Kwanini injili ya Barnabas iliteketezwa?

Nimekuuliza ukigundua makosa kwenye kitabu kingine katika biblia yako nacho utakikataa? hapo ndipo penye hoja
 
Unaweza kuthibitisha ni muislamu gani aliandika injili ya barnaba? unajua tatizo lenu WAKRISTO mnajaribu kuikosoa injili ya barnaba sio kwa hoja nzito ila tu kwa vile waislamu wanaisoma injili hiyo, kosoa injili ya barnaba kwa hoja bila kuwatupia lawama zako waislamu sawa sawa
 
Hata hii iliandikwa kuna vitu vimeachwa kwa makusudi sasa nashangaa kwanini wanamnyooshea barnaba vidole wakati hata ishara za Yesu waandishi waliamua kuzitupilia mbali wasiziandike, vipi kama barnaba kaandika yale wengine waliamua kutoyaandika?
YOHANA 20:30
" Basi kuna ishara nyingine nyingi, alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake ZISIZOANDIKWA katika kitabu hiki";

sasa kama kwenye kitabu hiki azijaandikwa , sasa zimeandikwa wapi? ili swali uenda barnaba amelijibu kwakumiletea yale mliyoyaacha kuyaandika ,sasa badala ya kumshukuru mnaanza kumpopoa
 
Nilibahatika kusoma nakala ya injili hiyo na kwa kiasi kikubwa inakubaliana na mafunzo ya Quran. Huenda ni kwa sababu hiyo ndo ikazuiwa isisomwe ili watu wasijewakaona hakuna kupingana katika mafunzo ya imani mbili hizi.
Wachangiaji wengi wanaipinga kwa kule kushabihiana na QURAN , lakini bado sijaona hoja ya msingi
 
Alikaimisha Mamlaka yake kwaKanisa [emoji117] View attachment 894731 umenielewa?
Kama alikaminisha mamlaka kwa kanisa ebu tuambie Nani alimwambia Yohana ASIANDIKE baadhi ya ishara za Yesu na kwanini?
YOHANA 20:30
";Basi kuna ishara nyingine nyingi, alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake ZISIZOANDIKWA katika kitabu hiki";
 
Tofautisha yudas msaliti na Yuda Muinjili [emoji117] View attachment 894775[emoji117] View attachment 894776 Ukristo una Wenyewe sio mnakuwa waongo na kudhania tu [emoji117] View attachment 894783 [emoji53] [emoji12]
Ni kweli kabisa QURAN imeweka wazi dhana ni jambo baya kwa mfano mimi sijui wana wa ZATU walikuwa wangapi kati ya hawa?
EZRA 2:8
" Wana wa ZATU , mia kenda arobaini na watano (945)
NEHEMIA 7:13
" Wana wa ZATU mia nane arobaini na watano"(845)

haya tuambie kwasababu DHANA ni mbaya sasa kati ya EZRA au NEHEMIA nani ametaja idadi sahihi ya wana wa ZATU waliotoka utumwani babiloni kurudi Yerusalem? tutoe hofu tupe jibu sahihi maana nasikia wewe unaongozwa na roho mtakatifu
 
Usianze kutoa malalamiko nimekuuliza , makosa akiandika barnaba ndio unakataa injili yake, vip tukikuonyesha makosa mengine ndani ya biblia utakataa pia kama ulivyoikataa injili ya barnaba? rahisi tu kipi ujanielewa
Nawewe uwe unaelewa.
Chapisho lolote kitaalamu au niite kisomi halikataliwi sababu limeandikwa na nani.
Linakataliwa au kukanushwa sababu ya uhalali au ukweli au ualisia wa kilichoandikwa na/au kukinzana kwa mambo ya kitakwimu, au kijiografia, kifizikia, kihistoria, kikemia au kifalsafa n.k.
Au kutokuwa consistency and conclusive kwa kuzingatia timeline of events.
 
Hivi ndivyo unavyopaswa kujenga hoja na kukosoa.
Sio ile unashikilia sababu ya jina la mtu.
 
Ndio hoja yangu hicho unachotumia kuitoa uhalali injili ya barnaba , mbona utumii kuvitoa uhalali vitabu vingine vyenye changamoto hizo ulizo andika hapo mfano KUKINZANA KWA MAMBO YA KITAKWIMU
baada ya wayahudi kuachiwa mateka huko babiloni walirudi Yerusalem sasa takwimu za EZRA kwa wana wa ZATU ni hizo
EZRA 2:8
" Wana wa ZATU , mia kenda arobaini na watano(945)

lakini NEHEMIA yeye takwimu zake kuhusu huyo huyo ZATU zikawa tofauti
NEHEMIA7:13
" Wana wa ZATU, mia nane arobaini na watano(845)
hapo utaona kabisa kuna kosa la KITAKWIMU sasa kwakosa hili maana yake mmoja kati ya hawa ni muongo kabisaa au wote ni waongo lakini hawawezi kuwa wakweli wote
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Me napenda maelezo yako huwezi kutoa nusu/mkato siku zote!..
Haaahaaa mkuu We sio mtu mzuri kabisa kuna mtu umemkimbiza Jf intelligence cku hizi hapost wala comment!! 😀😀
 
