siku ya Jumapili, ambayo ilizingatiwa kuwa ni siku ya jua. Hii ilikuwa ni sehemu ya desturi pana ya Kirumi ya kutenga siku maalum za wiki kwa ajili ya miungu mbalimbali, na Jumapili ilikuwa imetengwa kwa ajili ya mungu wa jua, au Sol.

Sol Invictus ("Jua Lisiloshindwa") alikuwa mungu wa jua wa Kirumi, pia sherehe yake, inayojulikana kama Dies Natalis Solis Invicti (Siku ya Kuzaliwa ya Jua Lisiloshindwa), ilisherehekewa tarehe 25 Desemba. Tarehe hii ilichaguliwa kwa sababu inakutana kwa karibu na kipindi cha majira ya baridi, ambayo ni siku fupi zaidi na usiku mrefu zaidi wa mwaka katika Nusu ya eneo la Kaskazini ya Dunia, baada ya hapo siku huanza kuwa ndefu, ikionesha kurudi au kuzaliwa tena kwa jua.

Sherehe ya Sol Invictus tarehe 25 Desemba ilikuwa ikienziwa kabla ya sherehe ya Kikristo ya Krismasi, ambayo baadaye ilihusishwa na kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Wanazuoni wengine wanaamini kuwa uchaguzi wa tarehe 25 Desemba kwa Krismasi ulitokana na sherehe ya Sol Invictus, kwani ilikuwa tayari ni mapumziko na likizo (holiday)muhimu katika Dola la Roma wakati wa utawala wa Constantine ambaye baadae alibatizwa na kuwa Mkristo. Baada ya hapo Constantine alianza kujenga makanisa, ambapo alijenga kanisa la Church of The Holy Sepulchre kule Jerusalem na akajenga kanisa la Old Saint Peter's Basilica.

Baada ya vita ya mara kwa mara, Mnamo 395 BK, Milki ya utawala wa Kirumi iligawanywa katika sehemu mbili:

Milki ya Kirumi ya Magharibi, iliyojikita huko Roma (Italia ya leo).

Milki ya Roma ya Mashariki, iliyojikita katika Constantinople (Istanbul ya kisasa).

Mgawanyiko wa taifa la Rumi kipindi ambacho Ukristo umeshamiri ulipelekea kuzalishwa makanisa ya Katoliki la Kirumi (Roman Catholic) ambalo lilijikita katika jiji la Roma na Kanisa la Othodoksi la Mashariki (Eastern Orthodox Church) ndani ya Milki ya Kirumi ulitokana na mchanganyiko wa tofauti za kisiasa, kitamaduni, vita na lugha kwa karne nyingi ambapo Eastern Roman Empire walitumia Kigiriki kufundisha na Western Roman Empire walitumia Kilatin.

Mgawanyiko huu, unaojulikana kama Great Schism kutengeneza Ukatoliki na Uorthodox, ulitokea rasmi mwaka 1054 BK, lakini mizizi yake inaweza kufuatiliwa nyuma hadi karne za mwanzo za Ukristo.

Mgawanyiko huu uliunda mazingira tofauti ya kitamaduni na kisiasa ambayo yaliathiri maendeleo ya Ukristo katika maeneo hayo mawili.

Baadae utawala wa Kirumi ulianguka lakini Falsafa na tamaduni ziliendelea kuathiri Ukristo kwa muda mrefu kufikia wakati wa kukazalishwa harakati za Kiprotestanti. Harakati za Kiprotestanti ziliongozwa na watu kama Martin Luther, John Calvin na wengine waliokuja baadae katika karne ya 16 hatimaye yalizua na kuanzisha makanisa ya Kiprotestanti. Vuguvugu hili la Kiprotestanti lilikataa kukubaliana na tamaduni au mazoea fulani ya Kanisa Katoliki la Roma na kusababisha kuundwa kwa madhehebu mapya kama vile Ulutheri, Ukalvini, na hatimaye mengine mengi kama vile Uanglikana. Uprotestanti maana yake kwa urahisi ni hali ya kupinga na kukataa tabia na tamaduni zilizoanzishwa na kanisa la Kirumi (Roman Catholic) zinazoenda kinyume na mafundisho halali ya Ukristo.

