Kwanini Halima Mdee na wenzake ni lazima wafukuzwe?

Kwanini Halima Mdee na wenzake ni lazima wafukuzwe?

Mrefu sana mzee kweli kila mtu ana bei yake. Na Ccm walivyowajanja usikute yule bulaya aliolewa makusudi toka TISS Kuja kumaliza na mdee kamaliza kazi dah hata mdee
Kesho ataongea na press muone Sasa watu watakavyovuliwa nguo
 
Mrefu sana mzee kweli kila mtu ana bei yake. Na Ccm walivyowajanja usikute yule bulaya aliolewa makusudi toka TISS Kuja kumaliza na mdee kamaliza kazi dah hata mdee
Na yule mbunge wa nkasi nae ni tiss
 
Kesho ataongea na press muone Sasa watu watakavyovuliwa nguo
Walishaongea wengi kwa kupangwa unakumbuka wale waliopora madai ya kuomba ngono? Hivi ulishasikia mwanamke mwenye akili timamu analalamika kutongoxwa hadharani wewe? Yaani mwanamke KUONGOZWA ikawa kete ya Ccm wakati ule. Leo unasikia anaongea
Lijua likali leo yupo wapi? Alilalamika kukatwa pesa watu wakaitwa PCCB? Mwisho ikawaje????
Chama cha Ccm kinafikiri dunia ipo miaka ya 1950 kumbe tupo 21thc hovyo kabisa.
Aongee na press wakati mnyika alishatoa utaratibu ambao haukufuatwa kumpata hugo mdee na wenzake???
 
Hivi kwanini CHADEMA mnanunulika kirahisi kiasi hicho? Hivi kuna mtu ndani ya CHADEMA anaweza kusema hanunuliki? Mpaka Mdee kweli? Hakuna chama hapo
Hivi mdee kuna kipindi nilisikiaga hajulikani alipo baada ya uchaguzi, what happened? Kwenye kujua tujuzeni jmn.....connect the dots.
 
Asante Sana, Kama kawaida yako, maneno meeeengi, mtu akimaliza kusoma hata hakumbuki Yericko kasema nini.
Kipekee, nikushukuru kwa kutuandalia malighafi muhimu kabisa kwa toilet paper. Asante, tutakuja kuzichukua!
Elimu ndiyo chanzo cha ufinyu wa uelewa wetu ktk mambo mengi sana yanayotukabili. Daah!
 
Wengi hawafahamu kwamba kwasasa "DEREVA" gari limeshamshinda, linayumba yumba barabarani tu (Things Are Out Of His Hands And Out Of Control - The Country Is In Deep Murmuring Chaos).

Na kawaida gari linapomshinda dereva basi kila atakachotaka kufanya ili kulikweka sawa na kila anavyopapatua, ndio anapo haribu zaidi na kulitoa nje ya barabara.

Sasa hivi kila mtu anajifanya mjuzi kuliko dereva, na ndio wanazidi kumchanganya na kumptoteza kabisa dereva. Huyu kawasha end-cator, yule kapiga honi, huyu kakunja sight-mirror zote (Waziri Wa Mambo Ya Nje alichokonoa mambo vibaya. AG na SPEAKER leo ndio "WAMECHOMOA BETRI" kabisa).

Kwa tulipofikia, gari linasubiri sababu tu lianguke na kuua abiria. Hakuna hatua yoyote ya kuliokoa gari wala kumsaidia dereva. Zaidi ya kumwomba mungu idadi ya wafu na majeruhi iwe ndogo.

● Kwa wenye akili na maarifa (hata wana CCM wenyewe) ndio maana wamekaa kimya na kujiweka pembeni. Wanatazama tu. Wanajua impact itakayotusibu kama taifa.

● Cha kujiuliza,

1) Kwanini siku ya leo "SERIKALI IMEONESHA INTEREST KUPITA KIASI" kuhusiana na hawa wabunge 19.???

2) Na kwanini bunge (Speaker) ameonesha "INTEREST KUPITA KIASI" kuhusiana na hawa wabunge 19.???

■ Nchi ina mihimili mitatu. Mihimili miwili tayari (Serikali na Bunge) vimeshakuwa "BIASED". Umebakia mhimili mmoja tu "MAHAKAMA".

■■■ Kwanini nasema "KWA TULIPOFIKIA, GARI LINATAFUTA SABABU TU YA KUANGUKA NA KUUA ABIRIA"???

PRINCIPLE KUU YA UTAWALA

"Binaadamu ana mahitaji makuu, ambayo ni "Chakula, Matibabu na kuijua kesho yake". Binaadamu hawatawaliwi kwa nguvu bila hayo matatu na utawala ukafanikiwa.

Nature ya binaadamu, akiwa "AMESHIBA (Ana chakula/pesa) basi anakua binaadamu na anatawalika kirahisi, ila akiwa na "NJAA (Hana chakula/pesa)" akili inafanya kazi kupita kiasi na anakua mnyama asiekua na uoga wowote na muogope kama Covid-19 au HIV AIDS!!!

Kifupi, binaadamu mwenye njaa hatawaliki na yuko radhi kufanya lolote.

Nchi yetu raia hawana kipato na hawana mwelekeo kwa sasa. Mbele yao ni giza nene. Muda si mrefu hawata tawalika wala kutii serikali.

JIBU.

