Kwanini Jeshi imara kama Israel halina 4 stars General?

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
10,406
Reaction score
19,892
Nilikua naangalia vita inayoendelea huko 'Middle East' kati ya Israel na wapalestina.

Nimegundua Jeshi la Israeli halina Four Stars General, Mkuu wa Jeshi la Israeli ni Lieutenant General (3 Stars General)

Kwa nin iko hivyo na wakati Majeshi ya Kiafrika ambayo ni very weak lakini yana mpaka Marshall?
 

Yawezekana majeshi yetu Kibongo bongo yako vizuri zaidi. 😂😂😂😂😂!
 
Israel upewi nyota au kupandishwa cheo kwa kukaa darasani au kisiasa,kule lazima ufanikishe mission maalum,au upate mafunzo yahari ya juu kiasi fulani,
Waziri mkuu wa sasa hv ni komandoo,special forces,alishiriki kwenye operation ya entebe ya kuokoa wanaisrsel waliokuwa wametekwa.
Sio hapa kwetu ukikuta general ana likitambi kama pipa,hajawahi kwenda kwenye mission yoyote,zaidi ya kukaa ofcn,kuingiza ndugu zake jeshini,na kula rushwa tu.
 
Israel hawatumii neno General wala zile ranks za Western military hutozikuta. Wao rank yao inayofanana na General inaitwa Rav Aluf ambayo hutumika kwa forces zote za jeshi. Tofauti na General inayotumika kwenye Army, Admiral inayotumika kwenye Navy na Marshall kwenye Air Force.

Nchi nyingine kama North Korea pia hazina ranks kama hizi tunazojua. Ndio maana NATO wana rank zenye namba badala ya majina kama General, unakuta cheo kutoka North Korea kimepewa namba sawa na labda Lieutenant General basi unajua hivi vyeo ni sawa.

Israel imekuwa na Rav Aluf kadhaa kina Moshe Dayan na wengineo
 
Hapo sawa wabongo wakikaa ofisini ya Yani Hadi kelo. Wanajaza matumbo na ndugu zao
 
Israel viongozi wake wa jeshi huwa wako competent mno sio kama Nigeria uko. Hata Ufaransa ile vita ya pili ya dunia walikuwa na majenerali hamna kitu mpaka alipojitokeza Charles de Gaulle akiwa uhamishoni
 
Nikusahihishe kidogo yule wa mission Entebbe ni kaka wa huyu kwa jina Jonathan Netanyahu. Na alipoteza maisha yake hapo hapo Entebbe
 
Safiii..
 
Ina maana mkuu Netanyahus kule Entebe walikuwa wawili? Yona Netanyahu alikuwepo na ndiye aliyeuwawa kwenye tukio hilo. Vipi kuhusu Benyamini naye alikuwepo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…