Kwanini DP World wamewakimbia watangazaji? Mpemba huyu ni msemaji wa DP? Hawa waandishi warudishe hela za watu?

Hii ni vita ya kiuchumi lakini serikali ya awamu ya sita itashinda tu. Wizi wa kutolipa kodi hapo bandarini hauna faida kwa wananchi wengi zaidi zaidi unawafaidisha matajiri wachache na marafiki zao waliokuwa viongozi wa awamu zilizopita.

GSM aliikimbia awamu ya tano, akaja kurudi alipoingia SSH ikulu, huyu hawezi kukubali kuona mteremko wake pale TPA ukienda kupotezwa na mifumo mipya ya uendeshaji.

Ni vita ya akilini zaidi lakini serikali itashinda tu.
 
Ngoma hii nzito
 
Hata wakiwa na uwezo wa kupokea meli kubwa sawa na mkoa mzima wa Arusha hakuna shida.

Warekebishe mkataba na watapokelewa.

Ila hiyo bure milele hapana aisee.
 
Hili sakata ....limekuwa nguli kweli kweli....limekaa kidini pia...nmeshangaa sehem iringa Muslims wanahamasisha ujio wa DP WORLD...n nini kipo nyuma ya pazia?
 
Blaza mbona unakuwa mkali watu wanapohiji maswala ya DP world!?
Pamoja na swali hilo kuwa zuri kwake, lakini hapa sijaona ubaya wa anayoyahoji.

Mleta mada mwenyewe anaonyesha ni shabiki wa upande wa pili, asiyekuwa na umakini juu ya jambo analolizungumzia.

Hili swala la mikataba mibovu haliwezi kuwa la kupiga 'propaganda' toka upande wowote.
 
Usichojua Ni kwamba Kitenge ni miongoni mwa watu walienda Dubai na akina Musukuma.

Kitenge kaenda kwa mwaliko wa Waarabu ili kufanikishs dili Lao. Ni mtu wako.
 
Tujue kwanza elimu ya Mauld
 
Si mnaona hapo, mfanyabiashara huyo, hana longolongo. Dubai Oyee, tena huyo hao ni ami zake kabisa.
 
Serikali imepoteza hela tena?
Kwamba hao kina Maulid wameenda Dubai Kwa hela za Serikali?
Na Una uhakika kabisa?
Kwani kuna siri kuwa wamelipiwa kwenda kuwahoji DP world? Umesikiliza kilicho ongelewa? Kweli hawajaitia hasara serikali?
 
Kwenye mambo ya namna hii, mstari wa mbele hupelekwa watu wasio na akili, wanaoweza kujitoa ufahamu kama akina Kitenge.
Na kweli wamejitoa ufahamu ndio maana wamebaki kuuliza historia ya DP world
 
Hapo ndiyo inatuthibitishia DP World wana akili na ni Wakimataifa.

Wewe ulitaka iweje?
 
Huyo ndiyo ambaye FaizaFoxy alitumia kuwalaghai vijana humu jukwaani kuwa kazungumza na mtu mzito sana DPW.

Akaleta porojo zake za kuku mwenye kideri.
Ooh, kumbe ndiyo huyo? Sasa mbona ulikuwa unakataa kijana?

Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu.

Mtu wenyewe una akili ya samaki - kwa sauti ya Aman Karume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…