SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Mada zangu zina kawaida ya kuwa mbele ya muda. Ukija kibishibishi muda utakuumbua.
Kuna siku nilihoji uhalali wa kusema ligi ya NBC ni ya 5 kwa ubora Africa, wengi wakanibishia bila chanzo cha kuaminika cha hiyo ranking. Matokeo yake sasa hivi, kila mtu, kuanzia mashabiki, wachambuzi hadi makocha wanahoji pia.
Dunia nzima, derby inaitwa jina la sehemu ambapo timu mbili husika zipo eneo hilo. Sihitaji kukupa mifano, itafute au ulizia utaambiwa derby zote duniani.
Kuna hii derby inayohusisha vilabu vikongwe vya Simba na Yanga. Derby hii imebatizwa jina la Kariakoo Derby.
Ukiangalia katika muundo wa kiserikali na kiutawala, makao makuu ya Yanga pale Jangwani hayapo katika kata ya Kariakoo. Ni Simba pekee iliyo katika kata hiyo. Yanga ipo ama kata ya Jangwani au ya Mchafukoge.
Ushauri wangu, tubadili jina la hii derby ya Simba na Yanga iitwe Dar es Salaam Derby. Mbona jina zuri tu.
Kwa nini tuibrand Kariakoo, eneo ambalo pamoja na umuhimu wake kibiashara halina mvuto wowote kwa watalii. Tuibrand Dar es Salaam tutafaidika zaidi na pia tutaepuka upotoshaji wa maksudi.
Katika clip hii hapo juu ni mkazi wa Jangwani na Mchafukoge akiadabishwa baada ya kuleta ujuaji maeneo ya Kariakoo.