Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Moyo wangu unaumia sana,unasononeka sana ,una uchungu sana ,una vuja machozi ya hasira kuona,kutizama,kusoma Mdude Nyagali akitumia lugha chafu kumdhalilisha Rais wetu.Kwanini jeshi la polisi Mnamuacha na kumtizama Mtu huyu akiendelea kumdhalilisha Rais wetu kiasi hiki? Mnataka mpaka aseme nini na atumie lugha gani kumdhalilisha Rais wetu ndio mchukue hatua? IGP upo wapi mzee wangu?
Huoni? Huguswi? Unaona ni sawa? Ni kawaida? Ni demokrasia? Kwanini ukae kimya wakati Rais wetu ana dhalilishwa kiasi hiki? Mtu huyu kwamba amekushinda wewe na jeshi lako kumchukulia hatua Kali za kisheria? Yaani Mdude mtoto mdogo akae akimdhalilisha Rais ,mkuu wa nchi? Kiongozi wa serikali na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama? Huku wewe ukiwepo Ofisini? Rais Wa Nchi Adhalilishwe kiasi hiki? Kwanini iwe hivi? Mnamuogopa? Kwa lipi? Kwa kipi?
Hamuoni lugha anayotumia ni ya kutweza utu wa Mheshimiwa Rais? Naomba niseme kuwa Watanzania tunapenda na tungependa demokrasia ,uhuru wa watu kuzungumza na kutoa maoni yao vinaendelea kushamiri hapa Nchini kwa afya ya Taifa letu na maendeleo kwa ujumla wake.
Lakini uhuru wa kumdhalilisha Rais wetu,kumtukana,kumshushia heshima haikubaliki hata kidogo,haivumiliki wala haipendezi wala hakuna mtanzania anayeweza kupenda kuona matumizi ya lugha chafu unaofanywa na Mdude Nyagali kwa Rais wetu.watanzania tunapenda ustaraabu , kuheshimiana,kukosoana kwa hoja na kukubaliana kutokukubaliana kwa lugha za kiungwana kabisa.
Hivi kweli mtu aliyepata malezi mazuri ya mama yake au wazazi wake,akakua katika mazingira na malezi yenye kumheshimu mkubwa wake au mtu yeyote yule pamoja na kuwa na hofu ya Mungu,anaweza vipi kutumia maneno na lugha chafu atumiazo Mdude? Ni kweli amewahi kukiri kuwa Mama yake alikufa zamani akiwa mdogo ,lakini mbona wapo watu walizaliwa na mama zao wakafa wakiwa bado wadogo lakini wana maadili mazuri na hawajazibuka na kukosa staha,adabu ,maadili na hekima kama alivyo Mdude Nyagali?
Mdude Nyagali ni mtu aliyekosa adabu,staha,hekima na busara.Ni mtu mropokaji na mkurupukaji tu. Ni mtu ambaye ni kama akili yake alishakatika kabisa mishipa ya fahamu,ni mtu ambaye ni kama ameshaathirka kisaikolojia.
IGP mzee wangu hii haikubaliki kabisa kuona Rais wetu akiendelea kudhalilishwa pasipo kuchukuliwa kwa hatua kwa wahusika aina ya Mdude.inaleta hasira na kuchochea chuki. Tunahitaji ukosoaji lakini siyo udhalilishaji na matusi kwa Rais wetu. Ni nani mwenye akili Timamu na anayejitambua anaweza kufurahia na kuunga mkono ayafayayo Mdude? Hapana hii haiwezekani hata kidogo.na kama tukiacha utamaduni huu wa kumdhalilisha Rais wetu ukaendelea utajenga picha mbaya kwa vizazi vijavyo.ni lazima tujenge Taifa linalojali utu wa mtu na kuheshimiana hata kama tunatofautiana Mitizamo.
Sitaki kuweka maneno aliyo tumia maana itakuwa ni kuendelea kumdhalilisha Mheshimiwa Rais wetu.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.