Mr Chromium
JF-Expert Member
- Aug 20, 2020
- 2,761
- 3,835
Humu jukwaani, kunapotokea ubishi wenye mwelekeo wa "Kimataifa", utaukuta ni baina ya Mkenya na Mtanzania.
Lakini inafahamika kuwa Jumuia ya Afrika Mashariki ina nchi kadhaa zaidi ya Kenya na Tanzania. Kwa nini ubishani wa kiutani uwe ni kati ya Mkenya na Mtanzania na siyo na Mtanzania na raia wa nchi zingine za East Africa?
Je! Inaweza ikawa,
1. Watanzania wanawahusudu Wakenya?
2. Wakenya wanawahusudu Watanzania?
3. Kwa sababu lugha kuu inayotumika humu jukwaani ni Kiswahili, lugha inayoongelewa zaidi Tanzania na Kenya?
4. Watanzania wanawaamini zaidi Wakenya kuliko wana Afrika Mashariki wengine?
5. Watanzania na Wakenya wana uasili wa karibu zaidi kuliko wengine?
Kwa nini imekuwa hivyo?
Sababu ni kua Kenya na tanzania tunaelekeana vitu vingi
Lugha kiswahili
Uchumi una karibiana
Ukubwa wa ardhi
Hapa hatuwezi kujiringanisha na mikoa kama rwanda na burundi ??? wenye GDP ya single digit
au na failed state kama somalia??
Uganda ndio atleast inaweza ingia kwenye hii game! ila ndo inajiona nyonge
kwanza imeji isolate
Hawajui kiswahili
Masikini
Na hawana tumaini la kuipiku nchi hata moja kat ya hizo mbili
Lakini mwisho ni democrasia
Uganda na rwanda ni nchi za kidikteta wataongea nini hapa nchi zimemilikiwa na koo au mtu mmoja itakua ni humiliation