Kwanini Dkt. Bashiru aseme anathibitisha kwamba, asiseme anaapa kwamba?

Kwanini Dkt. Bashiru aseme anathibitisha kwamba, asiseme anaapa kwamba?

Nashukuru kwa ufafanuzi huu ila najaribu kuangalia viongozi wengi wa dini zote wanatumia naapa kwamba, je ni kutokujua? Je jeshini napo wanaapa au wanathibitisha?

Pale wanapoapa kiapo kimoja mtu zaidi ya mmoja mbona sijawahi kusikia wakithibitisha? Rejea viapo vya kijeshi,
 
Hata waziri ofisi ya Rais Utawala bora mh Mchengerwa alisema "nathibitisha".
 
Nashukuru kwa ufafanuzi huu , ila najaribu kuangalia viongozi wengi wa dini zote wanatumia naapa kwamba, je nikutokujua? Je jeshini napo wanaapa au wanathibitisha?

Pale wanapoapa kiapo kimoja mtu zaidi ya mmoja mbona sijawahi kusikia wakithibitisha? Rejea viapo vya kijeshi,
Wote hupewa kiapo kikiwa na neno
Naapa/nathibistha ikiwa na maana kwamba akifika sehemu ya kusema naapa .......kama ni mkristo atatamka hivyo
Halafu akiwa Muislam atasema nathibitisha.....
Hivyo.
 
Hv kosa la huyu mtu Ni lipi mpk watu wamefirahi hvyo
Wewe mkuu unaishi wapi? Huyu ni kati ya wale wanaosemwa kuwa wana ndimi mbili. Alishasema mwenyewe kwamba ukatibu mkuu wa chama ndiyo cheo chake cha mwisho. Hatakubali uteuzi wowote ule. Mpka sasa ameshapokea teuzi mbili tayari, ni wa kumuamini kweli huyo?
 
Jamani acheni hizo kwanza tujue Noah zetu zimekwama wapi au kaondoka nazo
 
Mama Samia mbona aliapa au yeye si muislam?
 
Dr. Bashiru leo Bungeni badala ya kusema MIMI BASHIRU ALLY KAKURWA NAAPA KWAMBA...........ameasema MIMI BASHIRU ALLY KAKURWA NATHIBITISHA KWAMBA........

Wakati huohuo na kwa kipindi hicho hicho na kiapo kilekile Balozi Mulamula amesema Mimi....NAAPA KWAMBA....

Kwanini Dr. Bashiru aseme anathibitisha kwamba asiseme anaapa kwamba? Je kuthibitisha na kuapa ni neno moja? Au aliitega mamlaka ya Bunge?
Wanaoapa ni Wakristu, Kamanda, Waislamu huthibitisha. Padri husalimia waumini akisema Bwana awe nanyi, Askofu husema Amani kwenu. Yaani hii miito na miamkio hufundishwa Darasa la 4.
 
kawaida katika kiapo mkristo ANAAPA na mwislamu ANATHIBITISHA...
hii ni mwamujibu wa sheria ya viapo na matamko ya kisheria RE.2019.

Kwahyo kama bashiri ni muislam ni SAHIHI yeye kuthibitisha na si kuapa.
Hiyo ipo kwenye Tume ya uchaguzi na Bungeni lakini mbona Ikulu tumewaona hata hao waislamu wakiapa?
 
Upuuzi mtupu.

Mwisho utasema angevaa suti ya bluu ile haikumpendeza.
 
Konda msafi ule uzi vipi tena ili tuendelee kufurahia, haya mambo ya siasa yana chosha sana.
 
Dr. Bashiru leo Bungeni badala ya kusema MIMI BASHIRU ALLY KAKURWA NAAPA KWAMBA...........ameasema MIMI BASHIRU ALLY KAKURWA NATHIBITISHA KWAMBA........

Wakati huohuo na kwa kipindi hicho hicho na kiapo kilekile Balozi Mulamula amesema Mimi....NAAPA KWAMBA....

Kwanini Dr. Bashiru aseme anathibitisha kwamba asiseme anaapa kwamba? Je kuthibitisha na kuapa ni neno moja? Au aliitega mamlaka ya Bunge?
Ni sahihi. Maneno yote mawili "NAAPA" na "NATHIBITISHA" yanakubalika.
Kunawatu wana tatizo la kiimani na neno "NAAPA", hivyo wamekubaliwa kusema "NATHIBITISHA"
 
Daah ticha Bashiru isingekuwa kovidi ilitakiwa akapumzike Brazil 🇧🇷 kisiwani huko maana si kwa ekizaminesheni hizi,anaona bora angebaki chamani tu kama genelo sekretari tu......ameenda kuungana na wabunge aliokuwa anawapiga mkwara wa kuwakata, usikute alikuwa anapata vi mpesa kidogo.....amekosa friidomu kabisa
 
Back
Top Bottom