Baada ya muda, Ukristo uligawanyika zaidi katika madhehebu mbalimbali, kutia ndani Wabaptisti, Wamethodisti, Wapentekoste, na wengine, ambao wengi wao wanafuatilia mizizi yao ya kitheolojia hadi kipindi cha harakati za matengenezo mapya ya Kanisa (protestant) na ukosoaji wake wa Kanisa Katoliki.

Madhehebu Mengi ya Kikristo kama Roman Catholic (wakatoliki), Eastern Orthodox Church, Anglican Church (Episcopal church), Lutheran Church, Baptist Church, Methodist Church, Pentecostal Church na mengineyo yanaendelea kuenzi Siku ya Jumapili kama Siku yao kuu ya Kuabudu, huku Madhehebu mengine kama Seventh-Day Adventists (Wasabato), Seventh-Day Baptists, Church of God (Seventh Day), United Church of God, Messianic Judaism (Wayahudi wa Kikristo), Hebrew Root Movements, True Jesus Church na mengineyo yakitumia siku ya Jumamosi kuabudu.

Kwa ufupi madhehebu katika Ukristo yalianzishwa kama njia ya kutafuta ukweli kuhusu mafundisho sahihi ya Biblia (Agano la jipya na Agano la kale) na tamaduni za kale za Ukristo.
 
Hata mapacha waliotoka mfuko mmoja na kufanana , kuna vitu wanatofautiana tu, Kama Ukristo na Uislam ni vitu viwili tofauti kabisa
 
Hata ukristo pia umedandia treni la uyahudi
Wokovu unataoka kwa Wayahudi

Yesu anatokea KABILA la Yuda ,ni myahudi pia

Mitume wote wayahudi

Mudi ni Muarabu wa KABILA la Quraish

Hana hata nasaba na Uyahudi ,mudi ni sawa na mwamposa wa ileje mbeya
 
Sio Kusali Tu hata Imani Ziko Tofauti..
Imani kati ya Ukristo na Uislamu Zipo karibu sana Kuliko Imani Kati ys Ukristo/Uislamu na Uyahudi..

Wayahudi wana Tamaduni na Imani ambazo huwezi zikuta kwenye Dini zote hizo mbili
Hata Uislamu wana tamaduni ambazo huwezi kuzikuta kwenye dini hizo mbili na hata ukristo pia ni hivyohivyo
 
Wokovu unataoka kwa Wayahudi

Yesu anatokea KABILA la Yuda ,ni myahudi pia

Mitume wote wayahudi

Mudi ni Muarabu wa KABILA la Quraish

Hana hata nasaba na Uyahudi ,mudi ni sawa na mwamposa wa ileje mbeya
Achana na masuala ya ukabila muhimu ni kwamba wamedandia treni kwa mbele
 
  • Thanks
Reactions: K11
Kama wote tunavyojua, Dini ni miongozo ya kiimani hapa Duniani, mafundisho yake utupa njia na namna ya kuishi hapa duniani kwa kufuata miongozo ya mnae mwabudu.

Leo nitazungumzia kwa nini siku za Kuabudu utofautiana katika kila Dini na nitajikita zaidi kwenye Dini zenye chimbuko la Ibrahimu au Abraham (Abrahamic Religions).

1. UISLAMU
Katika Uislamu, Ijumaa (Jumu'ah) inachukuliwa kuwa siku muhimu zaidi ya wiki kwa ibada, tafakari za mafundisho, na mshikamano wa Waislamu. Uchaguzi wa siku hii ya Ijumaa kama siku ya ibada ulitokana na mafundisho na desturi za Kiislamu zilizoanzishwa kipindi cha Mtume Muhammad, zikiongozwa na ufunuo wa Qur'an na Hadithi zake. Ukisoma Qur'an 62:9, Mwenyezi Mungu "Allah" anawaamuru na kuwakumbusha waislamu kuwa wakisikia adhana siku ya Ijumaa waache biashara na vitu vingine waende kumkumbuka Mwenyezi Mungu wao.

