Daudi1
JF-Expert Member
- Dec 14, 2013
- 12,444
- 18,741
Salamu nyingi ziwafikie popote mlipo.....
Niende moja kwa moja kwenye mada kama kichwa cha mada kinavyojieleza, kwanza ijulikane maisha tunayoishi hatuishi kwa ajili yetu, yaani maisha yako ili yaende yanategemea watu wengine hakuna anayeweza kuishi kwa kujitegemea mwenyewe, vivyo hivyo hata katika mahusiano ili furaha na amani ipatikane inategemea na mchango wa mwezi wako katika maisha yako, yaani mwanaume hawezi kuishi bila mwanamke na mwanamke hawezi kuishi bila mwanaume. katika mazingira hayo kwasababu tumelelewa katika mazingira tofauti hata kama tungelelewa katika mazingira yale yale bado hali kukosana na kutoelewana isingekosekana hivyo kiunganishi cha kutufanya tuendelee kuwa pamoja au mahusiano yaendelee kudumu ni msamaha.
Msamaha ni hali ya kuondoa uchungu,manung'uniko au malalamiko juu ya mtu aliyekukosea, lengo nikukufanya ubaki huru ndni ya moyo wako. kumbuka usipokuwa mtu wa kusamehe uwezekano wa kuishi maisha marefu haupo, uwezekano wa kufanikiwa katika maisha yako haupo. Hebu tuangalie baadhi ya mambo yanakwamisha au yanaweka uzito katika kutoa msamaha:-
1. Kujihesabia haki;
Hapa mtu huwa anajiona hastahili kukosewa ama kutendewa aliyotendewa labda kwa sababu ya hadhi aliyonayo au kwa sababu ya wema aliouonyesha, na hapa huwa tunajisahau kuwa hata sisi huwa tunakosea, ukijua kuwa na wewe unakosea inakuwa rahisi kutoa msamaha, hebu angalia mfano huu, wa mama na mtoto, mtoto anapovunja glass atachezea fimbo za kutosha na maneno juu, lakini mama huyo huyo akivunja glass atasema bahati mbaya, hata maandiko yametukataza kujihesabia haki("Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani,ambaye afanya mema,asifanye dhambi.Tena usitie moyoni mwako maneno yote yaliyosemwa;usije ukamsikia mtumwa wako mwenyewe ali akitukana,kwakuwa moyoni mwako pia unajua ya kwamba wewe mwenyewe umewatukana watu wengine" mhubiri 7;20-22)
2.Kuangalia ukubwa au kiwango cha kosa ulilotendewa
hapa pia kuna tatizo tumekuwa wepesi kuyagrade makosa kwamba hili kubwa kuliko lingine, utasikia mtu anasema kwa hili hapana, ukiwa na uhakika kabisa kama wewe shetani anaweza kukupitia ukatenda kosa kwani huyo shetani ahwezi kumpitia mwenzako?? mwanaume akichepuka ni shetani amempitia ila mwanamke akichepuka ni malaya,kwa hali hii mahusiano mengi hayajafika mwisho sawa sawa na yalivyoanza
3. Kukumbuka yaliyopita
Lazima utambue kila siku ni mpya inakuja na mambomapya, kila mwaka ni mpya, sasa unakuta mtu wengine tunasherehekea mwaka mpya yeye ule mwaka unabadilika namba tu lakini hakuna kinachobadilika katika maisha yake, ana machungu ya yote aliyotendewa na mwenzake miaka iliyopita, na hii hali ya kukumbuka na kuhesabiana makosa inaua mahusiano kwa haraka mno, lazima tuwe wepesi kuachilia ili mambo mengi yaende, kumbuka nimesema tunaishi kwa ajili ya wengine, maana yake tusiporekebisha hapo wapo watakaoumia kwa sababu hizo mna mara nnyingi wahanga ni watoto.
4. Kiburi na jeuri
Kuna wengine wana kiburi cha asili yaani wao ukiwatendea kosa hawakubali kusamehe ndio wale wanafika mbali hata kwenye msiba wangu aliyenikosea asije, ukikutana na mwanamke wa namna hii au mwanaume usianzishe naye mahusiano utakuja kunishukuru baadaye, yaani ukianzisha mahusiano na wa aina hii umejichimbia kaburi au umeingia kwenye moto, na mara nyingi sio mara zote kiburi au jeuri vinahusishwa na ushirikina na uchawi.
Hatua nzuri zitakazokusaidia kusamehe kwa haraka
1. Kutambua kuwa hakuna aliyemkamilifu hata wewe unakosea
2. Angalia mazuri ya huyo aliyekukosea kuliko mabaya hii itakusaidia kuachilia na kuondoa uchungu ndani yako, kwa mfano amechepuka na ukifikiria siku aliyoanza kuchepuka ulimnyima chakula cha usiku itakusaidia kuondoa uchungu.
3. jitahidi usiwe mwenye kutunza mambo kwa muda mrefu, kumbuka pamoja na kuwa tunaishi kwa ajili ya wengine lakinimsamaha ni kwa ajili ya ustawi wako mwenyewe.
NAOMBA NIISHIE HAPO, SAMAHANI KWA ANDIKO REFU MAANA WENGINE HAWAPENDI, KARIBU KWA MCHANGO ZAIDI KATIKA YALE AMBAYO SIJAYAGUSIA UWE NA SIKU NJEMA