Kwanini Ikulu hawapokei simu zinazopigwa kwenye line walizotuwekea?

Kwanini Ikulu hawapokei simu zinazopigwa kwenye line walizotuwekea?

Huwa wanapokea.kipindi cha jpm niliwahi kuwapigia na kuwaandikia kupitia email walinijibu.Labda huwa wanaenda na upepo wa bosi
 
Kama wanashindwa kupokea e mails na cm zilizoko mezani kwao je muda wa "kujisomea" na kutekeleza hiki tunachoandika watatoa wapi??
Wanatusoma sana, trust me. Lakini ndio hivyo wanasema kelele za mlango...
 
Kuna watu wanaamini kufanyakazi Ikulu ni kama wapo Mbinguni. Hivyo wanaamini katika MAAMUZI YAO.

PSU wanapaswa kufahamu kuwa Ikulu ni mali ya wananchi. Wamsaidie Rais kutimiza wajibu wake na wasimfanye Rais kuwa unreachable...

Mabadiliko ni tiba ya wakati

wenzako wanaamini wapo pale kumtumikia tajiri aka Rais na sisi wengine ni vibwengo fulani tu, sidhani kama hata wanafahamu ni kodi zetu ndio zinawafanya waishi vizuri.

Wengine hata kazi zenyewe ni kamlete hakuna competency wala proffsionalism iliyowaweka pale zaidi ya mjomba/mama/baba/ shangazi nk..
 
Ndo utakatifu wa Ikulu yetu ulivyo kwa sasa.

KAMLETE 🤣🤣
 
Njoo hapa getini acha kimemo chako afu endelea na kazi zako, ujumbe utafika mapema zaidi.

Ahsante
 
Kuna mdau kashauri nifunge safari hadi getini Ikulu.

Dunia hii ya kidijitali nisafiri toka Kamachumu hadi getini Chamwino kwa tatizo linalomalizwa kwa mtu kuinua tu mkono kupokea simu!

Kwanini huyo anayekaidi kupokea simu za wananchi asiwajibishwe na wakubwa wake kazini?

Nafahamu wanasoma haya tunayoandika, wabadilike.
Watanzania tupo milioni 60+

Chukulia wenye simu na shida kama yako wapo milioni 3 tuu, mheshimiwa ataweza kuwasikiliza wote hata akigawa muda kwa mwaka mzima HAIWEZEKANI

Andika barua pepe, au barua ya kawaida hatakama hatajibu ujue ujumbe utamfikia na swala lako litatatuliwa kwa haraka KULIKO KUKATA SIMU NA KUPIGA TENA NA TENA
 
Watumishi wa Umma wengi Waporipori.
Mimi nimemwandikia barua Rais kupitia email ya Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi tangu mwezi mei mwaka huu,haijajibiwa.Ila wakati wa JPM walikuwa wanajibu.
Wanajua wasipo jibu utakutana nae kwenye mikutano
 
Watanzania tupo milioni 60+

Chukulia wenye simu na shida kama yako wapo milioni 3 tuu, mheshimiwa ataweza kuwasikiliza wote hata akigawa muda kwa mwaka mzima HAIWEZEKANI
Kapewa wasaidizi. Zile namba hazikuwekwa pale ili azijibu yeye. Awasukume hao wasaidizi wake kutimiza wajubu wao.
 
Kwenye tovuti ya Ikulu zimewekwa namba za simu unazoweza kutumia kuwapigia simu. Ukipiga kupitia namba hizo simu inaita pasipo kupokelewa, tatizo ni nini?

Simu zinapokelewa Ikulu ya Marekani, hata taasisi kongwe na tajiri kuliko taasisi nyingine yoyote duniani, wenye makao yao makuu Vatican wanapokea simu.

Kuna kitu gani hasa kinachozuia simu za wananchi zisipokelewe Ikulu yetu? Ikulu ni ofisi ya umma, wahusika mlijue hilo.
Tuma hata sms wahangaike nayo, potelea mbali
 
Wafanyakazi wote wapo busy kwenye ziara ya mama wanaizunguka dunia na majiji yake
 
Kama hawapokei kwanini usiende kabisa mwenyewe pale getini? Ninaamini watakupokea na kukupa huduma nzuri kabisa, amini au usiamini
Mwambie aanze kujifunza na lugha ya kitutsi maana pale getini wapo wale jamaa wa tolu au washarudi kwao?
 
Kwenye tovuti ya Ikulu zimewekwa namba za simu unazoweza kutumia kuwapigia simu. Ukipiga kupitia namba hizo simu inaita pasipo kupokelewa, tatizo ni nini?

Simu zinapokelewa Ikulu ya Marekani, hata taasisi kongwe na tajiri kuliko taasisi nyingine yoyote duniani, wenye makao yao makuu Vatican wanapokea simu.

Kuna kitu gani hasa kinachozuia simu za wananchi zisipokelewe Ikulu yetu? Ikulu ni ofisi ya umma, wahusika mlijue hilo.

Tasisi Nyingi za UMA zina huu UJINGA.

They Always never give attention to the Public kupitia hayo ma simu yao.

Kumbe baraka zote huanzia IKULU, sikulijua hili.
 
Mimi nilikuwa nataka turuhusiwe kwenda kufanya utalii wa ndani kama wafanyavyo pale White House
 
Back
Top Bottom