> “Enyi mlioamini, ikitangazwa adhana ya Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kumkumbuka Mwenyezi Mungu na muache biashara. Haya ni bora kwenu, lau mnajua.” (Qur'an 62:9).

Mtume Muhammad aliweka Sala ya Ijumaa ya pamoja (Salat al-Jumu'ah) kama tukio la kila wiki linalojumuisha sala, hotuba (Khutbah), na mshikamano wa Waislamu. Katika Qur'an 62:9, anayezungumza hapo ni Mwenyezi Mungu kupitia ufunuo ulioteremshwa kwa Mtume Muhammad. Waislamu wanaamini Qur'an yote ni Neno la Mwenyezi Mungu, ambalo lilifunuliwa kwa Mtume kupitia Malaika Jibril (Gabriel).

NB: Ijumaa inachukuliwa kuwa siku ya baraka ambapo matukio makubwa katika historia ya Kiislamu yalitokea, kama vile Uumbaji wa Adamu na pia kwa imani ya Kiislamu inasadikika Siku ya Kiyama inayosubiriwa itaangukia siku ya Ijumaa.

2. UYAHUDI
Wayahudi huadhimisha Jumamosi kama siku yao kuu ya ibada na kupumzika, inayojulikana kama Sabato (Shabbat). Sabato ya Kiyahudi uanza jioni ya Ijumaa, ambayo huendelea kutoka kuzama kwa jua (machweo) siku ya Ijumaa hadi usiku wa Jumamosi. Wayahudi hushiriki sala, mlo wa sherehe, na kupumzika wakati huu. Sabato inalenga zaidi Jumamosi, maandalizi na desturi huanza Ijumaa kwa Sababu katika maandiko Kisabato Siku uanza Jioni (Jua linapozama) na kumalizika kesho yake Jioni (Jua linapokaribia kuzama). Na hii ni kutokana na Maandiko ya Torati (Biblia Agano la Kale) wakati MUNGU anaumba Ulimwengu.

> “Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza" (Mwanzo 1:5)

Ukisoma kitabu cha Mwanzo sura ya kwanza mstari wa 5, kila siku ya uumbaji huanza na "jioni" na kisha "asubuhi," ikionyesha kuwa siku ya Kiyahudi huanza machweo na kuendelea hadi machweo ya siku inayofuata.

Kwa hivyo, Sabato, ambayo ni siku ya saba ya wiki, huanza machweo ya Ijumaa na kuendelea hadi machweo ya Jumamosi.

Desturi hii ya kuabudu siku ya Jumamosi inatoka katika zile Amri 10 za Mungu alizopewa Musa, ambapo Amri hiyo ni Amri ya Nne, inayopatikana katika Torah (Kutoka 20:8–11 na Kumbukumbu la Torati 5:12–15), inayosema:

> "Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana Mungu wako. Siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumishi wako wa kiume, wala mtumishi wako wa kike, wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Kwa maana kwa siku sita Bwana aliziumba mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo Bwana akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu." (Kutoka 20:8–11)

Kwa mujibu wa ufahamu wa Kiyahudi, Jumamosi ni "siku ya saba" ya wiki, ikiakisi siku ambayo Mungu alipumzika baada ya kuumba dunia.

Kalenda ya Kiyahudi, ambayo imekuwepo kwa maelfu ya miaka, imetumia mzunguko wa siku saba wa wiki bila kukatizwa au kuingiliwa.

Wayahudi kote ulimwenguni wamekuwa wakiadhimisha Sabato kwa karne nyingi, wakizingatia Jumamosi kama siku ya kupumzika na ibada.

Sabato ni agano kati ya Mungu na watu wa Kiyahudi, ikionyesha uhusiano wao wa kipekee na Yeye. Kuiheshimu Sabato ni ishara ya uaminifu kwa agano hili.

