Kwanini injili ya Barnabas iliteketezwa?

Kwanini injili ya Barnabas iliteketezwa?

Ukriato hadi raha kila mtu na injili yke ilimradi tu auze kitabu
 
Viwango viwango KUZINGATIWA alicho andika Barnabas fake ni sawa na baba yake fatuma [emoji53]
Ukisema alichoandika barnaba ni fake inawezekana lakini hakikisha unakuwa na original ISIYOPINGANA , hivyo basi thibitisha hilo
 
Umeandika pumba gani [emoji12]
Ukisema injili ya barnaba ni fake , maana yake kuna ORIGINAL , sasa basi onyesha huo mstari fake wa barnaba halafu onyesha huo mstari ORIGINAL USIOPINGANA na vyanzo vingine humo unaposomaga , hicho kinachokuaminisha kuwa injili ya barnaba ni fake nakunywa maji taratibu wewe jitoe akili
 
Daaa Mkuu umewaza nn mpaka ukagundua kuwa waraka wa barnaba uliteketezwa
 
wewe kipimo chako kujua hii fake na hii original nini? Nimekuwekea mistari KUTHIBITISHA UFUASI WA YESU UNA TBS sirudii Tena [emoji53] sirudii, sirudii tena [emoji12] kukataa dawa kwa mgonjwa ni Dalili ya kifo [emoji15] [emoji12]
 
Barna
Wewe unawezaje kumuwekea mashaka barnaba wakati ata Yohana anathibitisha kuna mambo mengine akuandika , inawezekana ndio hayo ambayo barnaba aliyaandika
YOHANA 20:30
"; Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake ZISIZOANDIKWA katika kitabu hiki";

labda wewe unaweza kutuambia ni mambo mangapi Yohana aliyaacha na kwanini aliyaacha? , kisha ndio uje umjadili barnaba kuhusu yale mambo ambayo hayakuandikwa huko mnaposoma
Barnaba halisi hajawahi kumwona yesu kwa sura ila alihubiriwa na Petro alafu isitoshe huyu barnaba mwarabu hajui chochote juu ya injili na historian + jografia ya Israeli .yaani aya ya kwanza tyu kakosea tena kaenda kinyume na bibilia + Quran pale anaposema Marian ni wa ukoo wa Daudi , aya ya pili wanasema yesu kazaliwa zamani za pontio pilato ilihali hilo sio pilato alitawala miaka 26 baada ya yesu kuzaliwa ,mwandishi wanasema yesu alienda na mashua kutoka yerusalem hadi nazareti ilihali hilo silo
 
