Kwanini hatutambui umuhimu wa China kwa mataifa yanayoendelea?

Hakuna cha bure duniani "there's no free lunch every where in the world"
 
Hivi kati ya Ulaya Magharibi na Ulaya Mashariki ni upande upi umetuibia sana? Mimi naona Waafrika ndio tuna chuki na ubaguzi kwa wachina
Tushasahau tulivyoteswa na hao wa magharibi nyakati za ukoloni na hadi leo hii bado tunatumikishwa na ukoloni mamboleo ila yote hayo tumefubazwa tunahangaika na mchina tu [emoji23]
 
Siko zote nawaambia Waafrika Wenzangu Sehemu pekee tutajifunza maendeleo ya Nchi na Jamii zetu ni EAST ASIA Full Stop.

Wana Juhudi, Nidhamu na Wivu wa hali ya Juu na Nchi zao. Wanasoma sana, Wanafanya kazi kwa muda na wanakamilisha kwa muda,
 
Kaulize nchi wanayoitawala Zambia ni kwanini hawaendelei pamoja na kuwa na shabba nyingi.
Sisi TZ tusiotawaliwa tumeendelea lini pa1 na kuwa na rasilimali za kutosha za kila aina?

Unajisahaulisha kuwa TZ iko dunia ya 3 kimaendeleo si kiuchumi na hata kidemokrasia?
 
60 years of independence still TZ is under dependence economic country as the third party of the world in economic development.

Bado sitakaa niamini kuwa nchi za magharibi zinatupenda kama unavyoelezea hapa.

UN hatuna "veto power" we ni mshiriki bora tu ila maamuzi yote unapangiwa na yale mataifa makubwa kimaendeleo "20 G" kama USA, France, UK, Germany n.k

Tujitafakari kuna sehemu hatuko sawa kama bado tunaamini hatuibiwi na nchi za magharibi.
 
Hoja nzito sana hii Chifu [emoji1666]

Afu mbona miaka ya 1961 TZ tulikuwa sawa kiuchumi na China?

Kwanini tunapenda kulalamika lalamika na kutaka mtelezo tu wa maisha bila kujua hata huyo Mchina mwenyewe kuna kipindi aliumia ndiyomaana sasa hivi anakula mema ya nchi yake?
 
Hebu acha KUKURUPUKA!!! Ulisikia lini nchi yoyote ile ya Magharibi kuchukua asset ya nchi yoyote ile Africa au third World kwa kushindwa kulipa deni!?
[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
Hivi ule mgodi wa Barrick unaochimbwa hapa, unapata asilimia ngapi za kipato chako ktk mgawanyo wa hiyo rasilimali ya TZ?

Bado tu huamini unaibiwa?

Kuna haja gani ya kujiita una rasilimali ilihali anayeichota kwa wingi na kuiuza duniani ni mwingine?
 
China imeligeuza bara la Africa kuwa sehemu ya uchuuzi wa bidhaa zake za kawaida kabisa za viwandani.
 
Wachina wanakukopesha ili ukawe na financial descipline na ufanye basics ila wazungu wanafurahi unapopeleka mkopo kununulia ma v8 make wanajua we hamnazo na daima you can never run away from the poverty line
Maviete ni gari za Mjapani, wajapani sio wazungu.
 
Tatizo sio China bali ni Zambia kwa kukopa bila kujua unaenda kufanyia nini huo mkopo
Kama Wachina wanawapenda sana Waafrika kwa nini wanawakopesha watawala wao bila kudai "business plans" za mataifa yao?
 

Anti China wanataka wakope wale burudani alafu zikiishia wakopeshwe tena.... Yaani maana kamili ya mawazo yao sio kukopeshwa bali wapewe tu kila wakihitaji huku raia wa hizo nchi zinazotukopesha waendelee kulipa kodi kwaajili yetu😁😁

Mawazo yao ni kama si ya kibinadamu kabisa
 
China ni taifa kiuhalisia bado halijastaabika... mchina mtu wa ajabu saana..

Ukitaka kujua taifa lao lilivyo..kaa jirani na Mchina - hovyo kabisa hawa jamaa

Hovyo alafu wakafikaje walipo? Tazameni haya mambo kwa umakini mtagundua mabeberu wanabadili tu style ya utumwa... Tangu utumwa wa kwanza wa kuuza mababu zetu kama bidhaa mpaka utumwa huu wa sasa ambao wanakulazimisha mambo ya hovyo ili wakupe mkopo
 
Siko zote nawaambia Waafrika Wenzangu Sehemu pekee tutajifunza maendeleo ya Nchi na Jamii zetu ni EAST ASIA Full Stop.

Wana Juhudi, Nidhamu na Wivu wa hali ya Juu na Nchi zao. Wanasoma sana, Wanafanya kazi kwa muda na wanakamilisha kwa muda,

Kabisa mkuu. Tatizo lipo kwa viongozi wetu hawajawa serious katika kuiga kikamilifu mbinu za kiuchumi kutoka Asia.
Mabeberu chumi zao zinategemea wizi wa nguvu na ujanjaujanja mwingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…