Kwanini hatutambui umuhimu wa China kwa mataifa yanayoendelea?

Sasa mfano hapa inaonekana kabisa mali za aliyekopa zinachukuliwa ambapo ni kitu cha kawaida hata kwa mtu mojamoja hata hapa kwetu katika mabenki.

Wewe unataka ukikopa ukishindwa kulipa uongezwe mkopo, alafu tena ukishindwa uongezewe tena vivyo hivyo kama vile hauna ubongo. Je, kwako wewe hii ni sahihi?

Unapowajibishwa pale unaposhindwa kulipa ni sawa na kukumbushwa kutumia mikopo kwa usahihi na si kununulia wapinzani, kuunda magenge ya kihalifu, kuhonga wanawake weupe weupe na kujijengea majumba ya kifahari na viwanja vya ndege vya kifahari porini ambako kutakufanya ushindwe kurejesha mkopo.

China inatumia kanuni za asili za kukumbushwa kulipa gharama ya matendo yako... Mataifa ya magharibi wanakunyamazia ili wawe na nguvu ya kukuforce kukubaliana na mambo yao hata kama hutaki
 
Tatizo sio China bali ni Zambia kwa kukopa bila kujua unaenda kufanyia nini huo mkopo
kwenye shabba ambayo zambia ingetosha kabisa kuwafanya wawe nchi ya maendeleo ya juu wanapata nini ? shabba ndiyo ipo kwenye betri zote na mitambo yote ya air condition na china inaongoza kwasababu ya Zambia. Haya madeni ya Zambia yamewekwa makusudi kuitawala na kuchukuwa shabba leo unataka tuwasifia china kwa lipi?
 
Hebu acha KUKURUPUKA!!! Ulisikia lini nchi yoyote ile ya Magharibi kuchukua asset ya nchi yoyote ile Africa au third World kwa kushindwa kulipa deni!?
😳😳😳😳😳
 
CHINA WANAKUSAIDIA WAKUMALIZE. KAULIZE ZAMBIA NA SRI LANKA... AFRICA IJITEGEMEE TUACHE KUSUBIRIA WAKOLONI
Dawa ya deni ni kulipa sio kutaka kuongezewa mikopo huku ukisamehewa mikopo ya zamani... Ukiwa na akili hizi za kutaka raia wa Ulaya walipe kodi alafu wakuletee wewe ule tu huo ni upumbavu wa hali ya juu sana!

Hivi ulishawahi kukopa kidogo kwenye taasisi yoyote au kwa mtu binafsi ujue haya mambo au nakupigia gitaa?
 
China aliwashikia mtutu kuwalazimisha kusaini hiyo mikopo?

Hapa Tanzania tu maviongozi yenu yanasaini mikataba mibovu ambayo unakuta wao wanaondoka na 90 huku asilimia 10 ikibaki. Haya hamyaoni ila mmebaki kushikilia propaganda za mabeberu dhidi ya China
 
Mleta mada, umeleta jambo zuri sana na niukweli usiopingika kuwa china imejitoa sana katika kulisaidia bara la Africa hasa katika masuala ya kiuchumi, vitu vilivyokuwa bei ghari kama magari imekuwa jambo la kawaida.

Lakini pia pamoja na yote hayo china inamalengo yake kwa Africa, pasipo kujali malengo yake au dhamira yake ching no rafiki bora Wa Africa ukilinganisha na mataifa mengine.

Naomba pia niulize swali, je Africa haiwezi kuendelea pasi na kutegemea mikopo?
 
Hebu acha KUKURUPUKA!!! Ulisikia lini nchi yoyote ile ya Magharibi kuchukua asset ya nchi yoyote ile Africa au third World kwa kushindwa kulipa deni!?
😳😳😳😳😳
Nini maoni yako? Waendelee kutupa mikopo na misaada tuile alafu waje tena kutujengea vyoo?
Hata baba mwenye uwezo hawezi kufanya hivyo kwa mwanae... Hayo ni matumizi mabaya ya akili
 
Jibu swali langu badala ya kulikimbia!!!
Nini maoni yako? Waendelee kutupa mikopo na misaada tuile alafu waje tena kutujengea vyoo?
Hata baba mwenye uwezo hawezi kufanya hivyo kwa mwanae... Hayo ni matumizi mabaya ya akili
 
Inaweza. Kinachoonekana mbele ambacho ni kizuri kwa wengi na kibaya kwa wachache ni kwamba, China itakapokuwa imewashusha chini mabwana waliopo sasa itapanga hadi safu ya viongozi wachapakazi sehemu zote duniani kwa lengo moja tu ambalo ni kujenga dunia yenye hatma ya pamoja.

Yani katiba itakayokuja kutawala dunia moja itakuwa ni katiba kutokea China ambayo itaunganisha watu wote wenye kuwajibika kwa usawa na kisheria... Jambo hili litachukua muda ila litatimia... Kwa sasa ufisadi ndio kitu kibaya sana kwenye mataifa masikini ambapo ndicho kitakuwa cha kwanza kuwekewa adhabu kali na serikali moja ya dunia itakayoletwa na watu wenye macho madogo.

Hivyo kwa swali lako, ili Afrika iendelee bila kutegemea mikopo itahitajika kwanza ufisadi na matumizi mabaya ya mali za umma vikomeshwe kwa kiwango kikubwa ili kodi za wananchi ziende kwenye elimu bora ya vitendo ambayo itazalisha maendeleo bila maumivu.
 
Umuhimu gani wakati China ni mkoloni mpya katika Afrika ambaye tofauti yake na wazungu ni kimo chake na wakati? Kwanini hatutaki kujitegemea kwa kuanza kufikiri kama binadamu na si manyani?
Umemaliza yote. Kuna msemo kuwa utumwa ulitufanya akili zetu ziwe tegemezi. Huyu ''mwamba'' yeye badala ya kuhoji ni kwa nini sisi wenyewe tusijitahidi kutengeneza mambo yetu yeye anahoji ni kwa nini tusijiondoe kutoka nchi za Magharibi tukimbilie kwa mchina.🤣🤣🤣🤣🤣
 
Sasa mkuu unategemea nini kwa mtu anaekukopesha mara kwa mara bila kukudai?
Huoni kuna siku atataka usichoweza kumpa?
Mkuu Unashindwa kutofautisha baina ya Mikopo ya kibaishara na mikataba yake na mikopo ya Kimaendeleo.

Mikopo mingi ya Kimaendeleo inakuwa himilivu na Riba ndogo sana, Sema ina masharti, mfano kama unachukua mkopo WA Elimu basi utumie kuendeleza Elimu. Mara nyingi interest rate ni single digit Asilimia 1 mpaka 9.

Mikopo ya Kichina mingi ni ya Kibiashara, yenye Riba kubwa na Huulizwi, kiongozi wa Africa anaweza chukua mkopo akamjengengea Hawara yake Nyumba, baadae wananchi wanalipa Riba na mkopo. China Wana Charge as much as 17% interest rate.
 
Sasa ni hivi mwenye makosa ni mkopaji sio mkopeshaji
 
China yupo Afrika kimaslahi zaidi

Hao so ndio wamekamatwa juzi Dsm wakitutengenezea K-Vant feki kabisa katika hali ya uchafu uliopindukia
 
China ni taifa kiuhalisia bado halijastaabika... mchina mtu wa ajabu saana..

Ukitaka kujua taifa lao lilivyo..kaa jirani na Mchina - hovyo kabisa hawa jamaa
 
Sisi Binadamu ni wanafki sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…