..IGP Sirro na jeshi la Polisi wamekuwa mstari wa mbele kukemea wanasiasa wanatoa kauli ambazo ameziita za kichochezi, na za shari.
..Kauli ambazo IGP amekuwa akizikemea mara nyingi huelekezwa kwa Nec na Wasimamizi wa uchaguzi.
..Je, tatizo ni wanasiasa wakorofi na washari, au tatizo ni ukosefu wa maadili wa watendaji wa tume na wasimamizi wa uchaguzi?
..Yapo malalamiko nchi nzima ya wagombea wa vyama vya upinzani ambao wameshinda rufaa zao; tume imewaruhusu waanze kampeni, lakini wakurugenzi na wasimamizi wamekataa kutoa barua za kuwatambua.
..Je, wakurugenzi na wasimamizi waliogoma kuwatambua wagombea halali wa upinzani hawatishii amani? Je, hawawezi kusababisha machafuko?
..Kwanini IGP Sirro na jeshi la Polisi wamefumbia macho suala hilo, na hawakemei wakurugenzi na wasimamizi wanaokiuka sheria na taratibu za uchaguzi waziwazi?
cc tindo, Nguruvi3, Erythrocyte , Pascal Mayalla