Minjingu...
Mimi wala sijipigii zumari langu.
Haya yote yamekuja kwa wewe kunihoji hili na lile.
Umejitakia mwenyewe.
Kwangu haya yamekuwa sehemu ya haiba na maisha yangu.
Wengi mmeumizwa na mimi kuandika historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika na chama cha TANU.
Hampendezewi na huu ukweli na wengine wameonyesha uadui dhahiri dhidi yangu.
Lakini juu hayo yote ukweli ni kuwa hao walioanzisha harakati za kuunda umoja wa Waafrika wa Tanganyika kwa nia ya kudai uhuru baadhi yao ni babu zangu kwa nasaba na wengine kwa ujamaa.
Hili ndilo lililonifikisha hapa nilipo kama unavyoona vyuo nilivyoalikwa kuzungumza na vyombo vya habari vinavyokuja kunihoji.
Umewataja BBC ukidhani labda mie siwajui.
Mahojiano ya kuajiriwa nilifanyiwa na Nelville Helmes Mkuu wa Idara ya Kiswahili.
Umewataja Al Jazeera.
Hawa wamekuja nyumbani kwangu Dar es Salaam na Tanga crew nzima kunihoji.
Matayarisho ya mahojiano kwa sauti na picha ya watu hawa utastaajabu.
Wengi mfano wako wamejaribu kupambana na mimi.
Hawakuweza.
Nimewashinda kwa mbali sana.
Sababu si kuwa mimi nina akili sana.
La hasha.
Historia ya uhuru wa Tanganyika na chama cha TANU ni historia ya wazee wangu.
Nawajua.
Sihitaji kuingia maktaba kusoma chochote kuhusu wao.
Video zangu zinawavutia watazamaji wengi sana.
Nitafurahi kusikia mahojiano yako.
Kaa ukitambua kuwa, ''Mtafuta nyingi nasaba humkuta mwingi msiba.''
Tosheka na haya na endelea na maisha yako.
Kulia Chama Omari Matata, Mohamed Said, Ali Saleh na aliyesimama nyuma ni (Balozi) Mohamed Maharage Juma BBC Club, Bush House, London.
Hamza Kassongo Hour 2007
Taazia ya Ali Nabwa niko nyumbani kwangu Bombo Tanga,
Ali Saleh na Mohamed Ghassani wako Studio za Channel Ten Dar es Salaam