Sisi kama taifa, asilimia 98% ya raia wanalalamika hali ni ngumu kupita kiasi (Hawana pesa kukidhi "Kupata chakula, matibabu na hawaijui kesho yao). Serikali nayo haina pesa kujiendesha yenyewe kupelekea kuongeza kodi kwa raia wasio na kipato.

Raia wangekua na pesa ya kukidhi mahitaji yao. Basi dereva angefanikiwa kuliweka gari sawa.

Hili ni "TIME BOMB (BOMU)" kwa serikali yetu, bomu hili linalosubiri muda/kiberiti tu liripuke. Kinacho chelewesha ni raia kuwa "WAOGA" bado, ila uoga ukitoweka kwa raia bomu linaripuka.

USHAURI KWA CHADEMA.

Wakikaidi na kuachana na "VITISHO VYA A.G na SPEAKER" kisha wakafanya maamuzi ya kuwafukuza "UWANACHAMA" hao 19 waliosaliti, kisha wakaongeza "PRESSURE ZAIDI NA ZAIDI" kwa dereva. Dereva watamchanganya zaidi na kupindua gari ndani ya muda mfupi sana.

Katika mapambano yoyote (hata mpira wa miguu), adui yako mwenye nguvu anapokua na "PRESSURE NA KUJIKANYAGA KANYAGA", usimpe nafasi ya kujipanga, ongeza pressure na mashambulizi zaidi ili aharibu zaidi na umjeruhi zaidi. Na kamwe usilipe fadhila ya kumpunguzia mashambulizi.

CHADEMA wakiamua kufunika kombe ili mwanaharamu apite (Wasipo wafukuza hao wasaliti 19 uwanachama) basi gari litapunguza kasi kidogo, pengine dereva akajitambua na gari litadondoka upande waliokaa wao CHADEMA na kuwaua (Chama kitakufa na kupoteza wanachama kama CUF ya Lipumba).

ZINGATIO

Ili CHADEMA na ACT WAZALENDO kuleta madhara zaidi na zaidi kwa Serikali ya CCM, Chadema "KUWAFUKUZA UWANACHAMA HAO WASALITI 19" haitoshi, japo ndio maamuzi sahihi ya kuchukua.

Baada ya kuwafukuza hao 19, kama vyama vya upinzani vikuu vinapaswa kuongeza "PRESSURE ZAIDI NA ZAIDI (ADD MORE PREESURE AND MORE PRESSURE) kwa serikali na NEC kutoa majibu ya hao waliopeleka hayo majina na kusign hizo form. Isiipe serikali nafasi ya kuvuta pumzi hata kidogo wala nafasi ya kujipanga.

Serikali na NEC isipotoa majibu ya kuridhisha, basi iendelee kupiga "KELELE" katika mataifa yenye nguvu duniani pamoja na AU/UN kuingilia kati.
Bwana Alexander ... umeongea ukweli wa hali halisi

Yetu macho na upande wa sokio
 
Kama watafukuzwa hiyo haina shaka utaratibu ufuatwe kwa mjibu wa kanuni na taratibu za chama nje ya hapo
 
Nyerere ifike hatua chadema lazima mji tambue na mfanye siasa Kutokana na Hali ya wakati uliopo

Hayo madai yenu Hayana msingi bcoz Mnadai kwa faida yenu wanasiasa na sio faida ya wananchi

Hivi kwa akili yako unadhan jpm atarudia uchaguzi? Kwa akili yenu Kuna katiba mpya hapa soon?

Nyie mkiambiwa lipieni uchaguzi hizo ela mnazo?

Mnaacha kujijenga kwa miaka mitano hii nyie kila siku ni tume Mpya na katiba mpya utadhan hakuna kitu kingine Cha serikali kufanya zaid ya kuwasikiliza nyie tu

Kama kweli mnahoja si muende ikulu pale mkadai hiyo katiba mpya mbona unaongea ukiwa zako umekaa kigamboni huko
Pumbavu wewe

Nyie ccm mmeshawahi fanya jambo kwa maslahi ya wananchi???

Utopolo sana wewe
 
Sasa jpm ndio Rais wa TZ kama hutaki Hilo vuka borders nenda msumbiji

Kazi ni kupiga kelele ambazo hazina msingi
Ameuliza kuwa mwenyekiti wa CCM alisema CHADEMA & vyama vya upinzani kwa ujumla wanachelewesha maendeleo,lakini leo CCM wanawalilia wabunge wa viti maalumu toka CDM,kunani hapo? Tupe jibu.
 
Yericko ndiyo ni muhimu kwa mustakabaii wa chama kujenga nidhamu, pia hakuna mkubwa kupita chama. Chama hakiwezi kuendeshwa na watu wasaiti. Shetani aifukuzwa kwa kusaiiti na ndiyo maana ni muhimu kuondoa Covid 19 kujenga nguvu ya chama. Serikaii inawahitaji hao kwa kusudi kueeza jumuiya za kimataifa kuwa kuna bunge na wapinzani wamo wanaweza kusimamia fedha zinazotowa kupitia kamati za PAC na nyingie, pamoja na 1tri na usee za EU.
 
Hawa watu hawawezi kufukuzwa. Jaribuni kupunguza munkari kidogo na kujaribu kuvivaa viatu vya Mwenyekiti for a minute na mtaelewa mambo haya.
 
Back
Top Bottom