Barca
JF-Expert Member
- May 3, 2013
- 1,448
- 1,624
Siyo Ndanda tu ni hospitali zote Ni lazima tujue dini yako. Kuna magonjwa yapo common kwa dini fulani. Mfano wakristo kwasababu wanakula kitimoto wana uwezekano wa kuwa na ugonjwa wa nguruwe tineasisi. Wakati waislam siyo sana. Lakini kuna dini ambazo wao hawaongezwi damu mfano mashahidi wa yehova.Salaam wanajamvi!
Sitaki kuwapotezea muda kwa kuwa nami sipendi kupoteza muda wangu, najielekeza moja kwa moja kwenye mada lengwa karibuni.
Jana nilienda hospitali ya Rufaa ya Mt. Benedikto (St. Benedict, Ndanda, Mtwara) kwa ajili ya matibabu. Nakiri hii ni katika hospitali bora kabisa kwa huku Kusini mwa Tanzania.
Hata hivyo, katika mchakato wa Usajili nilipata ukakasi baada ya kuulizwa dini yangu. Ilinichukua sekunde takribani 20 kutafakari na kujibu swali kwakuwa sikuona haja na hoja ya msingi kwa mteja kuulizwa swali hilo.
Niliamua kumuhoji mhudumu wa mapokezi kuhusu umuhimu wa kuwatambua wateja kwa dini zao, alijibu kuwa yeye hafahamu chochote kuhusu mantiki ya hilo bali anachofahamu hilo ni hitaji la lazima la usajili na mfumo wa usajili hauendelei kama kitarukwa kipengele cha dini.
Kwakuwa jamii Forums ni chaka la magwiji, majagina na maguru naomba kwa yeyote mwenye ujuzi anijuze iwapo ipo hoja na haja ya Mamlaka ya Hospitali hii ya Wakatoliki kuuliza dini za wateja.
Naomba kuwasilisha.View attachment 3251613
Wakristo kutairi ni optional wakati waislam ni lazima. So kuna magonjwa common kwa dini fulani pia.