Katika Torah, Mungu anasisitiza umuhimu wa Sabato katika vifungu kama Kutoka 31:16-17, vinavyosema:

> “Waisraeli wataishika Sabato, wakiisherehekea kwa vizazi vijavyo kama agano la kudumu. Itakuwa ishara kati Yangu na Waisraeli milele.” (Kutoka 31:16-17)

Hili ni Agano ambalo Mungu aliliweka kati yake na Wayahudi (Waisraeli).

2. UKRISTO
Maana ya Ukristo ni Ufuasi wa Yesu Kristo. Na Ukristo Chimbuko lake ni Uyahudi. Baada ya Wayahudi kushindwa au kukataa kumuamini Yesu, kulitokea mgawanyiko wa kiimani ambapo baadhi ya Wayahudi wakiwemo wanafunzi wa Yesu kuanza kuhubiri habari njema za Yesu baada ya Yesu kupaa mbinguni kwa mujibu wa Biblia. Ambapo miaka ya baadae wafuasi wa mafundisho ya Yesu Kristo wakatengeneza Dini ya watu wanafuata mafundisho ya Yesu Kristo ikiambatana na mafundisho ya Agano la Kale (Torati). Ukristo unaamini mafundisho ya Kiyahudi na mafundisho ya Yesu Kristo.

Katika Ukristo kuna mgawanyiko wa Siku ya kuabudu na hii ni kulingana na Madhehebu;

Siku ya Jumapili ndio utumiwa na Wakristo wengi kama siku ya kuabudu. Siku hii chimbuko lake linaanza miaka mingi saba baada ya Yesu Kondoka. Katika mwanzo, Wakristo wa mapema walikuwa Wakristo wa Kiyahudi. Hii ilimaanisha kuwa waliheshimu Sabato ya Kiyahudi, ambayo ilikuwa ni Jumamosi — siku takatifu ya mapumziko na ibada. Hata hivyo, Wakristo waliongeza mabadiliko baada ya tukio la ufufuo wa Yesu Kristo (Jumapili), ambao waliona kama kielelezo cha ushindi wa kifo na dhambi, na hivyo walijitahidi kufanya ibada ya kipekee siku ya Jumapili.

Kanisa la Kwanza la Kikristo lilianzishwa na Petro akishirikiana na James (Kaka wa Yesu). Na lilianza mara moja baada kufa na kufufuka kwa Yesu, na kanisa hilo liliitwa Church of Jerusalem.

Wakristo waliona Jumapili kama siku ya kwanza ya juma—siku ya kuanza upya, sawa na mwanzoni mwa uumbaji na ushindi wa Yesu dhidi ya kifo. Kwa hiyo, ibada ya Jumapili ilikuwa na maana kubwa zaidi kwa Wakristo, inawakilisha mabadiliko mapya na kufufuka kwa maisha kupitia Yesu Kristo.

Ingawa Wakristo wa mapema walikuwa bado wanajihusisha na Sheria ya Kiyahudi ambayo ilielekeza kutunza Sabato ya Jumamosi, siku ya Jumapili ilikua kama siku ya ibada kwa sababu ya ufufuo wa Yesu. Lakini kutumia siku ya jumapili kama Ibada ilileta shida nyingi kwa Wayahudi ambao ni Wakristo kupelekea changamoto kwa baadhi ya Wakristo ambao walikuwa wanataka kuendelea kuadhimisha Sabato kama ilivyokuwa kwa Wayahudi, kwa hofu ya kupoteza utambulisho wao wa kidini na kijamii.

Wakristo walikumbana na mateso kutoka kwa Wayahudi, hasa wale waliokuwa na maoni ya kiimani dhidi ya mabadiliko haya ya kuabudu Jumapili. Wayahudi waliokataa kumkubali Yesu kama Masiya waliona ibada ya Jumapili kama upotofu na kuikataa Sabato, hivyo walipinga kwa nguvu mabadiliko haya.