Injiri ya Barnaba Sio Injiri ya Kristo na haiendani na Theolojia ya Kristo hivyo haina mashiko kwa Wakristo.
Machache kati ya hayo ni kwamba.
-Mwandishi wake alikuwa na uelewa mdogo sana kuhusu jiografia ya Upalestina.
-Katika sura ya 99:21 mwandishi anaeleza alipanda kwa miguu kuelekea kijiji cha Kapernaumu, wakati kijiji hicho kipo zaidi ya mita 200 chini ya usawa wa bahari.
-katika sura ya 100 mwandishi anaeleza kuwa Yesu Kristo alienda Nazareti kwa mashua wakati kijiji hicho kipo mita 500 juu ya usawa wa bahari,
-Katika sura ya 151 anasema pia kuwa Yesu alienda Yerusalemu kwa mashua ukiangalia ramani inapingana na huo usemi.
-Barnaba ndiye pekee aliyeandika kuwa Mamajusi waliompelekea zawadi mtoto Yesu, walikuwa watu watatu tu, tofauti na Injiri ya Yesu ambayo haijataja idadi ya Mamajusi bali imetaja idadi ya zawadi tatu walizopeleka (uvumba, manemane na dhahabu)
-Katika sura 40:41 Barnaba analitaja jina la tunda la mti wa mema na mabaya kuwa ni tunda la Tofaa, lile alilokula Hawa ktk bustani ya Edeni, wakati kitabu cha mwanzo na Biblia kwa ujumla ambayo ndiyo chanzo pekee cha habari hii, haijataja popote jina la tunda la Tufaa ktk maelezo yake.
-Katika sura ya 54 Barnaba ameitaja Dinari kuwa ina Minuti 60, bila kujua kuwa Minuti ilikuwa fedha ya Uhispania iliyoanza kutumika mwaka 685 baada ya Kristo wakati wa utawala wa Khalifa Abdul Malaki. Enzi za Yesu hiyo fedha haikuwepo.
- Katika sura ya 150 Barnaba anaeleza kuwa Yesu Kristo alizaliwa wakati wa utawala wa Pontio Pilato akiwa kiongozi, wakati ukweli ni kwamba utawala wa Pilato ulianza mwaka 26 na 27 baada ya Kristo kuzaliwa.
-Katika sura ya 97 Barnaba anamtaja Mtume Muhammad kuwa ni Masihi na Yesu anamwita Kristo bila kujua kuwa neno Kristo ni kwa Kigiriki na Masihi ni kwa Kiebrania yakiwa na maana moja.
-Katika sura ya 222 Barnaba anaeleza kuwa Yesu Kristo hakusulubiwa, aliondolewa na Malaika, kisha Yuda alisulubiwa badala yake.
-Katika sura ya 44 Barnaba anaeleza kuwa Ibrahimu alimtoa Ishmaeli awe sadaka katika madhabahu, na anamwita Mungu wa Ibrahimu, Ishmaeli na Yakobo, tofauti kabisa na Mwanzo 22.
-Katika sura ya 192 Barnaba anasema Mwishmaeli ndiye aliyeiandika Torati.
-Barnaba anamweka mtume Muhammadi kama mbadala wa Yesu kristo, angalia sura ya 44, 45, 9, 112, 39 na nyinginezo ktk kitabu hicho.
{ hii ndiyo injili mnayoipigania iwekwe kwenye Biblia takatifu ? }
Katika ukweli huu mchache nadhani wasomaji mmeelewa mlengo wa Injiri ya Barnaba wala sina haja ya kuwaambia.
Injiri iliyowekwa katika biblia inaeleza wazo moja (maudhui yanafanana) ingawa inatofautiana maneno kutokana na mazingira ya kila mwandishi alivyofunuliwa na Yesu mwenyewe, tofauti na Injiri ya Barnaba.
[ Ndio maana kuna msemaji mmoja hapo juu nimemwambia, kama anaihitaji Injiri ya Barnaba, inapatikana madukani, akainunue na kuitumia ]

Hapo zamani za kale, kuna mtume mmoja alitokewa na kiumbe asichokijua, kwenye pango, na bila ya kujitambulisha kwamba kiumbe hicho ni kiumbe gani. Ghafla kikamkaba Koo na kumwambia " SOMA "
mkuu ni karatasi mbili tu ndizo zilizobaki pekee sasa wewe hizo sura zote umetoa kwenye injili ya barnaba ipi??
 
Daaa Mkuu umewaza nn mpaka ukagundua kuwa waraka wa barnaba uliteketezwa
gospel of barnaba iliteketezwa mkuu so nilikua na maswali mengi kwanini iteketezwe na karatasi mbili pekee ndizo zilizosalia moja kwa lugha ya kitaliano na moja ikiwa kwa lugha ya kispanish sasa mimi nashangaa baadhi ya watu wanakuja na misura kibao wakidai kua ndio injili ya barnaba wakati imethibitishwa ni karatasi 2 ndio zimesalia
 
mkuu ni karatasi mbili tu ndizo zilizobaki pekee sasa wewe hizo sura zote umetoa kwenye injili ya barnaba ipi??
Nan kakuambia imeteketezwa ? Ipo ila ndio ina pumba nyingi kwanza inaonekana barnaba anaongea na yesu ilihali hawajawahi kutuna
 
