Kwanini Hospitali ya St. Benedict, Ndanda, Mtwara huuliza wateja dini zao?

Kwanini Hospitali ya St. Benedict, Ndanda, Mtwara huuliza wateja dini zao?

Kwani huyu jamaa yeye ni muhindi au mzungu? kama ulitaka kusema ni wabaguzi basi badala ya racist ( ambao ni ubaguzi wa rangi pekee)ungetumia neno bigot ambao ni ubaguzi wa jumla racial, ,religion,ethnicity etc
If you can discriminate based on religion before providing services, how can you not discriminate based on race?
 
Ili kama ni mwislamu ukiwafia wasisumbuke kupeleka mwili wako mortuary ni kuita tu wachimba mchanga wa pale mwena wakakufukie
 
Hujui maana ya "racists".
Kwani dini inahusiana vipi na ubaguzi wa rangi?
Unaona kumbe hujui what racism is wewe, racism is a form of prejudice mkuu, whereby members of a particular group experience negative emotional reactions, negative stereotypes associated with them, and racial discrimination na huwa inaleta violence mkuu,
 
Sijatafsiri udini mkuu. Nashukuru kwa jibu lako. Je waonaje sensa ya nchi ikahusisha dini ili kusaidia kila mwenye lengo la kukusanya taarifa za kidemografia kwakuwa imeonekana hilo ni jambo muhimu.
Sensa inatumia kodi za wananchi
Hospital ni taasisi ya dini hata Muslim wanaweza kuuliza dini ya mtu kwenye taasisi yao usijitoe ufahamu
 
Wanata ukikata moto na ndugu zako hawajatokea wakuzike kwa heshima zote za dini yako.
 
Salaam wanajamvi!

Sitaki kuwapotezea muda kwa kuwa nami sipendi kupoteza muda wangu, najielekeza moja kwa moja kwenye mada lengwa karibuni.

Jana nilienda hospitali ya Rufaa ya Mt. Benedikto (St. Benedict, Ndanda, Mtwara) kwa ajili ya matibabu. Nakiri hii ni katika hospitali bora kabisa kwa huku Kusini mwa Tanzania.

Hata hivyo, katika mchakato wa Usajili nilipata ukakasi baada ya kuulizwa dini yangu. Ilinichukua sekunde takribani 20 kutafakari na kujibu swali kwakuwa sikuona haja na hoja ya msingi kwa mteja kuulizwa swali hilo.

Niliamua kumuhoji mhudumu wa mapokezi kuhusu umuhimu wa kuwatambua wateja kwa dini zao, alijibu kuwa yeye hafahamu chochote kuhusu mantiki ya hilo bali anachofahamu hilo ni hitaji la lazima la usajili na mfumo wa usajili hauendelei kama kitarukwa kipengele cha dini.

Kwakuwa jamii Forums ni chaka la magwiji, majagina na maguru naomba kwa yeyote mwenye ujuzi anijuze iwapo ipo hoja na haja ya Mamlaka ya Hospitali hii ya Wakatoliki kuuliza dini za wateja.

Naomba kuwasilisha.View attachment 3251613
Hizo ni taratibu za kawaida tuu za utbulisho wa mtu. Hata ukienda polisi unaulizwa jina, dini, umri kabila nk just
 
Wanataka wachukue tahadhari maana wavaa makobaz hawaaminiki wanaweza kumchinja doctor muda wowote
 
Au hii hospital imeanzishwa na wale magaidi wa Cabo Delgado wa Mozambique nini?
Tunajua pembeni ya Mtwara kuna kundi la kigaidi ambalo linawakata watu vichwa na ili usalimike wanakuuliza maswali kutoka kwenye kitabu kitakatifu cha Quran, ukishindwa kujibu wanajua wewe sio muislam wanakukata kichwa
Qur'an sio kitabu kitakatifu ni UONGO bhna
 
Salaam wanajamvi!

Sitaki kuwapotezea muda kwa kuwa nami sipendi kupoteza muda wangu, najielekeza moja kwa moja kwenye mada lengwa karibuni.

Jana nilienda hospitali ya Rufaa ya Mt. Benedikto (St. Benedict, Ndanda, Mtwara) kwa ajili ya matibabu. Nakiri hii ni katika hospitali bora kabisa kwa huku Kusini mwa Tanzania.

Hata hivyo, katika mchakato wa Usajili nilipata ukakasi baada ya kuulizwa dini yangu. Ilinichukua sekunde takribani 20 kutafakari na kujibu swali kwakuwa sikuona haja na hoja ya msingi kwa mteja kuulizwa swali hilo.

Niliamua kumuhoji mhudumu wa mapokezi kuhusu umuhimu wa kuwatambua wateja kwa dini zao, alijibu kuwa yeye hafahamu chochote kuhusu mantiki ya hilo bali anachofahamu hilo ni hitaji la lazima la usajili na mfumo wa usajili hauendelei kama kitarukwa kipengele cha dini.