Pia Wakristo hao wa Kale walikumbana vita kali ya kuteswa kutoka kwa Dola ya Roma. Wakristo wa Kiyahudi walianza kueneza Injili ya Yesu Kristo Duniani kote, na Ukristo ukazidi kupata wafuasi kuzidi kuenea na kushirikiana na watu wa mataifa mengine, Roma ilianza kuona Ukristo kama tishio kwa amani na umoja wa kifalme wa Dola ya Kirumi. Kwa sababu ya kuabudu Mungu mmoja na kutokana na imani yao ya ufufuo wa Yesu Kristo, Wakristo walichukuliwa kuwa waasi kwa kutoabudu mfalme au mungu wa Roma (Mungu Jua yani "Sol Invictus").

Warumi walifanya kila jitihada kuua ukristo, na Wakristo walikumbana na mateso kama kupigwa, kuwekwa jela, mashambulizi ya kikatili kama vile kuuliwa kwa kuchomwa moto na kutupwa katika mapango yenye wanyama, kukamatwa kwa ajili ya burudani ya watazamaji wa Kirumi. Petro ambaye alikuwa mwanafunzi wa Yesu alifahamika kwa jina lingine la "Simon" ni miongoni wa Wakristo waliouwawa na Warumi kwa sababu ya kueneza Ukristo. Petro alisulubishwa msalabani na Warumi kisha wakaugeuza msalaba kichwa chini miguu kujuu wakidai kuwa hawezi kusulubiwa kama Yesu hivyo wao watamsulubisha kichwa chini, na inasemekana Mji wa Vatican ndipo mahali aliposulubiwa kichwa chini. Mwingine aliyeuwawa ni Mtumishi Paulo ambae kiasilia alikuwa Raia wa Kirumi, Paulo aliuwawa kwa kukatwa kichwa katika jiji la Roma ya leo.

Kwa miaka kadhaa Rumi ilizidi kugawanyika na kutengeneza utawala wa Rumi ya Magharibi na Utawala wa Rumi ya Mashariki. Rumi hizi mbili zilipigana sana ambapo baadae alitokea mfalme mmoja kutoka utawala wa Rumi ya Magharibi aliyeitwa Constantine. Kama ilivyokuwa desturi yao ya vita Constantine aliendeleza mashambulizi dhidi ya Rumi ya mashariki, mpaka usiku mmoja ambapo alipata ndoto au maono na kuona msalaba angani ulioambatana na maneno "Kwa Alama hii, Utashinda" kisha akadai Yesu alimtokea na kumuambia kuwa kupitia Msalaba atashinda vita, ambapo aliwaamuru wapiganaji wake kuchora Alama ya Msalaba kwenye mavazi yao ya kivita. Constantine baadae aliibuka kidedea kwenye vita hiyo na kutoka hapo akashawishika kuingia katika Imani ya Ukristo ambao ulipigwa vita sana miaka hile.

Kwa sababu Constantine alikuwa ni Mfalme, Mwaka wa 321 AD kwa nguvu ya ushawishi wake mkubwa alitangaza rasmi Jumapili kuwa siku ya mapumziko kwa Dola ya Roma, jambo ambalo pia lilikuza ibada ya Kikristo. Ingawa ibada ya Jumapili ilikuwa tayari ikifanywa na Wakristo, amri hii ilifanya kuwa rasmi na kutambulika zaidi ndani ya utawala wa Roma.

Ikumbukwe kuwa Sol Invictus, yani mungu wa jua wa Kirumi, nae aliheshimiwa hasa siku ya Jumapili, ambayo ilizingatiwa kuwa ni siku ya jua. Hii ilikuwa ni sehemu ya desturi pana ya Kirumi ya kutenga siku maalum za wiki kwa ajili ya miungu mbalimbali, na Jumapili ilikuwa imetengwa kwa ajili ya mungu wa jua, au Sol.

