Waislamu huwa ukataa utume wa Paulo kwa kigezo kwamba " Paulo hakuwa miongoni mwa wale wanafunzi 12 wa Yesu ". Kutokuwa moja wa wale thenashara inamfanya Paulo asiwe mtume, na kama si mtume maandiko yake si sahihi kwa maana hakuwa na hiyo mamlaka ya kiutume kuandika hivyo vitabu vikawekwa kwenye Biblia.
Barnaba hakuwa miongoni mwa wanafunzi kumi na mbili, na alikuwa rafiki yake Paulo, kila sehemu alipokwenda Paulo, Baranaba alikuwepo, lakini Waislam kwa akili zao kubwa kupita kiasi wanaona kuwa Barnaba ni mtume na maandishi yake wanapaswa kutumia hadi na Waislamu. Huwa ninajiuliza, kwanini Paulo ambaye hakuwa miongoni mwa thenashara asiwe mtume, na Barnaba ambaye pia hakuwa mmoja wa thenashara ( wanafunzi 12 ) amekuwa mtume hadi anaaandika kitabu kinachopendwa na Waislamu?????. Barnaba ana kitu gani cha ziada????.
Kwa watu wenye akili hawawezi kuamini kile Waislamu wanachokiita "Injili ya Barnaba" kwa sababu Barnaba, mtume Mkristo, hakufundisha vitu vingine vilivyokuwa vinatofautiana na mitume wengine kama akina Paulo, Petro, Yohana n.k. nitatoa ushaudi wa kwamba Barnaba hawezi kufundisha kitu tofauti na Mtume Paulo ( asiyekuwa mtume kwa Waislamu ) ambaye waliongozana kwenda kuhubiri katika miji ya wayunani na pia kubishana na wayahudi wenye imani kali.
1. Paulo alipoongoka kwa mara ya kwanza, alikwenda kanisani Yerusalemu ambapo waumini wote walimkimbia, lakini BARNABA alimchukua akampeleka kwa mitume ( Petro, Yakobo na Yohana )huko huko Yerusalemu. ( Matendo ya Mitume 9:26-27).
2. Kanisa huko Yerusalemu waliposikia ya kwamba mataifa wanaliamini neno la Mungu wakamtuma BARNABA aende Antiokia kuiona hiyo neema, lakini Barnaba alikwenda Tarso kumtafuta Sauli ( Paulo ) akamleta Antiokia, wakakaa wakihubiri na kulifundisha pamoja kwa mwaka mmoja. ( Matendo ya mitume 11:19-26).
3. BARNABA na Paulo walibishana na wayahudi waliokuwa wanataka kuwapotosha wakristo. Mtazamo wa Baranaba na Paulo ulikuwa ni mmoja kuhusu kile walichokuwa wanakiamini ( Matendo ya Mitume 15: 2 ).
4. Paulo analiambia kanisa la Galatia kwamba "Paulo na BARNABA walipokwenda Yerusalemu kwa mitume Petro, Yakobo na Yohana, mitume hawa waliwapa mkono wa kiume wa shirika ili waende kwa mataifa na hao mitume wabaki kwa Wayahudi ( Wagalatia 2:9-10)
5. Baraza la kwanza la mitume wote lilipokaa Yerusalemu, wakapitisha baadhi ya sheria kwa watu wa mataifa, waliwapa Paulo na BARNABA hizo nyaraka wazisambaze kwa makanisa mbalimbali. ( Matendo ya mitume 15:1-35 ).
Kwa mifano hiyo hiyo ni dhahiri kabisa kuwa BARNABA hawezi kuja na injili inayopingana na mafundisho yaliyoko kwenye nyaraka za Paulo, Yakobo, Petro na Yohana. Hiyo Injili ya Barnabas imeandikwa baada ya miaka mingi kupita wakati huo Barnaba alikuwa ameshakufa. Injili ya Barnaba inasadikika kuandikwa mwaka 120 AD, wakati Mtume wa mwisho kufa alikuwa Yohana aliyekufa mwaka 100AD.
Hii injili ya Barnabas iliandikwa na Waislamu wenyewe ili waitumie kupotosha Wakristo wasiojielimisha.