wewe kipimo chako kujua hii fake na hii original nini? Nimekuwekea mistari KUTHIBITISHA UFUASI WA YESU UNA TBS sirudii Tena [emoji53] sirudii, sirudii tena [emoji12] kukataa dawa kwa mgonjwa ni Dalili ya kifo [emoji15] [emoji12]
Hii sio njia ya kukwepa maswali , lazima utoe majibu kwa ulicho ulizwa kijana, Yesu hakuandika hizo injili kabisa ni watu wengine kabisa walioandika, hivyo basi ukisema ya barnaba ni fake ni lazima uwe na ORIGINAL , ambayo wewe na wenzako mtaileta hapa kupinga kile alichokiandika barnaba(Kwa lugha laini namaanisha nukuu kwa nukuu) , mbona ni rahisi tu unakimbia kimbia kitu gani ?
 
Barna

Barnaba halisi hajawahi kumwona yesu kwa sura ila alihubiriwa na Petro alafu isitoshe huyu barnaba mwarabu hajui chochote juu ya injili na historian + jografia ya Israeli .yaani aya ya kwanza tyu kakosea tena kaenda kinyume na bibilia + Quran pale anaposema Marian ni wa ukoo wa Daudi , aya ya pili wanasema yesu kazaliwa zamani za pontio pilato ilihali hilo sio pilato alitawala miaka 26 baada ya yesu kuzaliwa ,mwandishi wanasema yesu alienda na mashua kutoka yerusalem hadi nazareti ilihali hilo silo
Lete vifungo vya barnaba ambavyo wewe unaona sio sahihi , halafu lete vifungu ambavyo wewe unaona ni sahihi (kifungu kinapingwa kwa kifungu ) , karibu sana
 
Injiri ya Barnabas haijateketezwa na ipo mitaani inauzwa na wala haijapigwa marufuku na taasisi yoyote, kama kitabu cha Aya za Shetani.
Kama unaihitaji unaweza kuinunua na ukaisoma na kuifuata bila bigudha yoyote ile kama unaipenda.
Wewe unayo?
 
Hii sio njia ya kukwepa maswali , lazima utoe majibu kwa ulicho ulizwa kijana, Yesu hakuandika hizo injili kabisa ni watu wengine kabisa walioandika, hivyo basi ukisema ya barnaba ni fake ni lazima uwe na ORIGINAL , ambayo wewe na wenzako mtaileta hapa kupinga kile alichokiandika barnaba(Kwa lugha laini namaanisha nukuu kwa nukuu) , mbona ni rahisi tu unakimbia kimbia kitu gani ?

Hicho Kitabu choote hakuna mlingano na Vitabu vingine [emoji12] huyo alikuwa anasimulia isa aliye zaliwa chini ya mtende na Tangazo lake la kuzaliwa lilitoka chini KUZIMU [emoji117]
IMG_20181009_140431_001.jpg
kinyume Kabisa na Waandishi wengine wa Biblia Takatifu [emoji15] [emoji12]
 
gospel of barnaba iliteketezwa mkuu so nilikua na maswali mengi kwanini iteketezwe na karatasi mbili pekee ndizo zilizosalia moja kwa lugha ya kitaliano na moja ikiwa kwa lugha ya kispanish sasa mimi nashangaa baadhi ya watu wanakuja na misura kibao wakidai kua ndio injili ya barnaba wakati imethibitishwa ni karatasi 2 ndio zimesalia

Nani kaiteketeza!? Wapi!? Kabla au baada ya Baba yake fatuma?!

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Baada ya kuonekana iko tofauti sana na injili nyingine ndo mana ikapigwa marufuku. Hiyo injili huumiwa sana na waislam katika baadhi ya mandiko ku support Quran kwani yaongelea ujio wa mtume Muhhamadi na kutouliwa kwa Yesu msalabani.

Kama umuelewa unaeza gundua hizi dini ni miradi ya watu ili kutuweka akili zetu ndani ya BOX.
Hebu tupe hiyo mistari mkuu
 
Back
Top Bottom