Kwanini Dully Sykes anasema yeye ndiye Mwanzilishi wa Bongofleva?

Kwanini Dully Sykes anasema yeye ndiye Mwanzilishi wa Bongofleva?

screpa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Posts
10,857
Reaction score
15,866
Nimekuwa nikimsikia mara kwa mara akijigamba hivyo kwenye media, na sielewi anamaanisha nini maana maandiko mbalimbali ya historia ya bongofleva hayatambui hilo. Kama anamaanisha 'kuimba' mbona kina Unique Sisters, Mr Paul, Jide, n.k walikuwepo kabla yake?!
 
Miaka hiyo wewe ulikuwa bado unanyonya
 
Nimekuwa nikimsikia mara kwa mara akijigamba hivyo kwenye media, na sielewi anamaanisha nini maana maandiko mbalimbali ya historia ya bongofleva hayatambui hilo. Kama anamaanisha 'kuimba' mbona kina Unique Sisters, Mr Paul, Jide, n.k walikuwepo kabla yake?!
USYK amemchapa mara ya pili mfululizo GYPSY KING
 
Nimekuwa nikimsikia mara kwa mara akijigamba hivyo kwenye media, na sielewi anamaanisha nini maana maandiko mbalimbali ya historia ya bongofleva hayatambui hilo. Kama anamaanisha 'kuimba' mbona kina Unique Sisters, Mr Paul, Jide, n.k walikuwepo kabla yake?!
Zamani kulikua na distinction kabisa ya Genre, R&B, hip hop, bongo flavor etc.

Waliokua wakiimba R&B kama Mr Paul hawakuwa wakiitwa Bongo flavor, ili uitwe bongo flavor sifa kubwa ni kubana pua, So Duly Sykes ni katika wabana Pua wa Mwanzo kabisa.

Mfano wake ni kama sasa hivi Singeli inatofautishwa na Bongo flavor, miaka 20 ijayo pengine Singeli ikawa part ya Bongo flavor, hivyo kina Man fongo wakisema wao ni waanzilishi wa Singeli unaweza ukashangaa, ukaona kama mziki ni ule ule wa kina Juma Nature.
 
Nadhani alitoboa na " Salome juu ya kaburi lako naliaa......." Mwaka 2002 kama sikosei. Kwa umri wangu najua wasanii wote wa Bongoflava miaka waliotoboa na nyimbo walizohit nazo...
Alikua maarufu kabla ya Salome, alikua na Nyimbo yake ambayo leo vijana wangeita nyimbo ya mashangazi, inaitwa Nyambizi, pia alikua na Julieta ya 1999
 
Alikuwa anachana then akaanza kuimba so ile wasanii waliokuwa wanarap then wakaanza kuimba ndio iliitwa Bongo Fleva
 
Kiufupi zamani walikuwa wanachana na huyo dully ndo alianzisha kuimba bongo fleva miaka 1998 hv had 2000 apo huyo dully ni wa kitambo we unamchukuliaje.
kabla hajaja lil sama a.k.a mr.blue, dully ndiye alikuwa dogo ila hakuwa muanzilishi wa bonge fleva. Makundi kama kwanza unity, soggy dog hunter, balozi dullah soul, 2proud a.k.a mr. 2, orodha ni ndefu kabla hajaja dully sykes in the late years 1990s hao ndio wanaweza kusema ni waanzilishi wa bongo fleva. Bongo fleva ya mwanzo ilikuwa ni miziki ya kimarekani ya kufokafoka, rap na hip hop za kina 2pac, biggie, naught by nature, ice cube, snoop doggy dog, na wote wale waliokuwa wanaimba hard core
 
Back
Top Bottom