Kwanini huko Ughaibuni kama Marekani na Uingereza wasomi (Maprofesa na Madaktari) hawashoboki na siasa?

Nkerebhuke

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2021
Posts
796
Reaction score
2,026
Wakuu nimejaribu kufuatilia huko mambele nimegundua wasomi wakubwa hawajitokezi sana directly kupambania madaraka kama huku kwetu gizani Africa. Huko kwa mabeberu wasomi wakubwa wako huru sana (autonomy) kutoa ushauri hata kukosoa huku kwetu wasomi wanatoka jalalani wengine ni chawa promax.

Mfumuko wa bei uko juu, wasomi wapo tu hatuoni maandiko yao wala juhudi zao kulisaidia taifa. Vitu vingi vimepanda bei kuanzia chakula mpaka vifaa vya ujenzi lakini tuna wasomi wa phd ambao ni political decision makers wapo tu.

Ni muda sasa wasomi kuachana na siasa wajikite kwenye utaalamu wao kulisaidia taifa badala ya kulamba ubuyu na kuashia kumtukuza mfalme huku ndugu zao wakiteseka na kuzika ndoto zao.
 
Wakuu nimejaribu kufuatilia huko mambele nimegundua wasomi wakubwa hawajitokezi sana directly kupambania madaraka kama huku kwetu gizani Africa. Huko kwa mabeberu wasomi wakubwa wako huru sana (autonomy) kutoa ushauri hata kukosoa huku kwetu wasomi wanatoka jalalani wengine ni chawa promax

Mfumuko wa bei uko juu, wasomi wapo tu hatuoni maandiko yao wala juhudi zao kulisaidia taifa. Vitu vingi vimepanda bei kuanzia chakula mpaka vifaa vya ujenzi lakini tuna wasomi wa phd ambao ni political decision makers wapo tu!

Nimuda sasa wasomi kuachana na siasa wajikite kwenye utaalamu wao kulisaidia taifa badala ya kulamba ubuyu na kuashia kumtukuza mfalme huku ndugu zao wakiteseka na kuzika ndoto zao.
Huku wengi njaa!.
 
Huko kwa wenzetu wanaanzisha research institutes, unakuta anaanzisha institute ya utafiti wa uchumi Afrika mashariki, humo ndani ya institute wanagawana idara, mmoja ana specialize mambo ya Kenya, mwingine Uganda, mwingine Tanzania. Hata kama Kuna nchi au taasisi au serikali, inataka kufanya maamuzi ya kisera, Wana wa consult na anakuwa na taarifa kiganjani.

Kunakuwa na specialist wa mambo ya Siasa, uchumi, sheria, usalama, mahusiano ya kimataifa. Yaani ukiwagusa ti eneo fulani, Wana taarifa mkononi na wanashauri. Wanaojua DRC ndani nje, Kenya ndani nje, Uganda ndani nje, Tanzania ndani nje. Wanauza ujuzi na taarifa za kisomi.

Sasa hivi DRC imejiunga na EAC, lakini taarifa zilizotamalaki ni za vita, sio fursa za kiuchumi, watanzania wengi tunadharau kilimo Cha mihogo, kumbe Burundi wanasaka unga wa muhogo mahali popote ulipo. Uganda, mchele wa Tizee unawatoa udenda.

Na mengine mengi.

Ma Prof wetu wao wanaishi katika theories, Kila mwaka ataingia Darasani atakuimbia theories za Plato, atarudi mwakani hivyohivyo, lakini watu wanataka waone hizo concept zinaonekanaje na kutumikaje mtaani katika ulimwengu wa Siasa, uchumi, na kijamii.

Ukienda pale Maruku chuo Cha utafiti wa kahawa na migomba, nje ya fensi yao kuna shamba la mwanakijiji lina migomba imedumaa na inaumwa, na kahawa ziko hoi, yaani hata usomi hauonyeshi ujirani mwema na jamii iliyowazunguka! Wananchi wanaona chuo kimekuja kukaba ardhi yao tu. Nenda Mabuki, mifugo ya jirani iko hoi, chuo wanafunzi na walimu wanakariri tu vitabu, hawana hata siku moja kwa mwezi walimu na wanafunzi kwenda Kijiji fulani kuona na mfugaji fulani.

S.U.A, profesa wa kilimoau dokta, hana hata shamba ili atajirike kwa elimu yake.

