Asha,awali ya yote ngoja kwanza nikumwagie misifa mitatu muhimu:
1. Unajituma. Kukandamiza mi post zaidi ya alfu mbili ndani ya siku 45 si mchezo mwanawane.Wengine tuko humu toka 2008 hata post alfu moja hatuna.
2. Unathamini mamemba. Siku 45 umemwaga mi senks zaidi ya mia nne,si haba.Mi likes ndo usiseme,kwa niaba ya ma memba wenzangu woooooote pokea li senks na li likes hilooooooooo mmmmwwwwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!
3. U msikivu. Iko siku niliku PM nikakushauri kitu na kwa unyenyekevu ukafuata ushauri wangu,wakati na ku PM nilidhani ungenibararusha si unajua tena mambo ya 'kupotezea'?
Ndugu Asha baada ya utangulizi huo naomba nirejee kwenye mada. Nakumbuka kuna siku nilikuwa napata supu asubuhi maeneo ya Kinondoni. Kipindi hicho ndo issue ya ufisadi wa meremeta imepamba moto.Basi bwana mmoja hapo kijiweni akawa anamsifia mtu anaitwa Mwanakijiji kuwa huyo jamaa kwa kuporomosha mabomu Lyatonga Mrema cha mtoto.Nikamuuliza Mwanakijiji ni nani?,akanishangaa kweli na kuniuliza 'we humjui Mwanakijiji?' nikamwambia simjui,akasema ingia website inaitwa JamiiForums utakutana naye. Nikaingia na kwa kuwa lengo lilikuwa kumsoma Mwanakijiji moja kwa moja nikagota jukwaa la siasa,mwanzoni nilichangia sana tu pale hadi nilipoanza kusikia kizunguzungu nikiingia humo, nikaona mmmhhh nitadata bure ndo nikatafuta jukwaa jingine.Naomba nikiri kuwa toka niingie MMU roho yangu imekuwa bariiiidi na siku ikipita sijaingia naona ka vile ntaumwa.Nawashukuru sana wana MMU kwa michango yenu na kikubwa zaidi namshukuru..........ambaye tumefahamiana humu MMU (mambo ya PM) hadi kuuuuuuu.........
Wasalam,
Wako mwaminifu,
Bishanga Abashaija.