Heshima yako Big sisy,
Mie kuna mdada hapa oficn ilikuwa kila tukiwa free yeye yuko bize na komputa,
Na akianza kucheka utafikiri anatekenywa,kwavile namie napenda kucheka nikawa namuuliza huwa anacheka nn,
Akanifungulia jukwaa la jokes na mie nikawa nacheka sn yani kila nikipata mda naingia km msomaji,
Ikatokea siku kuna mada uliandika ww mmu(Siikumbuki) yule bidada akaisoma then badae akanambia kuna mdada anaitwa Ashadii yani huwa anaandika vitu vya ukweli,
Mie wala sikuhangaika ikawa anafatilia post zako alafu anahadithia,
Hapo ndio nikataman kufungua MMU,khaaaaa nikakutana na uzi wako wa "Do you Feel LOVED"
Siku hiyo ilikuwa km wiki 2 tayari tangu uandike,niliposoma nilifurahi sana watu walivyokuwa wakifunguka,
Sikukufikiri mara mbili ndio nikaamua kujiunga rasmi tar 26 sep.2011,
Na mpaka leo naenjoy kuwa JF.