Asha,awali ya yote nikumwagie misifa mitatu mikuu:
1.Unajituma.Post zaidi ya alfu mbili ndani ya siku 45 si mchezo mwanawane.Wengine tuko humu toka 2008 hata post alfu moja hatuna.
2.Unathamini mamemba wenzio. Ndani ya kipindi kifupi ushamwaga mi semks zaidi ya mia nne na mi likes kibao.Kwa niaba ya ma memba wote nasema senks mmmmmwwwwwaaaaaaaaa!!!!
3. U msikivu. Kuna siku nili ku PM nikakupa ushauri,uliutekeleza.Kusema kweli wakati natuma PM nilidhani ungenipotezea(kwa lugha ya MMU)!
Baada ya utangulizi huo turudi sasa kwenye mada.
Mimi nimeijua JF wakati niko kijiweni napata supu na siku hiyo tukawa tunaongelea skendo ya meremeta,ndo hapo jamaa mmoja akawa anamsifia mtu anaitwa Mwanakijiji kuwa huyo jamaa kwa kumwaga upupu ni hatari.Nikamuuliza 'Mwanakijiji ni nani?' jamaa alinishangaa kweli akaniuliza yaani we Bishanga hujui website ya JamiiForum,humjui Mwanakijiji? Ndo kutokea hapo nikaigugo JF na kwa kuwa lengo lilikuwa ni kumsoma Mwanakijiji basi tokea mwanzo niligota kwenye jukwaa la siasa na nikawa nachangia sana.Lakini kama mnavyolijua jukwaa lile,yataka moyo kudumu pale.Nilipooona maji yamezidi unga ndo nikajimuvuzisha MMU,sijawahi kujutia maamuzi hayo na kusema kweli nikiingia MMU roho yangu inakuwa bariiiiiiidi na kikubwa zaidi kupitia MMU( mambo ya PM) nimeweza kufahamiana hadi kukutana na........................ hadi tukaaaaaaaaaa,,,,,,,,,,,,
Wasalam,
Wako mtiifu
Bishanga Abashaija.