Sol Invictus ("Jua Lisiloshindwa") alikuwa mungu wa jua wa Kirumi, pia sherehe yake, inayojulikana kama Dies Natalis Solis Invicti (Siku ya Kuzaliwa ya Jua Lisiloshindwa), ilisherehekewa tarehe 25 Desemba. Tarehe hii ilichaguliwa kwa sababu inakutana kwa karibu na kipindi cha majira ya baridi, ambayo ni siku fupi zaidi na usiku mrefu zaidi wa mwaka katika Nusu ya eneo la Kaskazini ya Dunia, baada ya hapo siku huanza kuwa ndefu, ikionesha kurudi au kuzaliwa tena kwa jua.

Sherehe ya Sol Invictus tarehe 25 Desemba ilikuwa ikienziwa kabla ya sherehe ya Kikristo ya Krismasi, ambayo baadaye ilihusishwa na kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Wanazuoni wengine wanaamini kuwa uchaguzi wa tarehe 25 Desemba kwa Krismasi ulitokana na sherehe ya Sol Invictus, kwani ilikuwa tayari ni mapumziko na likizo (holiday)muhimu katika Dola la Roma wakati wa utawala wa Constantine ambaye baadae alibatizwa na kuwa Mkristo. Baada ya hapo Constantine alianza kujenga makanisa, ambapo alijenga kanisa la Church of The Holy Sepulchre kule Jerusalem na akajenga kanisa la Old Saint Peter's Basilica.

Baada ya vita ya mara kwa mara, Mnamo 395 BK, Milki ya utawala wa Kirumi iligawanywa katika sehemu mbili:

Milki ya Kirumi ya Magharibi, iliyojikita huko Roma (Italia ya leo).

Milki ya Roma ya Mashariki, iliyojikita katika Constantinople (Istanbul ya kisasa).

Mgawanyiko wa taifa la Rumi kipindi ambacho Ukristo umeshamiri ulipelekea kuzalishwa makanisa ya Katoliki la Kirumi (Roman Catholic) ambalo lilijikita katika jiji la Roma na Kanisa la Othodoksi la Mashariki (Eastern Orthodox Church) ndani ya Milki ya Kirumi ulitokana na mchanganyiko wa tofauti za kisiasa, kitamaduni, vita na lugha kwa karne nyingi ambapo Eastern Roman Empire walitumia Kigiriki kufundisha na Western Roman Empire walitumia Kilatin.

Mgawanyiko huu, unaojulikana kama Great Schism kutengeneza Ukatoliki na Uorthodox, ulitokea rasmi mwaka 1054 BK, lakini mizizi yake inaweza kufuatiliwa nyuma hadi karne za mwanzo za Ukristo.

Mgawanyiko huu uliunda mazingira tofauti ya kitamaduni na kisiasa ambayo yaliathiri maendeleo ya Ukristo katika maeneo hayo mawili.

Baadae utawala wa Kirumi ulianguka lakini Falsafa na tamaduni ziliendelea kuathiri Ukristo kwa muda mrefu kufikia wakati wa kukazalishwa harakati za Kiprotestanti. Harakati za Kiprotestanti ziliongozwa na watu kama Martin Luther, John Calvin na wengine waliokuja baadae katika karne ya 16 hatimaye yalizua na kuanzisha makanisa ya Kiprotestanti. Vuguvugu hili la Kiprotestanti lilikataa kukubaliana na tamaduni au mazoea fulani ya Kanisa Katoliki la Roma na kusababisha kuundwa kwa madhehebu mapya kama vile Ulutheri, Ukalvini, na hatimaye mengine mengi kama vile Uanglikana. Uprotestanti maana yake kwa urahisi ni hali ya kupinga na kukataa tabia na tamaduni zilizoanzishwa na kanisa la Kirumi (Roman Catholic) zinazoenda kinyume na mafundisho halali ya Ukristo.

Baada ya muda, Ukristo uligawanyika zaidi katika madhehebu mbalimbali, kutia ndani Wabaptisti, Wamethodisti, Wapentekoste, na wengine, ambao wengi wao wanafuatilia mizizi yao ya kitheolojia hadi kipindi cha harakati za matengenezo mapya ya Kanisa (protestant) na ukosoaji wake wa Kanisa Katoliki.