Kwakuwa jamii Forums ni chaka la magwiji, majagina na maguru naomba kwa yeyote mwenye ujuzi anijuze iwapo ipo hoja na haja ya Mamlaka ya Hospitali hii ya Wakatoliki kuuliza dini za wateja.

Naomba kuwasilisha.View attachment 3251613
mimi nahisi wewe huna exposure au labda una chembe chembe za udini. Hilo swali hata hospital za serikali linaulizwa na kwa taarifa yako hawaishii tu kujua wewe nj muslim au mkristo, hata dhehebu lako linatakiwa kujulikana. Iman za kidini zinasaidia madaktari kujua matatizo ya wagonjwa wao, mfano kipindi cha Ramadhan ukampeleka mgonjwa kazimia, kama ni muislam Dokta si anaweza kufikiri huyu labda swaumu kali? Unajua kwamba mashahidi wa Yehova wao huwa hawaongezewi damu?
 
Sijatafsiri udini mkuu. Nashukuru kwa jibu lako. Je waonaje sensa ya nchi ikahusisha dini ili kusaidia kila mwenye lengo la kukusanya taarifa za kidemografia kwakuwa imeonekana hilo ni jambo muhimu.
Chombo cha Kidini kuuliza dini yako nadhani ni mahali pake, hata Nyerere aliwahi kusema kama Wakristo wanataka kujua idadi yao au Waislam wanataka kujua idadi yao wawa hesabu huko huko kwenye Makanisa na Misikiti yao. Labda hao Hospitali wanataka kujua ni watu gani wa dini ipi wanatumia huduma yao. After all hata Polisi ukifika kama mtuhumiwa unaulizwa jina, kabila na dini yako.
 
Au hii hospital imeanzishwa na wale magaidi wa Cabo Delgado wa Mozambique nini?
Tunajua pembeni ya Mtwara kuna kundi la kigaidi ambalo linawakata watu vichwa na ili usalimike wanakuuliza maswali kutoka kwenye kitabu kitakatifu cha Quran, ukishindwa kujibu wanajua wewe sio muislam wanakukata kichwa
Wacha chuki zako za dini imekujaje uislamu hapo na hiyo spitali ni ya christian wacha chuki wee mbwaa .
 
Nijambo jema kujua mana kunadawa znatengenezwa nakitimoto shehe ili waepuke kukupa hizo
 
Mbona hata hospital za serikali unaulizwa dini na kabila
Hospital gani ? Nlikuwa aghakhan sijaulizwa kitu kama hiyo, na kama wanauliza na wao ni racist pia, hakuna logical explanation ya kumtibu mtu ugonjwa na kujua dini yake na kabila lake. Kunatengeneza matabaka ya upendeleo wa huduma. Mfano kuna siku nlimpeleka mama dental clinic ya muhimbili sasa kwasababu ya jina lake la pili(ubini) na jina la pili la yule docta yalikuwa yamefanana akashow love sanaa, maza hakukaa folen kabisa, hiyo ni jina tu, likaonyesha wapo kabila moja ukapita upendeleo wa wazi na nliufurahia sababu unanifeva mimi, ila ukweli ndio huo, mambo mengine yanatengeneza matabaka
 
Sasa si mjenge hospitali zenu za Sheikh Ally Memorial Hospital nchini kote!! Malalamiko ya nini kwa watu walio jiwekea utaratibu wao?

Au ni kosa kisheria kumuuliza mtu kuhusu dini yake? Na kwa nini mnajisikia vibaya kuulizwa swali la aina hii?
Hili si jawabu Mzee mbona unakuwa na jazba?
 
Ile ni hospitali inayomilikiwa na taasisi kidini. Hivyo, ni dhahili inapata ufadhili kutoka kwa wafadhili na wabia mbalimbali. Hawa wafadhili/wabia huwa wana masharti kadhaa ikiwemo kutokuwa na upendeleo wa kidini katika kutoa ajira na kuwahudumia wateja. Na lazima kuwe na uthibitisho kuhusu hili.
Sasa; kwa upande wa ajira ni rahisi kupata hizo taarifa maana unapoajiriwa kwenye datasheet kipengele cha dini yako kinakuwepo hivyo ni rahisi kupata uwiano.

Upande wa wateja sio rahisi kuthibitisha hilo. Ndio maana hizo taarifa zinaombwa ili mwishoni kuthibitisha watu wote wanahudumiwa bila kigezo cha dini.

Hata hivyo, hapa nimetumia mfano wa hospitali tofauti na hiyo ambayo taarifa za dini ya mgonjwa zinaombwa kwa lengo hilo. Sina uhakika kama na hospitali hii inaziomba kwa lengo linalofanana na hili.

Asante
Hili ndilo jawabu sasa!

Ahsante sana kwa jawabu zuri.
 
Back
Top Bottom