Kwanini gari aina ya Nissan X-trial used zinauzwa cheep sana?

Kwanini gari aina ya Nissan X-trial used zinauzwa cheep sana?

Hapo kwenye ulazima wa ku change oil kila km 3000 bado pia ni kasoro,usiitetee kuwa ni gari nzuri,ukiwa na Toyota ambayo unatakiwa uchange engine oil km 3000 unaweza kujisahau ukafikisha mpaka km 5000 na bado gari ina dunda,sasa kwanini uing'ang'anie hiyo Nissan...
Dah....

Km3000 ni preventive tu mkuu you can go hata 10,000km interval ili mradi engine haichomi oil, but that will be at the expense of your car's engine life.
 
Nissan X trail ni slay queen unataliwa kila muda unampeti peti akililia pipi unatakiwa kuwa na box tofauti na happy unatakiwa kumukimbia tu [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] wakati unawaza kuulinda mfumo wa CVT transmission Kwa kutumia oil iliyokuwa unatakiwa na manufacturers pia bei ya spea iko juuu pia mafundi sio wa chini ya mti
Nissan xtrail ya kwanza haitumii cvt gear box, ila hizi za sasa ndo zinakuja na gearbox ya cvt, ambapo kuna zinatumia NS-2 or NS-3 transmission fluid, ila Nissan xtrail ya kwanza inatumia matic J fluid.
 
Binafsi nina marafiki wachache wanapenda sana hizi gari..japo kuzielewa why ukiuza haziuziki bado sijajua---kwenye soko la compact SUV's--nyingi ni ghali sana kama zikiwa na 4X4--Xtrail ina 4X4 nzuri tu--na kuwa na plastiki ndani inaosheka vizuri kama una shughuli za kuchafua gari.Labda ni mafundi wanaoharibu hii biashara,
 
Zina demand ndogo sana kwenye soko la second hand cars kwa Tanzania kwa sababu inaaminika kuwa ni mabovu (mafundi watakwambia ni mabovu sana, na watu wengi watakwambia hivyo). Pia, spare zake ni bei ya juu kuliko spare ya Toyota. Tatu, hizi gari mafundi wanaoziwezea wako wachache ukilinganisha na gari za Toyota, hivyo ikizingua unaweza ukahangaika sana na labda usipate kabisa fundi atakaemaliza tatizo lako, au ukapata fundi wakiwa wameshaliharibu sana. Sababu hizo hufanya demand yake kuwa ndogo sana, hivyo kusababisha bei yake kuwa chini sana zinapouzwa mkononi.
Bighorn je?
 
Back
Top Bottom