Madhehebu Mengi ya Kikristo kama Roman Catholic (wakatoliki), Eastern Orthodox Church, Anglican Church (Episcopal church), Lutheran Church, Baptist Church, Methodist Church, Pentecostal Church na mengineyo yanaendelea kuenzi Siku ya Jumapili kama Siku yao kuu ya Kuabudu, huku Madhehebu mengine kama Seventh-Day Adventists (Wasabato), Seventh-Day Baptists, Church of God (Seventh Day), United Church of God, Messianic Judaism (Wayahudi wa Kikristo), Hebrew Root Movements, True Jesus Church na mengineyo yakitumia siku ya Jumamosi kuabudu.

Kwa ufupi madhehebu katika Ukristo yalianzishwa kama njia ya kutafuta ukweli kuhusu mafundisho sahihi ya Biblia (Agano la jipya na Agano la kale) na tamaduni za kale za Ukristo.
Tuna pishana masaa na miaka.
Ukienda kwa waislamu wana kalenda zao ,bado wapo mwaka hata afrika ijaingia kugawanya nchi.

Ukija kwa wachina nao no hivo hivo .
Wa kristo tunafata sijui ile ya waroma kalenda
 
Jua = Nuru ya Ulimwengu = Yesu

Yohana 8
12. Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.

Walichokuwa wanakifanya wapagani kuabudu Jua hili linaloonekana Enzi hizo walikuwa sawa.
Jambo jema walililofanya ni kubadilika kutoka kuabudu Jua linaloonekana mpaka kuabudu Jua lisiloonekana ambaye ni Kristo.
 
Waislamu wanatia udhu wakati wengine hawatii udhu...
Una Uhakika Kuwa Wengine hawatii wudhu?

Wayahudi kabla ya Kufanya Ibada yoyote Takatifu kkiwemo Kuingia Hekaluni au Sinagogini au Kula Hunawa Baadhi ya Viungo vyao Ikiwemo Mkono huku wakitamka Maneno ya Baraka kitendo Kile cha Kunawa Huitwa Netilat Yadayim (נטילת ידיים),

na wanatumia Chombo maalumu na Utaratibu maalumu kama Inavyofanywa kwenye Wudhu..

Wakristo Hawafanyi Ila waliamrishwa Kufanya Na Yesu!
Soma Yohana 13:5-10
Screenshot_20250310_075530_Biblia Takatifu.jpg

Hapo Mpaka Yesu anafundisha Kuhusu Utofauti wa Wudhu (Kutawadha) na Kuoga (Kogo la wajibu) na anasema aliyeoga hana Haja ya Kutawadha.. nahisi Hata Waislamu wengi badi hawajui Ukioga Kogo la wajibu Si lazima Tena Uchukue Udhu..

Nahisi unaweza Kuniuliza Tena Kuhusu Kuoga Kulifundishwa Wapi..ndyo kuoga Janaba Kulifundishwa Zamani za Musa na Ndiyo ilikuwa Desturi..

Mambo ya Walawi 15:16-18
Screenshot_20250310_080055_Biblia Takatifu.jpg

NA kwa Kusema Hayo Bado hujaniambia kuhusu Tamaduni ya Kiislamu au Dini yoyote kama Nilivyosema hapo Juu....
 
Jua = Nuru ya Ulimwengu = Yesu

Yohana 8
12. Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.

Walichokuwa wanakifanya wapagani kuabudu Jua hili linaloonekana Enzi hizo walikuwa sawa.
Jambo jema walililofanya ni kubadilika kutoka kuabudu Jua linaloonekana mpaka kuabudu Jua lisiloonekana ambaye ni Kristo.
Good Point!
But Usisahau Kuwa Hata Shetani Ni Jua Pia!
Neno Lucifer Limetumika kwa Yesu na Kwa Shetani vile vile kwahyo ni neno Lenye maana Sawa ial Tofauti ni maana..

Lucifer=Light bringer=Mleta Nuru
 
Back
Top Bottom