Kwanini huyu anayesemekana kuwa ni mwanajeshi anayetuhumiwa kubaka alikuwa hajafungwa pingu? Na hao waliokuwa wanaongozana naye ni akina nani?

Raia anayetakiwa kuwa na nidhamu namba moja na isiyotiliwa shaka nchini ni askari wa JWTZ kutokana na kubanwa kwake na sheria zote za kiraia na kijeshi mtawalia.

Askari ama ofisa afanyapo kosa kambini hukabiliwa na mashitaka ya kijeshi , kuna summary trial kwa askari wadogo na kuna court martial kwa wote, askari na maofisa wao pamoja na raia kwa ujumla wake.

Summary trial huendeshwa na wakuu wa vikosi kwa makosa madogo madogo kwa askari, lakini Court martial huendeshwa na wanasheria wa kijeshi ambao huitwa mawakili (advocates).

Hawa mawakili hufanya kazi zote za kuendesha mashitaka na kutoa miongozo ya hukumu kwa mujibu wa sheria katika mahakama za kijeshi.

Afisa, askari ama raia anaweza kushitakiwa katika mahakama hii kutokana na kosa atalokabiliwa nalo.

Kuhusu mwanajeshi kuwajibika na sheria za kiraia, ni kwamba: mwanajeshi awapo nje ya kazi za kijeshi, mfano kupiga raia, wizi, ujambazi, mauaji nk nk, atakamatwa na kisha mkuu wa kikosi chake ataarifiwa na kama atatenda kosa uraiani na kukimbilia kambini, basi vyombo vya sheria (civ Police) wataomba kibali cha kumkamata kwa mkuu wake wa kikosi na MPs watumika kumkamata na kumkabidhi kwa Polisi.

Mwenendo wa mashitaka unatakiwa ufuatiliwe na Adjutant wa kikosi na kutoa ripoti kwa mkuu wa Kikosi namna mwenendo wa kesi unavyokwenda mpaka siku ya hukumu.

Kama mshitakiwa atapatikana na hatia atahukumiwa na kutumikia adhabu yake kama mwananchi mwingine yeyote.
Yapo maelezo mengi kuhusujambo hilo, ila haya maelezo mafupi waweza kupata mwanga.

Huwa hakuna sheria wala muhali kumlinda mwanajeshi anayefanya makosa ama uhalifu.

Ndomaana nikasema anatakiwa kuwa mnyenyekevu sana kwa sababu amelengwa na 'mishale' mingi.
 
Kwamba,mwanajeshi anakabidhiwa kwa Polisi? Hilo jeshi la nchi gani mkuu? Ikiwa hivo,basi hali si shwali kiaina. Hata mwanajeshi alieretire,kasoro tu Bongo labda, bado huwa chini ya uangalizi wa jeshi. Kasoro waliofukuzwa kwa utovu wa nidhamu.
 
Kwamba,mwanajeshi anakabidhiwa kwa Polisi? Hilo jeshi la nchi gani mkuu? Ikiwa hivo,basi hali si shwali kiaina. Hata mwanajeshi alieretire,kasoro tu Bongo labda, bado huwa chini ya uangalizi wa jeshi. Kasoro waliofukuzwa kwa utovu wa nidhamu.
Nilichogundua kuhusu wewe ni kwamba una over expectations sana kuhusu Jwtz.

Hivi mtu layman asiyeelewa lolote kuhusu sheria za kijeshi anaweza akashupaza shingo na kutetea uongo jamvini?

Hili ni jukwaa huru, aje yeyote anayefahamu sheria za kijeshi akanushe kama niliyoongea ni ya uongo.
 
Muulize kidogo kama anaifahamu kiasi Gani juzuu ya Pili.
 
Muulize kidogo kama anaifahamu kiasi Gani juzuu ya Pili.
Ndio maana Mimi binafsi sikuona sababu ya ku-argue na mtu mwenye akili kiduchu namna hiyo, badala yake kwenye moja ya comment yangu ya hapo mwanzoni nilimjibu kwa kufupi kabisa kwamba "You are completely Wrong and out of point."

In short that person is a FOOL, therefore, please don't argue with a FOOL because BRAVE people won't notice the difference.
I think you understand me.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…