Kwanini Historia ya Wachagga inafichwa Sana?

Wachagga, Wakinga, Wapemba na Wahindi ni makabila ya kuigwa. Ni watu ambao uwezo wao wa akili uko juu kuliko jamii nyingine za ki-tanzania.
Sio kweli sema wana experience ya biashara toka kitambo kwa akili eti ndo wana akili kuliko wote big noooo sema pia waliwahi pata fursa ya shule wazungu walikimbilia kwa wachaga sababu ya rutuba
 
Kijana Tembosa historia ya wachagga inawahusu wachagga wenyewe, sie ya nini? Ukitaka hiyo historia nenda uchaggani ukaisome kwa raha zako mwenyewe, sie wengine haina umuhimu kwetu.
 
Wakati Tanganyika inapata Uhuru kulikuwa na Watanganyika watatu waliotegemewa kupata Urais Kadiri Ya CIA cable ya mid 50s iliyoandaliwa na shushushu maarufu wa enzi hizo ambaye baadaye alikuwa waziri wa nje enzi ya Reagan , FRANK CARLUCCI
watanzania
Julius Nyerere
MANGI Thomas Marealle
Chifu Kidaha Makwaia

Hawa ndio walikua wanaandaliwa kwa siri kuwa rais , wote walikua watoto wa machifu au machifu , kwa hiyo sio kweli kuwa Marealle akitaka Uhuru wa wachaga

Kilichotokea ni kuwa Marealle kutokana na utajiri Mkubwa wa SERIKALI ya CHAGGA ( Kilimanjaro ) alijijengea unaarufu miongoni mwa council cha machifu wa Tanganyika wengi alikuwa akiwapatiaaa misaada ya Maendeleo kwakua walikuwa na instruments zote kuanzia Ikulu (palace) Bunge na Mahakama na akiba ya pesa za kigeni akawa maarufu na Tishio maana kama machifu wangeamua nani atawale Angekua yeye au Makwaia
Nyerere alilijua hilo akisaidiwa na Roman Catholic na Sunni Muslims ambao hawakutaka Marealle atawale kwakua alikuwa Mlutheri hasimu wa Muingereza yaani Ujerumani hivyo Uingereza wanaona bora Mwalimu hivyo Kidaha makwaia akabaki kati

Mwalimu akawa mjanja akaomba kuitwa mkutano wa machifu kuhutubia akaomba waungane na kuahidi kushirikiana nao kutawala ila nao wakubali kuacha uchifu
Wakalubali kuunga mkono Tanu nakutubusu Tanu iingie Kilimanjaro na maeneo mengine aliyokua na nguvu
Baada ya Uhuru Nyerere aliwajeuka Marealle na Kidaha aliwaofiaa aliwapatia machifu wote waliokua na elimu fulani kazi kama Chifu Fundikira, Chifu Mkwawa, Chifu Kunambi etc ambao hawakua na elimu alichukua watoto wao akawasomesha na kuja kuwapa kazi ila akawasaliti Kidaha na Marealle hakuwapa kazi Pamoja na kuwa ndio walikuwa na nafasi kubwa mmoja wao kutawala
Marealle Aliipewa kazi kama balozi wa WFP Italy na UN huku Kidaha aliamua kuhamia Moshi mbali na kwao akiishi maisha ya kipweke kama Mwalimu wa dini katoliki mashuleni akitembea kwa miguu haid alipokuja kiafrika miaka ya mwanzo ya 2000 kama Marealle pia

Kwa kifupi hiyo ndio sababu kubwa ya kuhofiwa watu wa Kaskazini Ndani ya SERIKALI ni kama vile baadhi ya jamii ya Kislamu ambao walisaidia uhuru lakini wakatelekezwa
Hiyo fitna ya kuwa Marealle Alidai Uhuru wa CHAGGA ni moja ya fitna ya kuendelea kuhalalisha mambo yao

Mwalimu badala yake Kanda ya kaskazini aliamua kuwatumia Peter Kisumo, Eliufoo ,Nsilo Swai, Mwapachu na Jackson Kaaya ( badala ya Kirilo ambaye alikua mshirika wa Marealle )
 
Mbona kwenye orodha ya vyeti fake, ingawaje wengine wamerudishwa baada ya kukata rufaa, asilimia kubwa ya surname/ ubini ulikuwa wa hao jamaa.

Hii inatokana na historia ya Elimu nchini Tanzania.

Kipindi cha Mwalimu Nyerere, ili kuleta usawa kwenye Elimu, alileta affirmative action. Hii iliitwa "kupiga mark-time". Kutekeleza sera hii, sehemu zilizoonekana kuwa na Elimu kubwa ziliwekewa pass mark kubwa. Pass mark, alama za ufaulu, zilikuwa juu Kilimanjaro, Dar es Salaam (city centre), kuliko sehemu nyingine.

Matokeo yake ni kusababisha wale "waliofeli" Kilimanjaro na maeneo mengine yenye alama za juu, kukimbia na kwenda kusomea maeneo mengine. Huko walipoenda, mfano Lindi, Singida, n.k. hakukuwa na mwamko mkubwa wa elimu. Wazazi wa maeneo ya huko hawakuona umuhimu wa shule. Watu kutoka Kilimanjaro walitumia hiyo kama njia ya wao kuendelea kusoma kwa kutumia majina mengine ya huko.

Ndiyo sababu leo hii ukikagua vyeti feki utaona wale wanaotoka sehemu zilizokuwa na pass mark za juu wapo wengi. Haina maana hawakuingia darasani na kusoma na kufaulu.

JokaKuu
 
ni tabia ya watu duni km ww kuwachukia waliofanikiwa .mchaga atabaki kuwa mchaga na huo ndio ukweli. walishawaacha. utabaki unaimba singo hyohyo hadi lini? CHEZEA MANGI.
 
KUHUSU AKILI KTK MUKTADHA WA KIKABILA TAFUTA POST YA PASCAL IMEDADAVUA VIZURI.
 
Shida wanajisifia mno bora mkajiweka chini ili mzidi kuchuma maendeleo bora mkawa kama kagera wanajinadi wako nyuma sana wakati vijiji vyao vimeendelea sana mbona
 
Shida wanajisifia mno bora mkajiweka chini ili mzidi kuchuma maendeleo bora mkawa kama kagera wanajinadi wako nyuma sana wakati vijiji vyao vimeendelea sana mbona
Ha ha ha ha ha
 
Safi sana
 
Wachaga ndio wameongoza kwa vyeti fake
Mbona kwenye orodha ya vyeti fake, ingawaje wengine wamerudishwa baada ya kukata rufaa, asilimia kubwa ya surname/ ubini ulikuwa wa hao jamaa.
 
Wachaga hawana kitu ni mbwembwe tu
ni tabia ya watu duni km ww kuwachukia waliofanikiwa .mchaga atabaki kuwa mchaga na huo ndio ukweli. walishawaacha. utabaki unaimba singo hyohyo hadi lini? CHEZEA MANGI.
 
Siku hizi mambo yote ni Chato,maendeleo yote ni Chato....niambie ni kweli ama si kweli?
 
Hakuna kabila linaloitwa wameru hao unaowaona ni wachagga waliohamoa mlima meru wakitokea machame
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…