Una maanisha nini? Kama timu unayoifanyia kazi bosi wake ni mo kipi wewe mo asiwe boss wako. Kama A=B na B=C kwanini A isiwe sawa sawa na C pia?
Asikudanganye mtu mashabiki wa Simba wanakuja uwanjani kwakuwa Simba inashinda mechi zake. Timu inashinda kwakuwa Ina wachezaji wazuri na wachezaji wazuri nacheza vizuri kwakuwa wamelipwa na anaewalipa ni mo, na mo anapata pesa za kuwalipa wachezaji wazuri kutokana na kuuza maji ya masafi, na Haji anauza maji ya Uhai ya Azam sokoni ili mo asipate hela za kuwalipa vizuri wachezaji. Kwa hili Haji ni msaliti wa Simba bila kupepesa macho Wala kupindisha maneno.
Haji alitakiwa kudai mshahara na mkataba kwa Simba hata kupitia vyombo vya Sheria lakini sio kufanyakazi za mshindani wa mo. Kumfukuza Haji Simba ni halali kabisaa.