Nina uzoefu mkubwa wa kujenga hoja , mara zote sijengi hoja bila kuangalia msemaji anasema kitu gani
Wewe mshahara unaitaka Injiri gani ?
Hebu tuweke wazi kwanza naona unatumia nguvu nyingi sana kwenye hii hoja.
Nakuuliza tena, ni Injiri gani unayoipenda na kuiamini ?
 
Wewe mshahara unaitaka Injiri gani ?
Hebu tuweke wazi kwanza naona unatumia nguvu nyingi sana kwenye hii hoja.
Nakuuliza tena, ni Injiri gani unayoipenda na kuiamini ?
Mkuu mbona unakuwa mkali mimi najadili kilichopo mezani, ukubwa wa nguvu ninayotumia labda unijuze umetumia kipimo gani?
 
Mkuu labda nirudie tena.... Musa hakuandika kitabu cha Mwanzo bali aliandika "makabrasha" na nyaraka kadhaa kama memoir,sheria za torati na amri kumi za Mungu. Ila hakuandika kitabu chochote maana kitabu cha mwanzo hadi Yoshua kwa ushahidi wa kitheolojia na kisayansi unaonyesha kuwa vitabu hivyo viliandikwa miaka 600 kabla ya kristo ilihali musa alikufa zaidi ya miaka 1000 kabla ya kristo.

Kama unafahamu kitabu alichoandika Musa unaweza kutusaidia hapa je ni kipi na alikiandika lini.... Utakuwa umetusaidia sana.
 
Haaahaaa mkuu We sio mtu mzuri kabisa kuna mtu umemkimbiza Jf intelligence cku hizi hapost wala comment!! 😀😀
[emoji23][emoji23] sasa kweli akaogopa kamtu kama Wick. Ila akili za wabongo mada zake basi ndio wanaona big news kuliko hizi wanazotaka zitoke kwenye bible pekee.
 
Mkuu mbona unakuwa mkali mimi najadili kilichopo mezani, ukubwa wa nguvu ninayotumia labda unijuze umetumia kipimo gani?
Hapana mkuu.
Mi nakufuatilia na kuona unavyochangia.
Naona tu unasema Injiri fulani imekosewa.
Ndio maana makuuliza,
Wewe umeisoma Injiri ipi ambayo ipo sahihi ?
Kama hujawahi kuiona injiri sahihi basi sema tu ili tujue mtazamo wako.
Kwakuwa huwezi kuikosoa injiri fulani bila kuijua injiri ya kweli.
Ndio maana nakuambia kuwa wewe kwa hekima yako unaikubali Injiri gani ?
 
Mkuu.
Katika Kutoka 34, Mungu anamwambia Musa aandike maneno ya Agano lake na Wana wa Israeli.
Nawe unatuambia kuwa Musa aliandika Sheria za Torati na Amri kumi, wakati Torati yenyewe iliandikwa, 600 kabla ya Kristo na Musa alikufa yapata miaka 1000 kabla ya Kristo.
Kwa manano yako Musa alikufa zamani zaidi yaani miaka 1000kk na Torati ikaja kuandikwa baadae miaka 600kk.
Naina jambo hili linafanana tu na walioandika Injiri na nyaraka nyingine za Agano jipya, kwamba wanafunzi na mitume waliandika Injiri ya Yesu Kristo baada ya Yesu mwenyewe kwenda mbinguni.
Huu ukweli unaweza kututhibitishia kuwa Musa alishaandika Agano la Kale ambalo tunaweza kuliita Torati, miaka 600 kabla ya Kristo, kama alivyoagizwa na Mungu katika Kutoka 34, kwa kuwa Sheria za Torati na Amri Kumi alizo andika Musa, ndio Torati yenyewe.
Manabii na Mitume wengine wakaja kuiandika kitaaluma zaidi, kwamba katika kuiandika na kuihifadhi katika vitabu vya kisasa, miaka 400 baadae.
Ndivyo ninavyo elewa kwa mtazamo wangu.
 
Kama alikaminisha mamlaka kwa kanisa ebu tuambie Nani alimwambia Yohana ASIANDIKE baadhi ya ishara za Yesu na kwanini?
YOHANA 20:30
";Basi kuna ishara nyingine nyingi, alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake ZISIZOANDIKWA katika kitabu hiki";

hayo yaliyo Andikwa Yanatosha KUAMINI NA KUFUZU [emoji123] [emoji123] [emoji106] [emoji117]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…