Kwanini hutaki kuonana na watu wa kijijini kwenu hapa mjini?

Kwanini hutaki kuonana na watu wa kijijini kwenu hapa mjini?

Wengi wao wambea na kuchunguza hali za maisha tu, especially kwa wale walokua vipanga shulen alafu wakasoma ad chuo na wakapigika mtaan kwa kukosa ajira hua wanachekwa na kudharauliwa sana na wale walioanza kujiajiri mapema na pia wapo mbali kimaisha
 
Kwema Wakuu,

Kama kichwa kinavyojieleza, ni sababu gani inayokufanya usitake kuonana na watu wa kijijini kwenu hapa mjini?

Mimi: Kwa sababu mambo yangu hayajakaa sawa. Wewe?
Tatizo sie kijijini kwetu tunakula sana panzi (senene) na kumbikumbi na tunaona sifa, wakija nyumbani hawa ndugu zangu wataanza kuokota kumbikumbi na senene wote hapa mjini na kuuza hapa mtaani.
 
Swala la kuzikuta habari zangu kwa majirani kule kijijini(unashangaa wazazi wako ndio wanajisikia unyonge wanavyoongelewa utafikiri kosa ni lako) ati hana kitu yule ama visifa viwili tu sizitakagi

😀😀

Visofa vya laizer
 
Huu uzi unawahusu watu wa mikoani niwaachie mjadili, ngoja mie nijipongeze na machungu ya kufa kiume Kule Misri
 
Back
Top Bottom