Kwanini hawa rafiki zangu wanaumia sana mioyo yao

Kwanini hawa rafiki zangu wanaumia sana mioyo yao

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Wakuu nipo Daressalam yapata mwezi sasa, nilitoka mkoani kuja huku kufukuzia fursa mbalimbali na kuongeza exposure.

Ukizingatia mimi sio mtu wa kuishi sehemu moja kwa muda mrefu, kule mkoani kuna ishu zangu ambazo huwa nafanya na zinaniingizia pesa ya kuendesha maisha yangu.

Toka nimekuja huku daressalam sijaweza kufanikiwa kwa lolote, naona watu wengi huku wanaishi kinafiki Sana, kuna rafiki yangu nimejiegesha kwake kwa muda yaani mimi ni kulala tu.. mambo mengine yote namaliza mwenyewe.

Sasa kinachoniacha hoi ni kuhusu hawa rafiki zangu wa dar😀😀 nikinunua kitu kizuri mfano kiatu au simu unaona kabisa wanaumia.

Bajeti yangu toka nimefika hapa huwa nanunua ile chupa kubwa ya maji lita 13 ...napo pia naona wanaumia nahisi walitegemea niteseke😀😀😀😀..
 
Sasa mbn unateseka kwa kuhisi unaonewa wivu..

Enewei.. jitahidi sana ukiwa unajitafuta ktk Mikoa ya watu usipende kufikia kwa ndugu, jamaa au marafiki.

Miaka ya zamani it was Ok, but kwa sasa hali ishabadirika.. ni KERO kwa wenyeji wako.

Jitahidi sana ujitegemee kwa kila kitu hasa swala la malazi.
 
Wakuu nipo Daressalam yapata mwezi sasa, nilitoka mkoani kuja huku kufukuzia fursa mbalimbali na kuongeza exposure..... Ukizingatia mimi sio mtu wa kuishi sehemu moja kwa muda mrefu, kule mkoani kuna ishu zangu ambazo huwa nafanya na zinaniingizia pesa ya kuendesha maisha yangu ...toka nimekuja huku daressalam sijaweza kufanikiwa kwa lolote, naona watu wengi huku wanaishi kinafiki Sana, kuna rafiki yangu nimejiegesha kwake kwa muda yaani mimi ni kulala tu.. mambo mengine yote namaliza mwenyewe..... Sasa kinachoniacha hoi ni kuhusu hawa rafiki zangu wa dar😀😀 nikinunua kitu kizuri mfano kiatu au simu unaona kabisa wanaumia.. Bajeti yangu toka nimefika hapa huwa nanunua ile chupa kubwa ya maji lita 13 ...napo pia naona wanaumia nahisi walitegemea niteseke😀😀😀😀..
sasa maji kunywa unanunua unaweka chumbani kwako unakunywa pekeyako wao wanakunywa ya dawasco, huchangii chochote kwenye chai na msosi unakula kwake na unalala free ulipojiegesha 🐒
huchangii chochote halafu unanunua vitu vya gharama na huna mshipa wa aibu 🐒

badilika na jiongeze bana usiwe mzigo mzito sana wa kuchosha haraka
 
sasa maji kunywa unanunua unaweka chumbani kwako unakunywa pekeyako wao wanakunywa ya dawasco, huchangii chochote kwenye chai na msosi unakula kwake na unalala free ulipojiegesha 🐒
huchangii chochote halafu unanunua vitu vya gharama na huna mshipa wa aibu 🐒

badilika na jiongeze bana usiwe mzigo mzito sana wa kuchosha haraka
Hapa Mimi nalala tu mkuu
 
Pakikucha salama mtafute dalali akuchekie room ukapange tu uanze kuishi mwenyewe. Hapo kidogo utakuwa salama.
Sidhani kama wanakuonea wivu kama usemavyo, ila ni mind set yako tu inakueleza mambo ambayo huenda wao hawana juu yako.


#WivuMpakaKwenyeMaji hii sio sawa!
 
Hakuna wa kukuonea wivu watakuwa wanakushangaa unavo ishi dar ukiwa huelewi dar unatakiwa uweze kujimudu.
 
Back
Top Bottom