Pole mzee hizi ngano zako za kidini kama ulivyokiri mwenyewe nje wapo watakaokupa attention kwa kiasi fulani lakini Tanzania kwa maana ya taasisi za Elimu hakuna mwenye time nazo😆😅🤣😂 labda kwenye mijadala yenu ya kiislamu na taasisi za kiislamu ndo wanaweza kukupa attention hii ni kumaanisha vitabu vyako vina walakini tena mkubwa sana najua wewe hulioni hilo maana ipo roho nyuma ya wewe kuandika hivi.
Salari,
Unaandika ukiwa una hasira.
Hasira ndiyo inayokufanya wewe utumie hata maneno ya kudhalilisha mathalan kuita kazi ya kisomi ''ngano.''
Wala hii si mijadala ya Kiislam vitabu nilivyoandika na kazi nilizofanya na kuchapwa hazikuchapwa na Waislam.
Mimi niko katika Cambridge Journal of African History na pia katika Dictionary of African Biography.
Hawa ni Waingereza na Wamarekani.
Mada nilizoandika zipo katika maktaba ya vyuo vikuu vingi Afrika, Ulaya na Marekani na ndani ya Library of Congress.
Ukishikilia kuwa hii ni mijadala ya Kiislam unadhihirisha kuwa kwanza haupo katika duru hizi za kisomi na pili una chuki tu na Waislam.
Labda nikufahamishe upate kunielewa vyema.
Soma hapo chini:
Awards: Several Awards
Visiting Scholar: (2011)
University of Iowa, Iowa City, USA
Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin, Germany
Kati yetu mimi na wewe unadhani wa kuhurumiwa na kupewa pole ni nani?
Wa kuwekewa vikatuni vinacheka ni nani?
Mimi au wewe?
Lakini mimi sitofanya hivyo kwani heshima yangu katika jamii hainiruhusu.
Niko hapa kubadilishana mawazo na fikra.
Siko hapa kumkejeli mtu yeyote.