Kwanini Dkt. Bashiru aseme anathibitisha kwamba, asiseme anaapa kwamba?

Kwanini Dkt. Bashiru aseme anathibitisha kwamba, asiseme anaapa kwamba?

Dr. Bashiru leo Bungeni badala ya kusema MIMI BASHIRU ALLY KAKURWA NAAPA KWAMBA...........ameasema MIMI BASHIRU ALLY KAKURWA NATHIBITISHA KWAMBA........

Wakati huohuo na kwa kipindi hicho hicho na kiapo kilekile Balozi Mulamula amesema Mimi....NAAPA KWAMBA....

Kwanini Dr. Bashiru aseme anathibitisha kwamba asiseme anaapa kwamba? Je kuthibitisha na kuapa ni neno moja? Au aliitega mamlaka ya Bunge?
Kakwepa laana ya kuapa. Maana hajiamini kuwa atafanya kweli.
 
Nakushauri ili uongeze maarifa katika elimu yako, chukua dakika tano tu kutafuta maana na matumizi ya maneno haya:-
1. Kuapa
2. Kuthibitisha

Halafu njoo kwenye lugha ya malkia jifunze kidogo kuhusu maneno haya :-

1. Swear
2. Affirm

Utanishukuru baadaye baada ya kugundua kuwa wachangiaji wengi humu huwa wanajibu kwa hisia na mihemko bila kujua kuwa kila kitu ni elimu.

Biblia na vitabu vya dini nyingi vinaweka msisitizo kwa watu wake ama waumini kuwa na elimu.

Ahsante.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Dr. Bashiru leo Bungeni badala ya kusema MIMI BASHIRU ALLY KAKURWA NAAPA KWAMBA...........ameasema MIMI BASHIRU ALLY KAKURWA NATHIBITISHA KWAMBA........

Wakati huohuo na kwa kipindi hicho hicho na kiapo kilekile Balozi Mulamula amesema Mimi....NAAPA KWAMBA....

Kwanini Dr. Bashiru aseme anathibitisha kwamba asiseme anaapa kwamba? Je kuthibitisha na kuapa ni neno moja? Au aliitega mamlaka ya Bunge?
Waislamu huwa hawaapi,in english waislamu hawatake oath bali wana affirm
 
Hivi kosa la huyu mtu Ni lipi mpaka watu wamefurahi hivyo
Kosa lake ni: kwa nini anakuwa mwadilifu kutuzidi? Kwa nini hataki kupokea na kutoa rushwa? Watu wana kuja na mihela kedekede kumuhonga anakataa kwa nini - anafagilia umasikini! Kwa nini akipewa kazi anafanya kwa bidii na weledi mkubwa! Au anataka sisi tuonekane wavivu na hatujali? Kwa nini hajilimbikizii mali wakati amepewa fulsa?
Hayo na mengine kama hayo ambayo hafanyi yanatutia ukakasi - anataka kujifanya siyo binadamu kama sisi bwana! Ndiyo maana tumefurahi alipo tendwa.
 
Hivi kosa la huyu mtu Ni lipi mpaka watu wamefurahi hivyo
Huyu jambazi kaua demokrasia ndo muasisi wa kununua wapinzani ,kuharibu uchaguzi ,na aibu atakayoipata Ni kua wale aliowanunua cdm ndo wanaenda kua maboss wake bungeni ,anauliza swali afu anajibiwa na lusinde,waitara,au Gekul
 
Nashukuru kwa ufafanuzi huu ila najaribu kuangalia viongozi wengi wa dini zote wanatumia naapa kwamba, je ni kutokujua? Je jeshini napo wanaapa au wanathibitisha?

Pale wanapoapa kiapo kimoja mtu zaidi ya mmoja mbona sijawahi kusikia wakithibitisha? Rejea viapo vya kijeshi,
Jeshin hakuna dini mkuu utaratbu unao wekwa ni wote mtaufuata
 
Maisha haya Yani bashiru kutoka kuwa Right hand Wa Mwendezake as CS leo anaenda kuwa Mbunge tena wa kuteuliwa aisee hii ni demotion kubwa sana, Mana jamaa ni kama amepunguziwa Clearance ya Information Hana impact tena na mfumo kwa level waliyomuweka
 
Bashiru ana mawenge....tumhurumie tu....maana siku anaapishwa kuwa KMK alisema ana apa sio anathibitisha....same to Mh. Rais siku anaapishwa alisema anaapa sio anathibitisha.....so, dini haiusiki hapo, ni wenge lake tu.
 
Bashiru ni muislamu, haapi

Inanishangaza jinsi waislam wanavyokula viapo vyao kwa namna tofauti tofauti. SSH alipokuwa akiapishwa kuwa Rais alisema, “naapa...” KMK na mawaziri na naibu mawaziri waislam karibu wote walisema, “naapa...” Nilimsikia mmoja tu akisema, “nathibitisha...”

Unatakiwa uwe muislam wa aina gani ili useme, “nathibitisha...”?
 
Kawaida katika kiapo mkristo ANAAPA na mwislamu ANATHIBITISHA...
Hii ni mwamujibu wa sheria ya viapo na matamko ya kisheria RE.2019.

Kwahiyo kama Bashiru ni muislam ni SAHIHI yeye kuthibitisha na si kuapa.
Nakumbuka mama samia wakati anakula kiapo alitamka 'naapa kwamba' wakati yeye ni muislam hii imekaaje mkuu.
 
Back
Top Bottom