Kwa hiyo unakuta Prof anakutana na mbunge musukuma au kishimba wanagombania ka nafasi kamoja!.

mmoja akaishia kukiita chuo kikuu jalala, jalala hukaa juu ya ardhi, nadhani ili chuo kile kiwe jalala, lazima kuwepo takataka juu ardhi yake, bila takataka hakuna jalala, na takataka ni huyo Prof
 
Huku wengi njaa!.
Nawaza sana vijana tutajikwamua aje tuachane na nyumba za kupanda maana vifaa vya ujenzi havikamatiki unless ujenge kanyumba mbuzi na uezeke majani. Inflation haikamatiki na wao wanazidi kupigilia misumari kwamba hawafungi mipaka. Dah wasomi mko wapi?
 
Sasa hivi DRC imejiunga na EAC, lakini taarifa zilizotamalaki ni za vita, sio fursa za kiuchumi, watanzania wengi tunadharau kilimo Cha mihogo, kumbe Burundi wanasaka unga wa muhogo mahali popote ulipo. Uganda, mchele wa Tizee inawatoa udenda.

Na mengine mengi.

Ma Prof wetu wao wanaishi katika theories, Kila mwaka ataingia Darasani atakuimbia theories za Plato, atarudi mwakani hivyohivyo, lakini watu wanataka waone hizo concept zinaonekanaje mtaani.

Ulienda pale Maruku chuo Cha utafiti wa kahawa na migombe, nje ya fensi yao kina shamba la mwanakijiji Lina migomba imedumaa na unaumwa, na kahawa ziko hoi, yaani hata usomi hauonyeshi ujirani mwema na jamii iliyowazunguka! Wananchi wanaona chuo kimekuja kukaba ardhi yao tu. Nenda Mabuki, mifugo ya jirani iko hoi, chuo wanafunzi na walimu wanakariri tu vitabu, hawana hata siku moja kwa mwezi walimu na wanafunzi kwenda Kijiji fulani kuona na mfugaji fulani.

S.U.A, profesa wa kilimoau dokta, hana hata shamba ili atajirike kwa elimu yake.

Kwa hiyo unakuta Prof anakutana na mbunge musukuma wanagombania ka nafasi kamoja! Au kishimba, mmoja akaishia kukiita chuo kikuu jalala, jalala hukaa juu ya ardhi, nadhani ili chuo kile kiwr jalala, lazima kuwepo takataka juu yake, bila takataka hakuna jalala, na takataka ni huyo Prof
Umenipa nondo za maana nimefurahi kweli maana niliwahi kusoma journals kutoka OXFAMS wanatujua ndani nje wameeleza mpaka how minority races walivyo take over sehemu kubwa ya soko la tanzania.
 
Wanaridhika haraka Kwasababu hawana malengo binafsi ya muda mrefu.
 
Wakuu nimejaribu kufuatilia huko mambele nimegundua wasomi wakubwa hawajitokezi sana directly kupambania madaraka kama huku kwetu gizani Africa. Huko kwa mabeberu wasomi wakubwa wako huru sana (autonomy) kutoa ushauri hata kukosoa huku kwetu wasomi wanatoka jalalani wengine ni chawa promax.

Mfumuko wa bei uko juu, wasomi wapo tu hatuoni maandiko yao wala juhudi zao kulisaidia taifa. Vitu vingi vimepanda bei kuanzia chakula mpaka vifaa vya ujenzi lakini tuna wasomi wa phd ambao ni political decision makers wapo tu.

Nimuda sasa wasomi kuachana na siasa wajikite kwenye utaalamu wao kulisaidia taifa badala ya kulamba ubuyu na kuashia kumtukuza mfalme huku ndugu zao wakiteseka na kuzika ndoto zao.
Mkuu, katika kipindi baada ya kupata uhuru Mwl. Nyerere alianzisha vita dhidi ya ujinga, maradhi na umaskini. Alikuwa na maana kwamba nchi itaweza kupigana na maadui hao watatu kwa mafanikio, na kugeuka kuwa kichocheo cha maendeleo na hadhi za maisha ya wananchi.

Miaka zaidi ya 60 imepita kwa kile ambacho kihistoria kimeaminika kama ajenda kuu ya nchi huru, kimebakia kuwa kama kiini macho kwa kuwa maudhui, mantiki na hata muktadha vyote vikiwa vimebadilika. Wakati adui wa nne akiongezeka, yaani uduni wa sayansi na teknolojia yake, viongozi wa sasa wenye fikra finyu wala hawaonyeshi kuhangaishwa na maadui hawa wa kihistoria, zaidi ya kuonekana kulinda maslahi yao binafsi ya kiuchumi.

Kinachoonekana sasa ni kujilinda kihoja kupitia takwimu za idadi ya vitu vilivyopo, wala si kwa ubora wa huduma kupitia vitu hivyo. Badala ya kuzungumzia ubora wa elimu inayotolewa, viongozi wao huzungumzia ongezeko la idadi ya madarasa, wingi wa wanafunzi na gharama zinazosemekana kuwa hutolewa bure kwa wanyonge.

Hali hii pia ipo katika afya, na shughuli nyingine zote za kijamii. Chama tawala kwa sasa kinaonyesha kunufaika sana na watu kutopea katika umaskini, ujinga, maradhi na uduni wa sayansi na teknolojia yake. Hunufaika kwa kuwa ipo katika kipindi ambacho kizazi cha watu wasioweza kuhoji, kujitambua, na utayari amauthubutu wa kufanya maamuzi magumu pale inapopasa kufanya hivyo.

Chama tawala kinatumia vibaya vyombo vya dola ili kibakie madarakani. Watawala huishi katika maisha ya ufahari na anasa kubwa, wakati wananchi wengi wakiishi na kutopea katika lindi kubwa la umaskini na ujinga. Licha ya wananchi kikatiba kuwa ndio waajiri wa viongozi, lakini wamekosa mbinu sahihi
za kuwawajibisha watawala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa za huko zinafanywa na watu wenye pesa nyingi sana ndio maana wakichaguliwa wanalinda utajiri wao na nchi yao!

Na nikisema matajiri ni matajiri haswa!

Mahali sisi tunapokosea ni kumchagua mtu yeyote mwenye maneno mengi!

Akisha chukua nchi ananza kuiba na kushindana na wafanya biashara ambao walikuwepo wakati wote!
Madactari na maprofesa wa kule hawana pesa za kushindana na matajiri!

Ndio maana Republicans wa Marekani wameshika bunge,
Democrates ni ya wananchi lakini haina nguvu!

Hata kama wakishinda kura!
Republican ndiyo imeshika bunge!

Mwenye Enzi Mungu atusaidie na kutubariki sisi na nchi yetu Tanzania [emoji1241]! Milele!
 
Wakuu nimejaribu kufuatilia huko mambele nimegundua wasomi wakubwa hawajitokezi sana directly kupambania madaraka kama huku kwetu gizani Africa. Huko kwa mabeberu wasomi wakubwa wako huru sana (autonomy) kutoa ushauri hata kukosoa huku kwetu wasomi wanatoka jalalani wengine ni chawa promax.

Mfumuko wa bei uko juu, wasomi wapo tu hatuoni maandiko yao wala juhudi zao kulisaidia taifa. Vitu vingi vimepanda bei kuanzia chakula mpaka vifaa vya ujenzi lakini tuna wasomi wa phd ambao ni political decision makers wapo tu.

Nimuda sasa wasomi kuachana na siasa wajikite kwenye utaalamu wao kulisaidia taifa badala ya kulamba ubuyu na kuashia kumtukuza mfalme huku ndugu zao wakiteseka na kuzika ndoto zao.
Huku ni mavilaza ni wa mchongo, kule wako vyuoni wanatengeneza wasomi na kufanya utafiti. Tena yule masifa Jiwe aliwachomoa vyuoni ili serikali yake ionekane ni ya wasomi. Waziri awe na digree to inatosha!
 
Huko kwa wenzetu wanaanzisha research institutes, unakuta anaanzisha institute ya utafiti wa uchumi Afrika mashariki, humo ndani ya institute wanagawana idara, mmoja ana specialize mambo ya Kenya, mwingine Uganda, mwingine Tanzania. Hata kama Kuna nchi au taasisi au serikali, inataka kufanya maamuzi ya kisera, Wana wa consult na anakuwa na taarifa kiganjani.

Kunakuwa na specialist wa mambo ya Siasa, uchumi, sheria, usalama, mahusiano ya kimataifa. Yaani ukiwagusa ti eneo fulani, Wana taarifa mkononi na wanashauri. Wanaojua DRC ndani nje, Kenya ndani nje, Uganda ndani nje, Tanzania ndani nje. Wanauza ujuzi na taarifa za kisomi.

Sasa hivi DRC imejiunga na EAC, lakini taarifa zilizotamalaki ni za vita, sio fursa za kiuchumi, watanzania wengi tunadharau kilimo Cha mihogo, kumbe Burundi wanasaka unga wa muhogo mahali popote ulipo. Uganda, mchele wa Tizee unawatoa udenda.

Na mengine mengi.

Ma Prof wetu wao wanaishi katika theories, Kila mwaka ataingia Darasani atakuimbia theories za Plato, atarudi mwakani hivyohivyo, lakini watu wanataka waone hizo concept zinaonekanaje na kutumikaje mtaani katika ulimwengu wa Siasa, uchumi, na kijamii.

Ukienda pale Maruku chuo Cha utafiti wa kahawa na migomba, nje ya fensi yao kuna shamba la mwanakijiji lina migomba imedumaa na inaumwa, na kahawa ziko hoi, yaani hata usomi hauonyeshi ujirani mwema na jamii iliyowazunguka! Wananchi wanaona chuo kimekuja kukaba ardhi yao tu. Nenda Mabuki, mifugo ya jirani iko hoi, chuo wanafunzi na walimu wanakariri tu vitabu, hawana hata siku moja kwa mwezi walimu na wanafunzi kwenda Kijiji fulani kuona na mfugaji fulani.

S.U.A, profesa wa kilimoau dokta, hana hata shamba ili atajirike kwa elimu yake.

Kwa hiyo unakuta Prof anakutana na mbunge musukuma au kishimba wanagombania ka nafasi kamoja!.

mmoja akaishia kukiita chuo kikuu jalala, jalala hukaa juu ya ardhi, nadhani ili chuo kile kiwe jalala, lazima kuwepo takataka juu ardhi yake, bila takataka hakuna jalala, na takataka ni huyo Prof
Ukiacha ushabiki wa kisiasa kumbe una madini kiasi hiki? Chiembe!
 
Umenipa nondo za maana nimefurahi kweli maana niliwahi kusoma journals kutoka OXFAMS wanatujua ndani nje wameeleza mpaka how minority races walivyo take over sehemu kubwa ya soko la tanzania.
Wahindi, wachina na waarabu, wahuni wamewapa fursa zote. Magari yaliyoagizwa juzi moja mil 500 na 600 alipewa tenda Karm Jee!
 
Wakuu nimejaribu kufuatilia huko mambele nimegundua wasomi wakubwa hawajitokezi sana directly kupambania madaraka kama huku kwetu gizani Africa. Huko kwa mabeberu wasomi wakubwa wako huru sana (autonomy) kutoa ushauri hata kukosoa huku kwetu wasomi wanatoka jalalani wengine ni chawa promax.

Mfumuko wa bei uko juu, wasomi wapo tu hatuoni maandiko yao wala juhudi zao kulisaidia taifa. Vitu vingi vimepanda bei kuanzia chakula mpaka vifaa vya ujenzi lakini tuna wasomi wa phd ambao ni political decision makers wapo tu.

Nimuda sasa wasomi kuachana na siasa wajikite kwenye utaalamu wao kulisaidia taifa badala ya kulamba ubuyu na kuashia kumtukuza mfalme huku ndugu zao wakiteseka na kuzika ndoto zao.
Wanaitumia taaluma yao kuandaa future ya nchi yao na vizazi vyao kwa 100+ years mbele
Sisi huku Maprofesa wanakimbilia siti za mbele👇

1673765725467.png
 
Huko Ulaya na Marekani Wasomi Maprofesa na madaktari wana fursa nyingi sana nje ya siasa na zinalipa vizuri sana tofauti na hapa kwetu ambapo siasa ndio fursa ya kupata mafanikio makubwa kwa haraka zaidi.

Ulaya na Marekani Wasomi wanaweza kupata kazi makampuni makubwa yanayo operate dunia nzima, wanaweza kuwa wachambuzi katika vituo vikubwa vya Television, wanatumiwa kama consultants sehemu nyingi za dunia, wanaweza kuandika vitabu ambavyo vinawapatia mamilioni ya dollar. Hii ni tofauti sana na hapa kwetu ambapo fursa kama hizo hazipo na malipo ya kufundisha ni madogo sana pia, hivyo siasa inabaki kuwa fursa nzuri zaidi kwao.
Wakuu nimejaribu kufuatilia huko mambele nimegundua wasomi wakubwa hawajitokezi sana directly kupambania madaraka kama huku kwetu gizani Africa. Huko kwa mabeberu wasomi wakubwa wako huru sana (autonomy) kutoa ushauri hata kukosoa huku kwetu wasomi wanatoka jalalani wengine ni chawa promax.

Mfumuko wa bei uko juu, wasomi wapo tu hatuoni maandiko yao wala juhudi zao kulisaidia taifa. Vitu vingi vimepanda bei kuanzia chakula mpaka vifaa vya ujenzi lakini tuna wasomi wa phd ambao ni political decision makers wapo tu.

Nimuda sasa wasomi kuachana na siasa wajikite kwenye utaalamu wao kulisaidia taifa badala ya kulamba ubuyu na kuashia kumtukuza mfalme huku ndugu zao wakiteseka na kuzika ndoto zao.
 
Tuna taasisi ya serikali ya utafiti wa teknolojia za ujenzi, Ina watumishi wa kutosha, wanaona wananchi wanajenga nyumba za tofali za kuchoma, nyumba ambazo zinaweza kuishi miaka elfu, hivi hawajagundua njia rahisi ya kuchoma tofali? Tena kisasa ziwe zimenyooka vizuri?

Wananchi hawamudu bei ya simenti, iko juu

Back
Top Bottom