Mikopo Chefuchefu
JF-Expert Member
- May 15, 2017
- 3,373
- 6,795
Mtawafukuza uanachama, wataenda mahakamani kuweka pingamizi mpaka miaka yao mitano itakwisha.. Waacheni.. Wamecheza karata yao vizuri kwa kuonesha kuwa Mboe na Mnyika si lolote si chochote.. Chama sio mali binafsi.. Hata Mboe na Mnyika wanaweza kufukuzwa uanachama kwa kutozingatia goals za chama ambazo wanatakiwa kuzizingatia.Faida ya Kwanza wakifukuzwa ni kwamba Watakosa uhalali wa kisheria kuwa wabunge wanaowakilisha CHADEMA Bungeni hata wakilindwa na Serikali.
Goalz za chama chochote Duniani ni kukamata dola.. Hata jeshi linapoenda vitani haliteki maeneo yote kwa mara moja.. Linateka mkoa mmoja, linaweka base, linaendelea mbele mwishowe linateka nchi nzima.
Harakati za vyama pia ziko hivyo, mnapoukosa urais, basi angalau mnahakikisha mnateka viti kadhaa vya ubunge, udiwani nk. Kwa mtazamo wa kuja kuteka dola siku za usoni.