Kwanini inashauriwa duniani kote Watu wa Usalama ( Intelligence ) lazima watokee katika Familia ambazo zina Historia ya kuweko huko?

Leo GENTAMYCINE Kazi yangu Kubwa katika huu Uzi ni Kusoma tu Comments zenu ili Nielimike zaidi nikiamini kuwa hapa JamiiForums kuna Wabobezi na Wazoefu wa Fani hii inayoitwa ya Wenye Nchi.
Wanakua na vinasaba vya kubeba siri ndani yao,pia hujifunza toka kwa wanafamilia AMBAO wamewahi KUWEPO kitengo yaani maisha yao huwa somo kwao HIVYO ni rahisi na wao KUINGIA na kutekelezwa majukumu ya wenye nchi!!
 
Na East Africa unaomba vipi? Tujuze.
Hizi nchi za kusadikika hata kazi ya bar maids wanaitana kimchongo.

Zamani special branch ilikuwa inachukuwa yenyewe wanafunzi bright vyuoni, lakini tangu wameingia kizazi cha ubinafsi kitengo kimekuwa ni urithi wa familia.

Hata JWTZ ni hivyo hivyo kila Askari mwenye influence lazima aingize ndugu zake.

Unajuwa tatizo ni nini, ni nchi zilizokosa fursa nyingi za ajira.

Binafsi nilikataa kuingia Jeshi ni nilipewa nafasi za kupendelewa lakini kuishi kwa Amri na kunyenyekea ni kitu siwezi kufanya.
 
Wanakua na vinasaba vya kubeba siri ndani yao,pia hujifunza toka kwa wanafamilia AMBAO wamewahi KUWEPO kitengo yaani maisha yao huwa somo kwao HIVYO ni rahisi na wao KUINGIA na kutekelezwa majukumu ya wenye nchi!!
Nimeshangaa na Kusikitika Dr Matola PhD utaratibu huu wa Kimfumo na ambao ndiyo umekuwa ukifanyika na Mataifa makubwa hasa kwa Watu wake wa Intelligence ameshindwa Kulijua.

Mkuu ulichokielezea ni sahihi kwa 95%
 
Kila kazi ina changamoto zake, na kwa kuwa walishakula kiapo, inaonelea itakuwa rahisi zaidi kukisimamia kizazi chao.
Nb: Kama baba na mama wanakula nyama ya punda, ni rahisi pia watoto kula nyama ya punda.
Kwani kiapo ni nini? Ina maana Rais hali kiapo? Wabunge hawali kiapo kiapo? Madiwani hawali kiapo? Wana ndoa hawali kiapo?

Unadhani kina Kigogo, Mwamakula, Lisu, Dr Slaa wanapata wapi Top secret?
 
Hizi nchi za kusadikika hata kazi ya bar maids wanaitana kimchongo.

Zamani special branch ilikuwa inachukuwa yenyewe wanafunzi bright vyuoni, lakini tangu wameingia kizazi cha ubinafsi kitengo kimekuwa ni urithi wa familia.

Hata JWTZ ni hivyo hivyo kila Askari mwenye influence lazima aingize ndugu zake.

Unajuwa tatizo ni nini, ni nchi zilizokosa fursa nyingi za ajira.

Binafsi nilikataa kuingia Jeshi ni nilipewa nafasi za kupendelewa lakini kuishi kwa Amri na kunyenyekea ni kitu siwezi kufanya.
Mbona kama vile kwa huu Mfano wako wa Kazi za JWTZ ni kama vile Umemlenga Classmate wangu SAUT Mwanza ( sasa ni Boss wa Timu ya JKT Tanzania ) ambaye ameingia huko kwa Mgongo wa Baba yake ( sasa ni Boss wa CCM Kiutendaji Dawati la Foreign ) muasisi wa hii Kauli ya Sadism is inevitable when the situation is alarming pale Mwandishi Mmoja wa Habari alipokurupuka na kusema Kifaru cha JWTZ Kimeibiwa?
 
Kila sehemu huwa iko hivyo.mfano ukienda BOT,Tra,ttcl,polis jw,pura,tpdc n.k utakuta wengi wao baba zao au kwa namna moja kuna mtu alimuunganisha huko.hivyohivyo na mawaziri au rais mwenyewe kumpa cheo kama ukurugenzi wa shirika ni kawaida.lakini hii inapatikana Tanzania pekee kwa nchi zenye kijitambua hakuna huo upuuzi
 
Kila kazi ina changamoto zake, na kwa kuwa walishakula kiapo, inaonelea itakuwa rahisi zaidi kukisimamia kizazi chao.
Nb: Kama baba na mama wanakula nyama ya punda, ni rahisi pia watoto kula nyama ya punda.
Wonderful. Najuta kutokuwa na Ndugu yoyote wa Familia huko kwani huenda angekuwepo nami ningekuwa huko.

Hongera zao Walioko huko kupitia Ndugu zao Waliotangulia kuwepo huko.
 
Jipitishe pitishe uko wilayani, wakuu wa mashule, wakufunzi n.k unaweza kubahatisha 😀😀, ila uhuru ni muhimu zaidi kuliko kazi; sasa hivi unaweza kubishana na boss wako, ila kwingine huna huo ubavu ni kutumika as a tool​
 
Kwani kiapo ni nini? Ina maana Rais hali kiapo? Wabunge hawali kiapo kiapo? Madiwani hawali kiapo? Wana ndoa hawali kiapo?

Unadhani kina Kigogo, Mwamakula, Lisu, Dr Slaa wanapata wapi Top secret?
Adhabu ya kila kiapo inatofautiana 😀 , viapo vingine chagua nyeupe au nyeusi
 
Hii ipo kwa nchi ambazo vitengo vyao vilikuwa au vina influence ya kgb. Na kuwekana ndugu inapunguza chance ya mapandikizi au moles ndani ya vitengo kwakuwa atleast background ya mhusika inajulikana kupitia relatives wake. Na kingine in most cases watu hawachagui kujiunga na kitengo .Bali kitengo ndicho kinachochagua wa kujiunga mle.
 
Back
Top Bottom