Uchaguzi 2020 Kwanini Dkt. Magufuli anakwepa mdahalo wa ana kwa ana?

Uchaguzi 2020 Kwanini Dkt. Magufuli anakwepa mdahalo wa ana kwa ana?

Inawezekana ikawa sikubaliani moja kwa moja na kila analolihubiri Tundu Lissu ila kwa kiasi kikubwa naheshimu sana uwezo wake wa kujenga hoja. Zaidi ya mara moja Tundu Lissu ameomba mdahalo na mgombea wa CCM ambae ndie rais lakini ombi hilo ni kama vile Bw. Magufuli hajalisikia, ila nina yakini kalisikia maana hoja nyingine za Lissu amejaribu kuzijibu kwenye kampeni zake.

Siku zote njia ya kumkamata mtu muongo (Lissu ni muongo kwa mujibu wa CCM) ni kumkabili uso kwa uso na kupangua kila hoja zake. Lakini hili swala la kutokuwa tayari kwa mdahalo kwa upande wa Magufulil inafikirisha sana. Linafikirisha endapo kila analohubiri hana uwezo wa kulitetea, kila anachojinasibu kukifanya hana imani nacho kuweza kukitetea endapo kutakuwa na maswali juu yake ama uwezo wake wa kujenga hoja ni mdogo kiasi kwamba anataka yeye tu awe ndie muongeaji na kusifiwa kwa kila alichokifanya pasi kuhojiwa.

Japo kuna watakaobisha ila ni swala la dhahiri matarajio ya CCM kwenye uchaguzi huu umebadilika sana kinyume na mipango yao. Walihisi kampeni hizi zitakuwa ni nyepesi mno kwa kuamini yale waliofanya ni makubwa mno kuweza kuwapitisha. Lissu kabadilisha fikra za walio wengi kupelekea kufanya watu waanze kuhoji vile ambavyo waliona havikuwa na umuhimu. Waswahili husema 'Usiongelee nafsi ya mtu', CCM waliongelea mioyo ya watu kuamini wote wanahitaji vile walivyovipa kipaumbele.

Isingekuwa Lissu leo hii wote tungekuwa tunaimba mapambio ya flyover na Bombardier kama walivyotaka CCM. Inawezekana hoja za Lissu zisiwe na mashiko lakini zinafikirisha kupelekea kuzua maswali. Njia ya pekee ya kuweza kurejesha watu katika mapambio yaliodhamiriwa awali ni kukubali mdahalo kwa Magufuli ili aweze kutetea na kutuaminisha kuwa alikuwa sahihi na Lissu anakosea (kama tu anakosea kweli). Ni fikra zangu tu.
#NIYEYE2020
 
Hawajui hawa mbumbumbu! Midaharo kitu gani bwana!
Kuna mwajiri yeyoye anaeajiri bila interview? Nimewahi kufanya kazi kwenye kampuni flani hivi kwa miaka 7, kazi ikaisha. Baada ya mwaka na nusu kazi zikafunguka tena na nikaomba position ile ile. Ila sikuingia tu hivi hivi kwa vile hiyo position nimeifanya miaka 7, nilifanya tena interview. Sasa Huyu Magu ni nani asifanyiwe interview?
 
Aje tumfanyie interview tumuulize ni kwa nini tumpe mi5 tena na sio mwingine. Kwani tatizo hapo ni nini? Hata professor lipumba akitaka kuajiriwa lazima afanyiwe interview. CV tu haitoshi
Kwani ni nini maana ya kampeni hizi za kila siku??

Kila siku anahubiri sababu ya kuichagua CCM na yeye kama mgombea wa urais huku akimwaga sera zake kuwa atawafanyia nini wananchi wake.
 
Labda waombe mzee Shivji na Ulimwengu wawasaidie.
 
Back
Top Bottom