Kwanini Elimu isitolewe kwa kiswahili mpaka PHD?

Kwanini Elimu isitolewe kwa kiswahili mpaka PHD?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
nikiangalia mataifa yote yaliyoendelea kama japan, china, uingereza, s.korea, taiwani, hispania na ufaransa wote hutumia lugha zao za asili kujifunzia. ukweli ni kuwa mtu akijifunzia lugha mama anaelewa sana na kwa kasi zaidi. pia inaondoa tatizo la kukariri na kuongeza ubunifu..

kama miaka kumi iliyopita nilisomaga kitabu cha Alex Haley kinaitwa Roots(kunta kinte)lakini kilichotafsiriwa kwa kiswahili kikiitwa asili. nilikiinjoi sana na nilikisoma kwa muda mfupi sana. mdingi alikuwa anavitabu vingi vya kiingereza lakini ngeli ilikuwa haipandi. bila shaka kingekuwa nacho cha kiingereza nisingekisoma. hapa nataka kusema kiingereza kinanyima watu wengi haki ya kujisomea. imagine kitabu cha rich daddy na poor daddy kingekuwa cha kiswahili?

mi napendekeza kiingereza tungejifunza kama lugha ya kimataifa lakini jiografia, uraia, kemia, biolojia, hisabati na historia tujifunze kwa kiswahili mpaka chuo kikuu. pengine waafrika ni maskini kwa sababu tunajifunzia lugha tusizoelewa vizuri. we mdau unamaoni gani kuhusu wazo ili?.
 
hivi wameshatafsiri hata Abott na Nelkon kwa.kiswahili?
inabidii tuanze sasa kutafsiri. nguvu=kani x umbali uliosafiriwa kwenye uelekkeo wa kani. see! siio hata ngumu
 
Umenikumbusha kitabu cha roots cha Kiswahili, nilikisoma nikiwa mdogo.

Kiswahili inabidi kikue katika jamii kwanza kabla ya kutumika masomoni, ama sivyo Kiswahili cha masomoni kitakuwa tofauti na cha mtaani kama Kiingereza kilivyo tofauti na Kiswahili halafu tutarudi square one bila ya kuwa na faida katika nyanja za kimataifa.
 
kama WENGI wenye PhD ya kiswahili,masomo kama physics,chemistry,mathematics kiukweli Waliishia kuyasoma vizur f2 sasa unategemea huyu mtu anauweza wa kutafsiri CHAND,.ikumbukwe kuwa kiingereza cha sayansi kinatofautiana sana na kiingereza cha kawaida ndo mana wengi wanakimbia umande,so bado kazi tunayo wameshindwa INDIA sembuse TZ ya UKAWA
 
Mwl nyerere aliwahi kusema "...kiingereza ni kiswahili cha dunia.." tafakari...chukua hatua.
 
Ucfkirie kiraic ivo hatuna uwezo hata wakutoa ajira wala hatuna plants kubwa za kuweza zalisha machines kubwa bado unataka tuangaikie wht has no meaning
 
Ucfkirie kiraic ivo hatuna uwezo hata wakutoa ajira wala hatuna plants kubwa za kuweza zalisha machines kubwa bado unataka tuangaikie wht has no meaning

Kwani ukisoma kwa kiswahili usomi wako unakua tofauti kiasi kwamba inakuwa ngumu kupata ajira sehemu nyingine (mfano, mtu akisoma udaktari wa binadamu kwa kiswahili, kifaransa, kiingereza, kirusi na kichina wana tofauti gani), thamani ya elimu itakuwa ile ile uniambiee mchakato wa kufanya tafsiri ya vitabu vya fani mbalimbali katika lugha yetu ukiongeza na kubadili mfumo mzima wa ufundishaji utakuwa na gharama pia jamii yetu imejiandaaje nayo ni changamoto maana ukiangalia kwa kina kiingereza wengi hatujui na kiswahili pia watu hawakijui japokuwa tunajifariji sie ni wataalamu wa kiswahili
 
Ni kweli kabisa, nchi zilizoendelea zinatumia lugha zao kufundishia madaraja yote. Ishu kwetu inakuja, hatuna rasili mali za kuwezesha hili ukilinganisha na nchi hizo. Hii ni kwa nchi zote za Afrika. Tatizo ni rasili mali, ndo maana tunatumia lugha za mataifa yaliyotutawala. Ila kwa chi yetu imekuwa funika. Tunakuwa na wakati mgumu zaidi sababu wengi tunaanza na lugha mama kwenye msingi (Swahili) kisha ghafla tu kwenye huo msingi tunakuja weka lugha nyingine. Hivyo tunabaki in a state of limbo. Ila endapo tungekuwa na rasili mali, hii ingewezekana kabisa na tungekuwa na watu ambao hawakukremishwa, bali wenye welevu na ubunifu katika fani tofauti za maendeleo.
 
nikiangalia mataifa yote yaliyoendelea kama japan, china, uingereza, s.korea, taiwani, hispania na ufaransa wote hutumia lugha zao za asili kujifunzia. ukweli ni kuwa mtu akijifunzia lugha mama anaelewa sana na kwa kasi zaidi. pia inaondoa tatizo la kukariri na kuongeza ubunifu..

