Kwanini inatumika "Mama Samia" badala ya Rais Samia?

Sioni tatizo lolote mbona kuna mama Michelle Obama, Mama Anna Mkapa why not Rais Mama Samia
 
Je inatakiwa aitwe Raisi Bi. Samia Suluhu?

Ingawa Hapo Bi ni kifupi. Akiitwa Raisi Bibi Samia as you said itaonekana kaitwa Bibi yake. .

Raisi Mheshimiwa Samia ....
 
Mama ni jina, kiwakilishi cha sifa na kielezi. Unapomuita mtu mama inategemeana na mukhtadha unatamka katika mazingira gani. Mama pia ni kisifa kuonesha heshima
 
Pia kuna watu wanaitwa baba mtakatifu, baba askofu, baba mchungaji. Mke wa baba mchungaji anaitwa mama mchungaji, hii kuitwa mama mchungaji haimaanishi mchungaji ni mtoto wake. Mama maana yake ni mtu mwanamke. Ukiita mama mchungaji maana yake huyo mama ni mke wa mchungaji. Hata mtoto mdogo wa kike anaitwa mama kwa kuwa ni mwanamke. Mama ni jina la heshima kwa mwanamke. Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania ni mama yetu mpendwa dkr. Samia Suluhu Hassan, kuna taarifa unaweza ukatamka hivyo ukaeleweka vizuri bila tahsishi
 
Jina lake Samia; kwanini aitwe mama Samia, badala ya kuitwa Rais Samia?

Maana ukisema mama inasimama badala ya mama yake, au mume wake angeitwa Samia (Mrs).
Tfsiri ya mama ni mtu mwenye heshima automatically hauwezi ukamtukana mama yako hauwezi ukajibizana na mama yako wala hauwezi kubishana na mamayako ndio maana Mama Samia amepewa hashima hiyo kubwa ya kuwa mama wa watanzania wote anaefanya maendeleo muda wote kwa ajili ya watoto wake We are so proud of her
 
Hii kitu nilidhani inanikwaza na kunikera pekee yangu. Aiseee hakuna kitu huwa kinanichanya nizime redio, au kubadilisha channel ya tv au kuacha kumsikiliza mtu anayeongea mara tu nikianza kusikia katika matamshi yake anamrefer MHESHIMIWA RAIS kama Mama.

Hapo hapo huwa naingia ukakasi.

Mama sio cheo cha kisheria au kiserikali ni hadhi ya kijamii. Kitendo cha watendaji wa serikali wote kuanzia waziri mkuu kumwita MHESHIMIWA RAIS kwa jina MAMA ni kinyume na katika ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Hakuna sehemu imesema tutampigia kura BABA au MAMA ashike mamlaka ya kuongoza inchi. Bali imeweka bayana tutampigia kura mgombea wa uraisi ambaye atakuja kuwa MHESHIMIWA RAIS.

Sasa majitu mazima mengine ni mazee yamekaza Mama mama mama mama. Huu ni upumbavu na ukiukwaji wa katiba kwa kumtaja kiongozi wa inchi kwa jina ambalo si la kisheria au kikatiba.

Kwahiyo kesho na kesho kutwa tutaanza kuitana waziri mkuu Baba mkubwa, waziri wa mambo ya ndani Mama mdogo, waziri wa kilimo Mjomba, waziri wa tamisemi na naibu wake Wifi na Shemeji. Huu ni Upumbavu. Tuukemee.
 
Rais mwalimu Jk Nyerere.
Rais mama samia. S . H
 
Sasa wewe unaonyesha ni kiasi gani ulivyo na chuki Mama ni jina la heshima zaidi duniani kote na ndio maana limekubalika kwa Rais Samia Suluhu
 
Kwahiyo kikatiba yule samia ni mama au RAIS?
 
Aitwe mama au raisi bado atabaki kuwa mama na mwanamke anaeongoza taifa la tanzania na kaitwa mama kwakua ni mama kama sifa yake kuu hapa duniani
 
Jina lake Samia; kwanini aitwe mama Samia, badala ya kuitwa Rais Samia?

Maana ukisema mama inasimama badala ya mama yake, au mume wake angeitwa Samia (Mrs).
Ni kutokana na kujikomba na ujinsia. Pia, wanaomtukuza. hawajui kuwa wanamzeesha bure
 
Asilimia 95 ya Wanamwita mama katika hali flani ya kujikomba
 
Back
Top Bottom