Kwanini Elimu isitolewe kwa kiswahili mpaka PHD?

kuendelea kwa nchi kuna sababu nyingi na lugha ni mojawapo, tena kubwa tu. hapo kwenye red inatakiwa tushangilie sana kwa kiswahili kuweza kueleweka na watanzania wengi.
 
ahsante kwa kunielewa kaka. Tumekosa maamuzi japo tatizo twalifahamu.
 
kiingereza tutasoma kama somo la kutuwezesha kuwasiliana kimataifa. unafikiri wajapan, wachina au warusi huwa hawaendi kusoma au kufanya kazi uingereza na marekani?
 
ok mkuu nimekupata sasa tunaenda sawa
 
kiswahili ndiyo kinaongoza kwa ufaulu.
Mimi bado sijashawishika kwamba eti kiingereza ndio sababu ya kufeli.
Hivi kwa mfano somo la hisabati ambalo ni miongoni mwa masomo yanayoongoza kwa kufelisha, kiingereza kinasababishaje?
 
ahsante kwa kunielewa kaka. Tumekosa maamuzi japo tatizo twalifahamu.
ni kama watu tuliopotea nnjia lakini tunaona uvivu kurudi kuanza upya kisa tumeshafika mbali.
 
Mimi bado sijashawishika kwamba eti kiingereza ndio sababu ya kufeli.
Hivi kwa mfano somo la hisabati ambalo ni miongoni mwa masomo yanayoongoza kwa kufelisha, kiingereza kinasababishaje?
mkuu hata tukifundisha kwa kiswahili lazima kunasomo litakuwa linaongoza kufelisha na bila shaka litakuwa hisabati. hisabati sio somo la number tu lisilokuwa na maana. hiyo maana ndiyo tunaikkosa kwa kufundishwa kwa kiingereza. wengi wetu tumekariri tu earth as a sphere sijui caliculus na kinematics lakini practical applicatiions zake hatuelewi sawasaawa. watu wanakariri haadi formula derivation?
 
Maendeleo kupitia sayansi yanahitaji kufahamu lugha ya sayansi; hisabati hiyo ndio itakayokupa mawe ya kuvukia mtoni. Nchi nyingi zilizoendelea zilihimiza umahili wa hisabati kwanza mengine yalikuwa ziada.
 
kiingereza tutasoma kama somo la kutuwezesha kuwasiliana kimataifa. unafikiri wajapan, wachina au warusi huwa hawaendi kusoma au kufanya kazi uingereza na marekani?

Hao uliowataja wanajua kiingereza, wasiojua hawatoki nje kufanya kazi zinazohusus interaction/communication na watu.
 
Ningependa kukisoma kitabu hiki. Nitakipata wapi? kimetafsiriwa na nani na kilichapishwa nchi gani?
 
Ningependa kukisoma kitabu hiki. Nitakipata wapi? kimetafsiriwa na nani na kilichapishwa nchi gani?

Muda mrefu sana umepita hata sikumbuki aliyetafsiri na kilipochapwa. Nakumbuka nilikisoma darasa la nne au la tano mwanzo.

Jaribu kwenda kwenye bookshop kubwa kama ile ya hapa Samora Avenue karibu na Askari Monument.

Pia angalia contacts za Mkuki na Nyota Publishers hapa http://www.mkukinanyota.com/
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…