Ujerumani baada ya vita ya kwanza, uchumi ulidorora lakini wayahudi sababu walikuwa hawaruhusiwi kumiliki ardhi lakini waliweza kuwa na interectural career pamoja na kujiajiri walikuwa wanafanya vizuri kwenye kuuza madini, picha za kuchora na innovations nyingi. Wayahudi wengi ndo walikuwa wasomi wazuri mfano Einstein na wengine wengi hivyo Ingawa Hitler hakuwa mjerumani alikuwa mtu wa Austria aliweza kupata upenyo na kuweza kushinda na chama chake. Hitler alitaka kila mtu amchukie myahudi sababu siyo Caucasian na siyo Aryan yaani watu wenye rangi nyeupe, macho ya blue na nywele blonde ndo wateule waliokuwa wamechaguliwa na Hitler kuwa watatawala ulimwengu. Ndo maana kwenye olyimpic ya 1938? kuna mmarekani alishinda gold medal 4 lakini huyu bwana alikataa kumshika mkono na US ilitishiwa sana sababu ya kuwa na wanegro na wayahudi kwenye timu.
Wayahudi wamekuwa wakimbizi wa kwanza duniani kabla ya kristo ndo maana ukisoma agano la kale unaona Joseph alivyolelewa Misri na vizazi vya wayahudi walivyotoroka toka misri Exodus. Ulaya nzima imejaa mazila ya wayahudi waliokimbia utumwa wa warumi, waarabu na baadaye mauaji ya kimbali ya manazi. Myahudi ni mtu ambaye ameweza kuweka ustaarabu wake kichwani pamoja na kukimbilia kila mahali duniani na ndo maana hata ukienda New York utafikiri upo Jerusalem. History ni ndefu sana ndugu google utawaelewa hawa watu wengine wapo Africa hata Zimbabwe wapo na wana rangi nyeusi kama sisi lakini ni Jews.