Kwanini hotuba za Wanasiasa wa Tanzania (wa Upinzani na Chama Tawala) ni za kiwango cha chini mno? Nimewawekea mifano ili wajiongeze

Kwanini hotuba za Wanasiasa wa Tanzania (wa Upinzani na Chama Tawala) ni za kiwango cha chini mno? Nimewawekea mifano ili wajiongeze

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
Hivi tatizo ni nini? Hatuna waandishi wazuri wa hotuba? Au viongozi wetu wamepungukiwa kiuwezo?

Hebu angalieni hotuba hii hapa chini jinsi ilivyotulia.


 
Hapa viongozi wetu walikuwa wanatoa hotuba zinazohusu mashirikiano ya kimataifa ktk nyanja mbalimbali kuanzia afya, siasa za kimataifa, ushawishi wa Tanzania ki geopolitics na kikanda.

Kuhusu hotuba inayoangazia masuala ya siasa za ndani ya nchi kama hotuba ya Barack Obama, kwa Tanzania upande wa upinzani wapo vizuri kuainisha changamoto zetu kwa undani kuliko chama cha CCM.

 
..hii hotuba ni kwa ajili ya kumuomboleza Madiba, au kueleza mchango wa Tanzania ktk harakati za ukombozi?

Kwa hotuba za kuchanganua changamoto za ndani ya Tanzania kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa kweli sikumbuki hotuba yoyote ya Jakaya Kikwete ninayoweza kusema naweza kufananisha na hiyo hotuba ya Barack Obama kwa waMarekani kuelezea siasa za ndani ya Marekani kama ktk clip uliyoweka.

Inaonesha mapungufu ya wanasiasa wa CCM iwe kwa wale bado wapo ofisini wakitumikia nchi na hata wale wastaafu.

Ndiyo maana hata kwenda ktk vyuo vikuu kutoa mhadhara au mahojiano viongozi wote wale waliopo na wastaafu wana mkwamo ila Joseph Sinde Warioba na Pius Msekwa wanajitahidi kuchanganua fikra zao kwa kiwango cha kijana kama mimi kuanza kufikiri pamoja na kukubaliana kutofautiana nao ktk baadhi ya maeneo lakini wazee hawa wawili wanasiasa wastaafu wanajitahidi.
 
bagamoyo,

..hebu msikilize John Kennedy ktk hotuba aliyotoa 1962.

..mara ya mwisho mwanasiasa wa Tz kutuunganisha wote, na kutuhimiza kufanya mambo makubwa ilikuwa lini?

" We choose to go to the Moon in this decade and do the other things, not because they are easy, but because they are hard; because that goal will serve to organize and measure the best of our energies and skills, because that challenge is one that we are willing to accept, one we are unwilling to postpone ..." -- John Kennedy



 
Mzee Joseph Warioba anazungumza kwa kutumia fikra kubwa sana ambayo huwezi kuona viongozi wa juu wa CCM wakijaribu kujieleza kwa undani mawazo yao na ndiyo maana unaona waziri wa awamu ya 4 akibahatika kuwemo ktk baraza la awamu ya 5 anakuwa mtu tofauti kabisa maana hawana wanachoamini, kukisimamia au kukitetea kwao ni ajira na siyo wajibu mkubwa kwa nchi.
 
Hapa Kwame Ture anawachambua viongozi maslahi wanaogombea nafasi za uongozi wakiwa hawana chembe ya imani yoyote ya kiitikadi bali zaidi zaidi wanataka nafasi ya kujinufaisha.

Wengine wanajipachika uzalendo, uanamapinduzi, Ari mpya n.k lakini hawawezi kuutetea kwa hotuba katika majukwaa, mimbari wala mahojiano au kwa vitendo tukaona ndivyo wanavyojidai kuwa.

Kwame Ture on The African Bourgeoise and Class Struggle

 
Kingunge Ngombale-Mwiru : Kuyumba kwa waTanzania kwa kukaa kimya na kukosa ujasiri wa kusema ukweli

 
Hivi tatizo ni nini?

Hatuna waandishi wazuri wa hotuba?

Au viongozi wetu wamepungukiwa kiuwezo?

Hebu angalieni hotuba hii hapa chini jinsi ilivyotulia.



Mkuu Americans speak about people,watu,utu,maisha bora ya mtu,Uhuru wa mtu ndiyo priority yake,Huyu magufuli anasema pale singida kuwa uchumi wetu ni zaidi ya kitu chochote including uhai wetu, miundombinu ni bora kuliko watanzania,Kama watanzania tungekuwa watu,tungekuwa na akili .it was a good time to say no to Magufuli.
 
Back
Top Bottom