Kwanini familia za nchi zilizoendelea hazina wasaidizi wa kazi za nyumbani (house girls)?

Kwanini familia za nchi zilizoendelea hazina wasaidizi wa kazi za nyumbani (house girls)?

Unafikiri kwa taratibu za uajiri za hao wasaidizi wa ndani kwa ulaya zingewekwa hapa kwetu naona kabisa hakuna ambaye angeajiri hao wasaidizi labda matajiri...
 
Nimekuwa nikitafakari kwa muda sasa.
Kwanini familia za waafrika bila dada wa kazi au housegirl mambo hayaendi?

Mke atalalamika, nyumba itakuwa chafu, chakula hakitaiva kwa wakati yaani mambo yote yatakuwa vurumai.

Lakini ukiangalia wenzetu walioendelea familia nyingi ni baba, mama na watoto na wote wanajituma katika majukumu yao.
Ni familia chache za matajiri sana wenye mansions ndio utakuta kuna maids.

Je ni uvivu?
Je ni kwasababu wanapatikana kwa bei chee?

Ni tabia zetu tu kupenda ubwanyenye?
Nna ndugu yangu aliendaga huko majuu yee hanaga mfanya kazi akarudi TZ na ujuzi wa kupika msosi wa wiki nzima alafu unapaki kwenye vicontena vdogovdogo then unagandisha mkitaka kula mnakitoa kimoja kama ni cha maharage na kingine cha nyama then kazi ni kusonga tuu ugali ama kupika wali.
Sasa Cha ajabu ndugu wa mume wakienda pale wanalalamika etii kaka Yao analishwa vipolo[emoji2]wakati mwanamke ni mtu busy sana Hana mda wa kupika l.

Isitoshe familia zetu watu weusi kazi za nyumban zote ni zamama usishangae mkarudi kazin wote Satatu usiku baba akanyosha miguu seblen mama ukaanza kuhangaika na majiko mawilimawili kama upo na mlemavu umo ndani.
 
Unafikiri kwa taratibu za uajiri za hao wasaidizi wa ndani kwa ulaya zingewekwa hapa kwetu naona kabisa hakuna ambaye angeajiri hao wasaidizi labda matajiri...

Kwahiyo serikali inashiriki housegirls kunyonywa
 
Nimekuwa nikitafakari kwa muda sasa.
Kwanini familia za waafrika bila dada wa kazi au housegirl mambo hayaendi?

Mke atalalamika, nyumba itakuwa chafu, chakula hakitaiva kwa wakati yaani mambo yote yatakuwa vurumai.

Lakini ukiangalia wenzetu walioendelea familia nyingi ni baba, mama na watoto na wote wanajituma katika majukumu yao.
Ni familia chache za matajiri sana wenye mansions ndio utakuta kuna maids.

Je ni uvivu?
Je ni kwasababu wanapatikana kwa bei chee?

Ni tabia zetu tu kupenda ubwanyenye?
Nchi zilizoendelea Matajiri Wana maids hata watano. Ila Hawa wanaishi kwenye vijumba vyao häwana nafasi, Wanaishi Maisha madogo sana yasio na furaha wanateseka mno
 
Hizo familia zilizoendelea hawatumii mkaa kupika Wala masufuria dhaifu ya aluminum yanayopoteza mvuke.

Pia hawafui nguo kwa mikono, Wala hawaendi umbali mrefu kutafuta maji.
Umemaliza kila kitu.
Hawaamki Saa kumi kuteka maji, Wala SAA Kumi na Moja kuandaa Watoto shule
 
Hakuna haja ya housegirl. Kujiendekeza tu. Wakuta kina mama tena wa nyumbani wanarusha miili yao barabarani huku nyumbani hata kuosha vyombo issue. Hata hizo nguo za mazoezi wanafuliwa! Bongo uvivu ubwanyenye ukatili utumwa na uonezi.
Kama wote mnapiga job ni kujipanga tu. Kuna nurseries wakiwa wadogo. Mpokezane. Kila kitu kiwe 50 50. Iwe usafi mapishi kufua kuhudumia mtoto/watoto nk Mambo ya husband/wives kwenda bar hovyo hovyo yaachwe.
Yawezekana. Na bado naamini weekend kuna muda wa kutosha kula bata bar au na familia…
 
Hapo hujaweka gharama ya kumlisha na kumvisha.
Au ndo wale mnawafanya mahousegirl watumwa?
Kwa mtu mwenye utu gharama ya chakula huwa haiongezeki sana anapoongezeka mtu mmoja kwenye familia na mara nyingi (hasa nyumban kwetu) housegirl anakula chakula tunachokula familia nzima.
 
Nimekuwa nikitafakari kwa muda sasa.
Kwanini familia za waafrika bila dada wa kazi au housegirl mambo hayaendi?

Mke atalalamika, nyumba itakuwa chafu, chakula hakitaiva kwa wakati yaani mambo yote yatakuwa vurumai.

Lakini ukiangalia wenzetu walioendelea familia nyingi ni baba, mama na watoto na wote wanajituma katika majukumu yao.
Ni familia chache za matajiri sana wenye mansions ndio utakuta kuna maids.

Je ni uvivu?
Je ni kwasababu wanapatikana kwa bei chee?

Ni tabia zetu tu kupenda ubwanyenye?
Nchi zilizoendelea MTU anayeweza kumlipa housegirl ni wale mafogo aka matajir wakubwa. Kule HYo ni Kazi rasmi Kabsa na unalipa pesa za kutosha. Sio Kama huku uyaya unalipa 50000 na Bado unamsimamanga
 
Mwingingine ni uduwanzi tu

Imagine nmetoka kuoa tu na tuna miezi mitatu tu kwenye ndoa , maisha bado vurugu vurugu yan hadi bado madeni mengine ya harusi hatuja clear... Halafu wife analilia mfanya kazi na yeye ni mama wa nyumbani.. Kidume nkakaza kwamba hapana hiyo kitu haiwezekani hilo wazo la mfanya kazi lifte kabisa...

Mara ghafla mtu hodi mlangoni na mashangazi kaja mawili safari ya kuvuka mikoa mitatu na nauli kalipiwa na dada ake wife yani shemeji angu... Haloo huyu binti anapiga kazi balaa...

Ataamka mapema atafanya usafi, atapika chai mapema, maji anafata, chakula anapika kwa wakati japo quality inapungua ukilinganisha na anavyopika wife... yani hapa nawaza nmtimue yeye au nmtimue wife Na ni lazima mmoja atimkie mbali fumbafu
Mwanangu nipasie huyo housegirl,,Ili niokoe ndoa yako. Niko sirias
 
Nimekuwa nikitafakari kwa muda sasa.
Kwanini familia za waafrika bila dada wa kazi au housegirl mambo hayaendi?

Mke atalalamika, nyumba itakuwa chafu, chakula hakitaiva kwa wakati yaani mambo yote yatakuwa vurumai.

Lakini ukiangalia wenzetu walioendelea familia nyingi ni baba, mama na watoto na wote wanajituma katika majukumu yao.
Ni familia chache za matajiri sana wenye mansions ndio utakuta kuna maids.

Je ni uvivu?
Je ni kwasababu wanapatikana kwa bei chee?

Ni tabia zetu tu kupenda ubwanyenye?
Hujakua bado ukikua utaelewa
 
Hizo familia zilizoendelea hawatumii mkaa kupika Wala masufuria dhaifu ya aluminum yanayopoteza mvuke.

Pia hawafui nguo kwa mikono, Wala hawaendi umbali mrefu kutafuta maji.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom