Kwanini huko Ughaibuni kama Marekani na Uingereza wasomi (Maprofesa na Madaktari) hawashoboki na siasa?

Namba moja malipo yao sio haba,

Namba mbili think tank za nchi ziko vyuoni, watengeneza think tank ambazo zinashiriki kutoa direction za nchi,

So wanasiasa wanabaki kuimplement mawazi ya majopo ya wanazuoni,

Heshima pia ni kubwa sana, South Korea professor anaheshimika sana, wanasema anachukua nafasi ya pili kwa heshima ya kwanza ni ya mungu
 
Kule ma Prof na wasomi wanalipwa vzuri kuliko wana siasa...wana pesa za research za kufa mtu, kutwa kukimbizana na reasearch, na hawazitafuti zinawafuata wao...Huwezi myumbisha mtu mwenye pesa na hana muda wa mchezo mchezo...huku Tz ma Prof wanalipwa kiduchu na wapo idle, shida inaanzia hapo.
 
Point kubwa sana jinsi viongozi wetu wanavyojilonda na hoja dhaifu.
 
Wanasiasa wengi katika nchi za kiafrika ni wezi
 
Huko kipato kinaendana na uwezo wa kuelimu, huku wenye vipato vikubwa ni wanasiasa. Na ukiwa mwanasiasa hasa wa CCM, unaweza kufanya biashara ukawa na kinga ya kutokulipa kodi.
 
Mkuu

Sababu kuu ni kwamba

Hawajaifanya SIASA kama kazi inayolipa mapesa Mengi kama huku bongo!!

YAANI SIASA kwao ni KAZI ya kawaida yenye malipo ya kawaida na professionals zinalipa kulikot hata siasa!

Huku kwetu kinyume CHAKE!
Kabisa siasa ni passion kwao sio sehemu ya maslahi.

Nchi kama U.K. Rish Sunak alikuwa na kampuni yake ya hedge fund ingeweza kumuingizia hela kushinda siasa na mkwewe familia yao ni filthy rich.

Savid Javid kaacha six figures sums plus bonuses za investment banking, kuingia kwenye.

Shadow Chancellor Racheal Reeves keshashika senior post kwenye central bank yao, kawa mshauri wa U.K. government in dealing with USA, kaenda private banking na kabla ya kuingia siasa rasmi alikuwa na job offer ya six figures J.P Morgan akaikataa.

Phd akiingia humo amtishi mtu sio kwa hoja tu na paper yake yenyewe wanaweza ichambua on merit kumwambia its bias mwenyewe akakimbia. Kuna mijitu humo kwenye bunge lao imebobea kwenye kila sector na wana first degrees tu.

Wako wengi sana, sema wana one thing in common wote hao walishiriki siasa za vyama wakati wapo vyuoni, baadae wakishafanikiwa kwenye maisha through their proffesions wanarudi kwenye siasa, ni passion to make changes more than anything.

Ila huko kwenye civil services wamejaa Phds.
 
Kule siasa ni wito, huku siasa ni ajira
P
Umenena, especially hapa Tanzania hatutaendelea kamwe Kama taifa.wanaotakiwa kufanya tafiti kuisaidia nchi wamesogezwa kwenye siasa na Sasa hawana hamu na uprofesa wala udaktari waliouhangaikia. So sad nchi ya masikitiko
 
Mkuu

Sababu kuu ni kwamba

Hawajaifanya SIASA kama kazi inayolipa mapesa Mengi kama huku bongo!!

YAANI SIASA kwao ni KAZI ya kawaida yenye malipo ya kawaida na professionals zinalipa kulikot hata siasa!

Huku kwetu kinyume CHAKE!
Sijawahi ona nchi Kama Tanzania hata Kama huna elimu,unaweza kulala unaamka na kukutana umeteuliwa kuwa waziri tena wa fedha,hatari sana
 
Bongo wengi wanaingia kwenye siasa kwa ajiri ya njaa hata yule wa majalalani alikiri hilo, kwa US au Western countries maprofesa na madaktari wengi wana ajira nzuri na wanalipwa vizuri sana kuliko hata wanasiasa, lakini sio kama hawapo kwenye siasa wapo wengi tuu ila wengi hawapendi kujitambulisha kama maprofesa au madaktari wanatumia majina yao ya kawaida tuu, mfano Obama alikuwa Law Professor lakini hukuwahi kumsikia akijitambulisha kwa hiyo title, Africa hata zile za kupewa wanajitambulisha nazo
 
Kumbe kuna wakati huwa unaandika mambo ya maana!! Inaonekana akili nzuri unayo, sasa muda mwingine sijuo kwa nini huwa unajitoa ufahamu.

Kwa ujumla, leo umetoa mchango solid.

Tanzania, wengi tunaowaita wasomi, ni waganga njaa. Yaani watu wenye uelewa duni kabisa, wataalam wa kukariri, na wengine wataalam wa kununua vyeti, ndiyo tu awaita wasomi
Sasa hivi kila mwanasiasa, hata mwanasiasa mbumbu, anataka aitwe dokta. Wanasiasa pekee ambao hawahangaiki kuitwa madokta ni wa vyama vya upinzani. Lakini huko CCM, ni uchafu mtupu. Wanatumia pesa zao kuupata udokta. Ebu wafikirie wafuatao:

1) Musukuma - dokta
2) Mwigulu - dokta
3) Biteko - dokta
4) Jaffo - dokta

Kibajaji, huenda naye anausaka udokta.
 
Umenipa nondo za maana nimefurahi kweli maana niliwahi kusoma journals kutoka OXFAMS wanatujua ndani nje wameeleza mpaka how minority races walivyo take over sehemu kubwa ya soko la tanzania.
Kula Australia kuna conference huwa inafanyika kila mwaka juu ya Africa mineral potential. Nilihudhuria mara 3. Kila nilipohudhuria, mwafrika nilikuwa pekee yangu. Mara moja, weusi tulikuwa wawili, lakini mwenzangu alikuwa Muingereza.

Ukihudhuria zile conference utajua utajiri wa madini yote yaliyopo Afrika, na utajua pia nani anafanya nini katika nchi gani kuhusiana na madini, Afrika. Na yote unayapata toka kwa wazungu.

Wakati wazungu wakiwa wanafanya hayo, viongozi wa Afrika wao wanapanga mbinu usiku na mchana wataiba kura namna gani ili wabaki madarakani. Na wananchi wa kawaida watakuwa kwenye mabishano juu ya ushabiki wa vyama.
 




Huyu hapa msomi, mwanaharakati, mpigania haki za watu, mwanamageuzi, mwenye/ana ndoto (i have a dream), mwanasiasa...

Wasomi wa aina gani una wazungumzia?

Wasomi ni wengi sana na wameingia katika siasa...

Usitake kusema nchi zao wanasiasa wote ni wana elimu level ya wakina msukuma, kibajaji, kishimba, tabasamu, lema, wenje, mbowe, msigwa nk...
 
Nchi za ulaya haziongozwi na madakitari wala maprofesa feki, sijawahi kusikia rais wa marekani akiitwa dokta, wala rais wa nchi yoyote ya ulaya akiitwa dokta.
 
Point yako tamu sana kuisoma, mabunge ya nchi za mabeberu yana vichwa kwelikweli, unaweza kuingia na paper yako ukaikimbia mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…