Hii kitu sijai-notice Mara moja ,nime-notice mara nyingi sana, utakuta unapiga story na baba mkubwa, anakwambia yule mke wa mdogo wangu anachosubiria ni pensheni tu ya mdogo wangu wa kiume.
Au mkaka in his early 30's akioa, utaskia mama MTU mzima akisema, huyo mdada ameolewa kwasababu anataka nyumba ya yule mkaka.
Utakuta mwanaume ana-date na Mwanamke, halafu ndugu wa mwanaume wanaanza kusema kuwa huyu Mwanamke kaja kufuata pesa tu kwa kaka yetu
Na matukio meengi mengine yanayofanana na hayo.
Watu wa nje wanajuaje kuwa alichofuata huyo Mwanamke kwenye mahusiano ni pesa, wakati wao hawako ndani ya hayo mahusiano?