kama miaka kumi iliyopita nilisomaga kitabu cha Alex Haley kinaitwa Roots(kunta kinte)lakini kilichotafsiriwa kwa kiswahili kikiitwa asili. nilikiinjoi sana na nilikisoma kwa muda mfupi sana. mdingi alikuwa anavitabu vingi vya kiingereza lakini ngeli ilikuwa haipandi. bila shaka kingekuwa nacho cha kiingereza nisingekisoma. hapa nataka kusema kiingereza kinanyima watu wengi haki ya kujisomea. imagine kitabu cha rich daddy na poor daddy kingekuwa cha kiswahili?

mi napendekeza kiingereza tungejifunza kama lugha ya kimataifa lakini jiografia, uraia, kemia, biolojia, hisabati na historia tujifunze kwa kiswahili mpaka chuo kikuu. pengine waafrika ni maskini kwa sababu tunajifunzia lugha tusizoelewa vizuri. we mdau unamaoni gani kuhusu wazo ili?.

Kama hutegemei kutoka nje ya Tanzania, au kufanya kazi na wageni katika managerial position/technical positions, go on with Kiswahili to university level
 
Umenikumbusha kitabu cha roots cha Kiswahili, nilikisoma nikiwa mdogo.

Kiswahili inabidi kikue katika jamii kwanza kabla ya kutumika masomoni, ama sivyo Kiswahili cha masomoni kitakuwa tofauti na cha mtaani kama Kiingereza kilivyo tofauti na Kiswahili halafu tutarudi square one bila ya kuwa na faida katika nyanja za kimataifa.
lakini huwa najiuliza kama kijapan, kichina na kikorea zilikuwa lugha kubwa sana kuliko kiswahili zilipoanza kutafsiri elimu za magharibi kwa lugha zao?. pia sehemu kubwa ya vitabu huwa ni maneno ya kuelezea na machache ni magumu/kisayansi ambayo hata wazungu wenyewe kwao ni magumu.
 
Ucfkirie kiraic ivo hatuna uwezo hata wakutoa ajira wala hatuna plants kubwa za kuweza zalisha machines kubwa bado unataka tuangaikie wht has no meaning
inawezekana hatuna plants kubwa na uwezo wa kuzalisha ajira kwa sababu tumejifunzia lugha za watu na kuzalisha wataalamu substandard. tatizo unalofikiri ni dogo linaweza kuwa ndiyo kubwa kuliko yote.
 
Kama hutegemei kutoka nje ya Tanzania, au kufanya kazi na wageni katika managerial position/technical positions, go on with Kiswahili to university level
watu wengi husema tutashindwa kuwa kimataifa. niliona japo tunatumia kiingereza waliokimataifa bado ni wachache. marekani kuna watanzania 20,000 tu. pia sio kwamba tukisoma kwa kiswahili kiingereza ndio tutakuwa hatusomi kabisa, tutasoma kama lugha ya kimataifa. mbona wachina na wajapan wanasoma kichina lakini wanafanya kazi na wageni na nje ya china?
 
Maendeleo hayaji kwa watu kutumia lugha yao sana.

Watu kutumia lugha yao sana huja kwa kufuata maendeleo.

Unataka watu watumie lugha yao hata printing presses za kutosha huna?

You have it backwards.

Kuza uchumi upate umuhimu wa kimataifa utaona mpaka waChina wanajifunza Kiswahili en masse.

Endelea ku import kila kitu utaona hata Waswahili wanasahau Kiswahili.

This is a function of the economy.

Kwa nini Kiingereza kinatumika dunia nzima.leo wakati Uingeteza ni kisiwa kidogo tu kilichokuwa na watu wachache sana?
 
ni ujinga wa viongozi wa kiafrica kuwa na vijimavi vya ukoloni katika vichwa vyao...kiswaili ni lugha kubwa thana na inawezekana kabisa kufundishia ngazi zote za elimu...ila naamini tutapata viongozi watakao kuja kufanya mageuzi haya makubwa..
 
Ukweli ninaoufahamu mimi, lugha si tatizo, kisingizio wala kichocheo.

Wanafunzi wanafundishwa kiswahili hadi anafika darasa la saba, lakini bado wanakuwa hawajui kuandika. Hapa hapa mtandaoni, tunashuhudia kwa macho yetu watu wengi hawawezi kujadili kwa hoja. Sana sana wanaishia kutukana matusi kana kwamba matusi yataleta uzito wa hoja. Uwezo wa kuchanganua hoja na ku reason uko chini. Tatizo la lugha lina nafasi ndogo sana kwenye uelewa. Ni vyema tukakubali kwamba elimu yetu kwa ujumla imekuwa na matatizo makubwa sana siku za hivi karibuni (awamu ya nne). Njia sahihi ya kutatua ni kutafiti sababu halisi za anguko lile, kuzikubali na kuzi address ipasavyo. Vinginevyo tutaendelea na visa vya mbaazi anapokosa maua.

Nchi alizozipanga, hazijaendelea kwa sababu zilitumia lugha zake shuleni. Ukizitazama ni nchi zenye juhudi kubwa sana katika ukuaji na maendeleo ya sayansi na technolojia.
 
Back
Top Bottom