Kuwa kwao mbele ni sababu ya utanganyika wao na sio uislamu ndicho tunachopinga
Inside10,
Hili la Uislam ndiyo chanzo cha tatizo la uandishi wa historia ya uhuru wa Tanganyika.
TANU chama kilichopigania uhuru wa Tanganyika waasisi wake hawakupata kutajwa katika historia rasmi.
Mimi nayajua majina ya waasisi wote.
Nayajua kwa kuwa yaliandikwa katika mswada wa kitabu alioandika Kleist Sykes kabla ya kufariki kwake mwaka wa 1949.
Mswada huu alikuwanao Abdul Sykes had mwaka wa 1968 alipompa mwanae Aisha ''Daisy'' Sykes aliyekuwa mwanafunzi wa Education and History University of East Africa na akaandika seminar paper akieleza maisha ya babu yake.
Hii seminar paper iko Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam East Africana: ''The Life of Kleist Sykes'' (1968).
Semina Paper hii ina majina tisa ya waasisi wa African Association: Cecil Matola (President), Kleist Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Suleiman Majisi, Raikes Kusi na Rawson Watts.
Katika paper hii inaelezwa kuwa Wakristo walikuwa wanaonywa kanisani wasijiusishe na mambo ya siasa.
Hii ndiyo sababu ukiangalia hiyo orodha ya waasisi wa African Association utaona wengi wao ni Waislam.
Baada ya kuunda African Association 1929 Waislam hawa wakaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) mwaka wa 1933.
Naamini umeelewa hoja.
Angalia picha hiyo hapo chini:
Kulia Haruna Iddi Taratibu, Saadani Abdu Kandoro, Julius Nyerere, Sheikh Mohamed Ramia na Iddi Faiz Mafongo Dodoma Railway Station 1955/56